Edward Lowasa uliona mbali, ushauri wako unaitesa CHADEMA

Edward Lowasa uliona mbali, ushauri wako unaitesa CHADEMA

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
3,889
Reaction score
8,487
Mara baada ya Waziri Mkuu Msitaafu Edward Lowassa kujiunga na kuinunua CHADEMA ili awe mgombea urais mwaka 2015 , kitu cha kwanza kabisa alipokabidhiwa tu chama alipiga marufuku siasa za kiharakati na kushauri siasa hizo hazina tija kwa sasa. Edward Lowassa alionya kuwa CHADEMA lazima igraduate kutoka chama cha kiharakati hadi kuwa chama cha siasa sasa.

Edward Lowassa alifafanua madhara ya chama kubaki cha kiharakati muda wote kuwa ni pamoja na kupinga maendeleo yote ya nchi ,kuombea mabaya nchi ,kushirikiana na mabeberu ili kuiibia nchi ,pamoja na kushangilia kila lililobaya kwa taifa ili kumfurahisha tu anayefadhili hizo harakati zako. Matokeo ya harakati hizi ni chama kuchukiwa na wazalendo na kupoteza ushawishi kwa wananchi.

Hakika Lowassa aliona mbali. Leo brand ya chadema imeharibiwa vibaya, chama kilichojizolea umarufu kwa kutetea wanyonge leo kinataka machinga na mama ntilie wafukuzwe mitaani!!! Leo ni furaha kubwa kwa Chadema ndege kukamatwa na wazungu!!!

Mbowe yeye anaona ni jambo la maana sana kulewa konyagi na kuanguka kisha akalitangazia taifa kuwa ametekwa na kupigwa na wasiojulikana.

Mbowe leo hi anaona jambo la maana sana kufungiwa biashara na akaunti zake na familia kisha akalitangazia dunia kwamba amefungiwa akaunti zake na Magufuli!!

Ni aibu kwa chama kikuu cha upinzani nchini kuchangisha wabunge billioni 8 kisha kuziiba kwenye fixed account na kuzitafuna huku chama kikiwa hakina hata ofisi.!

Hayati Rais Magufuli alikuwa akijenga hospitali nzima kwa milioni 400 tu ,hebu jiulize kwenye billion 8 zilizotafunwa , chadema wangejenga ofisi ngapi kwa million 400?

Hali hii haikubaliki ni lazima sasa chadema wapone unyumbu na waanze kuhoji mambo kama haya na kulazimisha hela zirudishwe ili waweze kujenga ofisi za chadema nchi nzima na waachane na utaratibu wa kupanga kwenye mapango ya ufipa na kuishia kufanyia vikao vya kamati kuu kwenye hoteli za kitalii zinazogharimu mabilioni ya shilingi

Pia, Tundu Lissu aelewe kuwa hawezi kuwa rais wa Tanzania kwa kushinda Twitter akikejeli kila lililojema kuhusu nchi yetu

Tundu Lissu atakuwa ameelewa na kupata darasa kwamba ukitaka kupendwa na Watanzania tumikia watanzania na siyo kutumikia Acacia
 
Mkapa ktk kitabu chake anasema CCM ni majizi yaliyo kubuhu. Tulifikiri yanaiba kura tuu kumbe hadi pesa za umma. Samia nae anasema Kuna fadha za umma mmeiba na kuzipeleka uchina kuzificha.
Hangaikia kwanza pesa hizo za umma achana na Chadema.
Wapora pesa za watu wamepeleka China
 
Mkapa ktk kitabu chake anasema CCM ni majizi yaliyo kubuhu. Tulifikiri yanaiba kura tuu kumbe hadi pesa za umma. Samia nae anasema Kuna fadha za umma mmeiba na kuzipeleka uchina kuzificha.
Hangaikia kwanza pesa hizo za umma achana na Chadema.
Unauonaje ushauri wa Lowasa?
 
Naona Mzee wa mashambulizi umerudi kazini kutoka kifungoni. JF walikupumzisha kidogo, tulikuwa tusha-kumiss. Welcome back Mzee wa Mashambulizi. Stories zako huwa tunazijua..We siku zote stories zako ni Mbowe, Chadema, Lissu na Sabaya. Ni rahisi ku-predict utazungumza nini. Ha ha haa.
 
Naona Mzee wa mashambulizi umerudi kazini kutoka kifungoni. JF walikupumzisha kidogo, tulikuwa tusha-kumiss. Welcome back Mzee wa Mashambulizi. Stories zako huwa tunazijua..We siku zote stories zako ni Mbowe, Chadema, Lissu na Sabaya. Ni rahisi ku-predict utazungumza nini. Ha ha haa.
Unaonaje ushauri wa Lowasa?
 
Nikafikiri kuwa unazungumzia siasa za chuki na matusi, nitupie video
 
Ukileta mada inayotaka tujadili kuhusu 1) Namna ya kupunguza ajali barabarani 2) Namna ya kukabiliana na inflation 3) Namna ya kupunguza changamoto ya ajira 4) Namna ya kuongeza uwajibikaji ktk ofisi za umma na kupunguza rushwa 5) Namna ya kufanya kilimo kiwanufaishe vijana wa KiTanzania 6) Namna ya kubana matumizi ya vigogo wa Serikali na kupunguza kodi kwa watu wa chini 7) Namna ya kuimarisha utawala bora 8) Namna ya kuboresha huduma za kijamii zitolewazo na Serikali 9 ) Namna ya kuwafanya waajiriwa wawe na mishahara inayoendana na gharama za maisha 10) Namna ya kuimarisha usafiri wa anga Bongo, unistue.

Ukianzisha mada mojawapo ya hizo nilizotaja au inayofanana na hizo uni-tag mkuu nitakuja kutoa mchango wangu pia.
Jikite kwenye hoja
 
Hata TANU kilianza kama chma cha kiharakati.
Tulieni mtaelewa tu.
 
Back
Top Bottom