Pasaka kwangu bwana, ilikuwa hivi

Pasaka kwangu bwana, ilikuwa hivi

aise

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2018
Posts
8,748
Reaction score
24,532
Kwanza binafsi huwa "sina shobo na sikukuu"
Ila sasa msimu huu nami nikaona si vibaya japo nikienda sawa na wenzangu (Maana ukienda kivyako unaweza onekana ni mchawi)
Basi bwana, nikasema, mimi pia siku ya sikukuu nibadiri japo "Jiko na Chungu"

Kama ada sikukuu ikafika, nikajichomeka sehemu, bwana nakwambia umeletwa msosi mpaka nikajionea aibu. Chakula kimepikwa kikapikika (Tangu kuzaliwa kwangu sijapata kuona chakula cha namna hii)

Yaani nimefukia mpaka nikasema "eeh" kwanza mpaka hapa sijajua kilikuwa ni chakula gani kile?
Maana chakula kile kilikuwa na radha ya
•Samaki walioungwa
•Nyama iliyoungwa
•Mayai yaliyo kaangwa
Halafu kwa mbali kuna harufu flani takribani 6 hivi (Hizo harufu sijawahi kuzinusa popote pale)
Kilikuwa ni chakula gani kile? Mnaweza nisaidia jinsi ya kukiaandaa? [emoji120]
 
Ilikua birian ya Mariam
57204172_136845290781200_3722111947258374116_n.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom