kayanda01
JF-Expert Member
- Feb 14, 2014
- 1,086
- 913
Habari wana JF wote.
Natumai mu wazima wa afya. Poleni na majukumu ya kila siku katika kutafuta riziki ili maisha yaendelee.
Mimi nina shamba kidogo lenye ukubwa wa ekari 3. Eneo lina maji (kisima), na umeme upo (solar power). Halina fence. Eneo lipo kata ya Toangoma (maeneo ya Mbagala - DAR).
Nikafikiria namna ya kulifanya eneo hilo liwe productive. Nimepata idea ya kufanya ufugaji wa kuku. Hata hivyo, changamoto kubwa ni uhaba wa mtaji kuanzisha mradi wa kufuga kuku. Pia sina utalaamu wowote wala uzoefu kwenye ufugaji kuku.
Hivyo, natafuta mtu mwenye uzoefu kamili kwenye ufugaji kuku ambaye yeye labda changamoto ni eneo. Natafuta mtu ambaye ana physical experience kabisa kwenye kufuga kuku na masoko yake. Tufanye partnership, kwa maana ya kwamba mie mchango wangu ni eneo, huyo partner mchango wake ni utalaamu/uzoefu kwenye ufugaji kuku. Pia MTAJI (financial capital) kamili utachangiwa kutoka pande zote mbili nusu kwa nusu (by 50%).
Kuhusu USIMAMIZI wa mradi, itakuwa ni joint supervision, kwamba wote tutashiriki kwenye kuusimamia mradi bila kutegea, na kutafuta soko. Cha muhimu ni kwamba mradi uwe beneficial to both of us. Kama tutaamua kuweka kijana wa kusaidia kazi ama uangalizi, chumba kipo available kimoja kwenye shamba hilo. Mimi ninaishi Mbagala pia, ila sio karibu na shamba husika. So ningependa kupata business-partner ambaye yupo tayari, kwa pamoja, tuji-commit fully kwenye mradi huu.
Kuhusu benefits: Tukishafanya mauzo, MTAJI unatolewa kwanza, tunagawana FAIDA (net profit) nusu kwa nusu (by 50%). MTAJI unaendelea na phase inayofuata. Kama mradi ukienda vizuri, kuupanua zaidi iwe ni moja ya malengo yetu.
N.B: Tutaingia Joint Venture Agreement ambayo ni rasmi kabisa so that to create sense of ownership ya mradi kwa pande zote mbili. So hatufanyi mambo kienyeji !
Wakuu, hilo ndiyo wazo langu. Kwa yeyote who is interested na maelezo hayo, karibu sana tulisongeshe. Pia mpendwa yeyote mwenye constructive advice kwenye hili, karibuni pia mnijenge kimawazo maana penye wengi pana mengi.
Vijana tuungane kujikwamua kimaisha.
Natanguliza shukrani za dhati. Mwenyezi Mungu atubariki sote.