Nawaomba radhi wana CHADEMA, nilimwelewa vibaya Mhe. Mbowe - Pasco

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,450
Mkuu sana Mhe. Regia Mtema,

Heshima mbele!.

Kwanza samahani kuchelewa kuomba radhi, nilikuwa nasubiri ile hansard uliyoahidi, ili nijiridhishe, nilimwelewa vibaya Mhe. Mbowe.
Baada ya kusoma michango mingi humu jukwaani kuhusu hoja hii, nimeona sina sababu ya kuendelea kuisubiria hiyo hansard, hivyo ninatumia fursa hii kwa kusema yafuatayo kwa dhati ya moyo wangu

Mimi Pasco wa JF, "Nawaomba Sana Radhi Wana CHADEMA, Nilimwelewa Vibaya Mhe. Mbowe".

Nawaomba radhi kwa dhati ya moyo wangu, wale wote waliofedheheshwa na uelewa wangu.

Kwa vile sisi ni binadamu na tumeumbwa tofauti, hivyo tofauti za uelewa kati ya mtu na mtu ni kawaida, hakuna binadamu mkamilifu, kufanya makosa ni jambo la kawaida na kuombana misamaha pale mnapotofautiana pia ni kawaida, hivyo samahani sana.

Msamaha huu nimeufungulia thread inayojitegemea, ili niweke na chanzo cha uelewa wangu huo uliopelekea kumwelewa vibaya Mhe. Mbowe hivyo kutoa fursa kwa Chadema, kutuelewesha vizuri kusije jitokeza mikanganyiko kama hii kwa siku za usoni.
Utangulizi
Baada ya kumalizika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, kilitangazwa kutokuridhishwa kwake na jinsi zoezi zima la uchaguzi lilivyoendeshwa, hivyo wakakataa kuyakubali matokeo ya kura za urais na kutangaza rasmi kutomtambua mshindi.

Binafsi sikukubaliana na msimamo wa Chadema na niliandika humu jamvini kwanini sikukubaliana nao. Tangu mwanzo wa mchezo, Chadema wakijua wazi, the playing ground is not level, lakini walikubali kuingia uwanjani na kupambana hivyo hivyo, huku mmoja ameshika mpini, ungetegemea nini?.

Chadema walikubali kutia saini kanuni za mchezo, hivyo sio busara kuja kukiuka kanuni hizo kwa kukataa matokeo, ndio maana kwa maoni yangu nilisema, the right forum kwa Chadema, kuyakataa matokeo, ni kufika siku yanatangazwa, kususa kusaini na kuwaeleza Watanzania sababu, ikiwemo kutomtabua rais, unamweleza pale pale in front of his face, na jamii yote ya kimataifa.

Kwa kutomtambua rais, Chadema walitoka nje siku ile rais akilihutubia Bunge.
Kilichotokea
Ulipowadia wakati wa kuchangia hotuba ya rais, waliosusa kuisikiliza, nilitegemea Chadema, wangenyamaza kimya, kuonyesha kuendelea kumsusia rais, au wangechangia bila kumtaja ili kuonyesha kutomtambua.

Kitendo cha Mwenyekiti wa Chadema, kusimama, akaanza kumsifu, kumshukuru na kumpongeza rais Kikwete, mimi nilichanganyikiwa na kuhamanika kwa furaha nikiamini sasa Chadema wanamtambua rais Kikwete ndipo nikapost thread hii
Chadema yakubali yaishe! yamtambua Rais!, yampongeza Rais!. - JamiiForums

Kwenye thread yangu hiyo, chini niliweka angalizo hili
Angalizo!.
Kuna kitu kinaitwa expressly na impliedly!
Expressly ni kwa Mbowe kutangaza kwamba sasa Chadema inamtambua Rais!
Impliedly ni pale Mbowe alipompongeza rais, akamsifu na kumshukuru na kuonyesha spirit ya reconciliation.

Mkubali msikubali, Chadema imemtambua Rais JK impliedly na wamekubali yaishe zaidi ya hapo ni ubishi tuu, vinginevyo Mhe. Mbowe afanye Press Conference afafanue na kukazia kutomtambua JK!


Pamoja na angalizo hilo, haikusaidia watu kunielewa ni mpaka Mbunge wa Chadema, Mhe. Regia Mtema aliponitaka kuomba msamaha kupitia thread hii

Pasco Tuombe radhi CHADEMA-Umemwelewa Vibaya Hon Mbowe - JamiiForums

Hitimisho
Mwanzo niliamini kwa vile Chadema, walitamka expressly kuwa hawamtambui JK, kubadilika na kutamka tena expressly kuwa sasa wanamtambua itakuwa ni kugeuka nyuma na kugeuka jiwe la chumvi, hivyo niliamini wamechukua njia ya ustaarabu zaidi kwa kutosema expressly wamemtambua, bali impliedly kuonyesha kumtambua kwa kauli na matendo na hili ndilo kosa langu, nakubali kosa na naomba msamaha wa dhati.

Natumaini msamaha wangu emeeleweka japo sio lazima ukubalike, tuendelee kuchambua hoja mbalimbali humu jamvini kwa maslahi ya taifa.

Natanguliza shukrani.

Wenu

Pasco.

Angalizo: Pasco wa JF ni mwanachama wa chama cha siasa, ila sio kada, sio mkereketwa, sio mfurukutwa bali ni mshabiki wa demokrasia ya kweli ndani ya Bunge. Principle ya uchangiaji wangu ni kuongea nothing but the truth kwa kuzingatia truthfulness, accuracy, objectivity, impartiality, fairness, na balance nikiweka mbele maslahi ya taifa.
 
content ya hii sredi haioneshi kuwa unaomba msamaha bali unazidi kung'ang'aniza lilelile. Naona umeanzisha hii sredi kujaribu kutushawishi kivingine tuamin jambo ambalo halikufanywa na Mbowe. Hulazimishwi kuomba bali tulijaribu kukuelekeza umeelewa ILA UNAGOMA KURIDHIA.
 
Pasco, mwenye macho haambiwi ona...Huwezi kumuita mtu rais kama sio rais au mke wangu kama sio mke wako. Binafsi sijaona ulipokosea..
 
You have proven Maturity but next time it's better to listen careful to the speaker, understand the words, think critically, analyze the statement in relation to the future and current situation, etc before coming up with your perception. Huwa tunawashauri viongozi wetu wasikurupuke kwenye kutoa statements nadhani hiyo ina apply hata kwetu, TUSIKURUPUKE KISHABIKI.

Otherwise let's join our hands for the TANZANIA we want
 
Hongera kwa uungwana na udhati wa kauli yako, uungwana ni sehemu kuu ya hali ya UTU WA MTU.
Daima ubaki katika imani ya UUNGWANA & UKWELI.
 
MSAMAHA SIO SABABU YA KUFANYA KOSA,
WATANZANIA WENGI WANA FANYA MAKOSA MAKUSUDI KWA SABABU WANATEGEMEA KUOMBA MSAMAHA SAAS HILI NI TATIZO NA MIMI SIKUBALIANI NALO

JITAHIDI ,KUWA MAKINI,FANYA UCHUNGUZI WA KINA KABLA YA KUSEMA AU KUANDIKA CHOCHOTE,KWANGU MSAMAHA SIO TIBA KWANI HATA POLISI WETU WANAUA HALAFU WANAOMBA MSAMAHA SASA HII INA FAIDA GANI KWA MAREHEMU

badilika msamaha sio TIJA
 
Mimi nimesoma mstari ulioomba msamaha tu, blah blah nyngne hazina nafasi, maana ni MARUDIO ya misimamo yako ya tangu dahari.
Kwenye msamaha tusiendeleze ligi ya kuongea,..aksante.
 
I wish waandishi wote wangekuwa kama wewe, wasiofungamana na chama chochote cha siasa, wenye kuzingatia truthfulness, accuracy, objectivity, impartiality, fairness, na balance nikiweka mbele maslahi ya taifa, tungefaidika sana kupata habari za uhakika zisizo na upendeleo wala chumvi. I LIKE YOUR APPROACH - Big up Pasco.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom