Paschal aliona mbali sana kuhusu hamahama ya CHADEMA

MKEHA

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
714
1,137
Kuna wakati Paschal Mayala aliutahadharisha umma wa Tanzania na dunia hususani wapenzi,mashabiki na wanachama wa CHADEMA kwa trend ili ya wabunge na madiwani kukihama chama hicho. Mwanzoni tulimwona kama mnoko aliyetumwa na wasiokipenda CHADEMA.

Sasa kwa yanayoendelea hasahasa baada ya kuisikiliza hotuba ya Lijuakali nimeanza kumwamini Paschal kwamba pengine aliona mbali kushinda wengi. Kina shida mahali ndani ya CHADEMA hata kama ukweli huu utakuwa mchungu.

Kiwango cha majonzi aliyoonyesha Lijuakali kinatupa somo flani. Lakini pia hotuba mbali mbali za Silinde zimekuwa na mambo ya kutafakarisha sana.

Kama wabunge vijana ambao hawakuwa na dalili za kuhama wala kusaliti chama wamefokia uamuzi wa kwenda kinyume na.msimamo wa chama na mwenyekiti Mbowe hili swala ni RESEARCHABLE.
 
Why Mbowe kila siku mgombea pekee wa wa uenyekiti?
Why wabunge wanakatwa hela na chama kinapokea ruzuku?
Maswali Chadema ni mengi sana..

Hata kama CCM Wana hila na wanatumia Dola kuiua Chadema bado Chadema wenyewe wanafanya mambo ya kujiua pia
Inawezekana wanakatwa hiyo hela kulingana na makubaliano kama wanavyosema nia yao ni kuitumia kuimarisha chama.
 
Tatizo moja tu ambalo naonaga walalamishi wa Chadema wanakosea ni kwamba Je tunawalinganisha na Chama gani? maana kila Chama kina matatizo makubwa
 
Mie sio chadema but wengi waliohama chadema ni kwa sababu ya upeo mdogo wa akili au sababu ya tamaa ya pesa au madaraka
 
Why Mbowe kila siku mgombea pekee wa wa uenyekiti?
Why wabunge wanakatwa hela na chama kinapokea ruzuku?
Maswali Chadema ni mengi sana..

Hata kama CCM Wana hila na wanatumia Dola kuiua Chadema bado Chadema wenyewe wanafanya mambo ya kujiua pia
Chama kinapata ruzuku lakini mahitaji ya chama ni makubwa kuliko ruzuku. Kumbuka kuwa chama bado ni kichanga kinahitaji kujengwa.
 
Chama kinapata ruzuku lakini mahitaji ya chama ni makubwa kuliko ruzuku. Kumbuka kuwa chama bado ni kichanga kinahitaji kujengwa.
Na wakukijenga awe mbowe Tu Kwa miaka zaidi ya 20?

Na wote wanaolalamika hawaelewi umuhimu WA kujenga chama?
 
Chama kinapata ruzuku lakini mahitaji ya chama ni makubwa kuliko ruzuku. Kumbuka kuwa chama bado ni kichanga kinahitaji kujengwa.

More than 20 years unasema chama kichanga? Badirisheni mwenyekiti wenu ambaye ni opportunistic ndipo mtashudia mabadiriko
 
Hakuna asie jua Mboe ni homa ndani ya ccm,sasa kinachofanyika ni kuwaamnisha watanzania waaiojielewa na wasiokwenda shule kuamini kuwa Mboe ni tatizo kumbe ni mbinu za mafisi kutaka Mboe aachie kitu wamuweke mtu wao,sasa kama kweli Chadema inakufa na hao wanaondoka wamemchoka Mboe mwambieni babaenu aruhusu mikutano ya nje muone kijani ina dhamani gani au CHADEMA imekufa au la
 
Back
Top Bottom