Partnership kwenye ufugaji kuku

Partnership kwenye ufugaji kuku

Mimi nakushairi usistick kwenye ufugaji wa kuku tu. Huenda partner wako akawa na idea tofauti na ya kwako mfano kufuga nguruwe, au hata kilimo cha bustsni. Yaani ninachosisitiza hapa ni kwamba uwe open-minded na idea ya ufugaji wa kuku uiwasilishe kwa partner wako kama wazo tu ili naye awe na nafasi ya kulichanganua. Pia uwe tayari kupokea mawazo mapya maana mwisho wa yote ni pesa haijalishi zimepatikanaje.
 
Nakushauri uanze mwenyewe hata kwa hicho kidogo ulichonacho...utapata uzoefu as you go along. Mi pia nipo kwenye mradi huo nimeenda taratibu sana na sasa nipo kwenye hatua za mwisho. Tatizo la kufanya kazi na mtu mnaweza kurudishana nyuma na hata kuingia kwenye migogoro ya kutafutana ubaya japo Partnership nyingine huwa zinaenda vizuri
Mkuu wewe unafanya biashara ya kuku wa nyama au!?
 
Kama unataka kupata uzoefu anza na kuku wachache ya nyama km 200 , niko tayari kukupa free consultation; nina uzoefu wa 10 yrs sasa nilianza kidogo kidogo lkn nimekuwa naongeza idadi ya kuku wa nyama na mayai na kununua vyakula direct toka viwandani
Mkuu ninaomba nikutafute na mie kwa ushauri hasa kuhusiana na biashara hiyo ya kuku wa nyama
 
Habari wana JF wote.
Natumai mu wazima wa afya. Poleni na majukumu ya kila siku katika kutafuta riziki ili maisha yaendelee.

Mimi nina shamba kidogo lenye ukubwa wa ekari 3. Eneo lina maji (kisima), na umeme upo (solar power). Halina fence. Eneo lipo kata ya Toangoma (maeneo ya Mbagala - DAR).

Nikafikiria namna ya kulifanya eneo hilo liwe productive. Nimepata idea ya kufanya ufugaji wa kuku. Hata hivyo, changamoto kubwa ni uhaba wa mtaji kuanzisha mradi wa kufuga kuku. Pia sina utalaamu wowote wala uzoefu kwenye ufugaji kuku.

Hivyo, natafuta mtu mwenye uzoefu kamili kwenye ufugaji kuku ambaye yeye labda changamoto ni eneo. Natafuta mtu ambaye ana physical experience kabisa kwenye kufuga kuku na masoko yake. Tufanye partnership, kwa maana ya kwamba mie mchango wangu ni eneo, huyo partner mchango wake ni utalaamu/uzoefu kwenye ufugaji kuku. Pia MTAJI (financial capital) kamili utachangiwa kutoka pande zote mbili nusu kwa nusu (by 50%).

Kuhusu USIMAMIZI wa mradi, itakuwa ni joint supervision, kwamba wote tutashiriki kwenye kuusimamia mradi bila kutegea, na kutafuta soko. Cha muhimu ni kwamba mradi uwe beneficial to both of us. Kama tutaamua kuweka kijana wa kusaidia kazi ama uangalizi, chumba kipo available kimoja kwenye shamba hilo. Mimi ninaishi Mbagala pia, ila sio karibu na shamba husika. So ningependa kupata business-partner ambaye yupo tayari, kwa pamoja, tuji-commit fully kwenye mradi huu.

Kuhusu benefits: Tukishafanya mauzo, MTAJI unatolewa kwanza, tunagawana FAIDA (net profit) nusu kwa nusu (by 50%). MTAJI unaendelea na phase inayofuata. Kama mradi ukienda vizuri, kuupanua zaidi iwe ni moja ya malengo yetu.

N.B: Tutaingia Joint Venture Agreement ambayo ni rasmi kabisa so that to create sense of ownership ya mradi kwa pande zote mbili. So hatufanyi mambo kienyeji !

Wakuu, hilo ndiyo wazo langu. Kwa yeyote who is interested na maelezo hayo, karibu sana tulisongeshe. Pia mpendwa yeyote mwenye constructive advice kwenye hili, karibuni pia mnijenge kimawazo maana penye wengi pana mengi.

Vijana tuungane kujikwamua kimaisha.

Natanguliza shukrani za dhati. Mwenyezi Mungu atubariki sote.
Una idea nzuri bro mm nmesomea mifugo tena shahada ya sayansi ya mifugo. Sema elimu ya tz haitujengi kujitegemea bali imetujengea dhana ya kuajiliwa alafu ukizingatia kipind hki cha mpito ambapo hamna ajira.
Ngoja nirejee mafa kuu
Mm wazo langu n kwamba tayarisha mbegu bora ya kuku pind upatapo mtaji maana kufuga kuku kunahitaj chakula bora
Hvyo bas zingatia
Mtaj
Mbegu bora
Dawa ya kuku
Chakula cha kuku well formulated balanced diet
Banda bora
Zen tafuta soko
Bila kusahau kununua vitabu vya ufugaj wa kuku kisasa
Natumai nimejatibu kukupa mwanga
 
Mimi nakushairi usistick kwenye ufugaji wa kuku tu. Huenda partner wako akawa na idea tofauti na ya kwako mfano kufuga nguruwe, au hata kilimo cha bustsni. Yaani ninachosisitiza hapa ni kwamba uwe open-minded na idea ya ufugaji wa kuku uiwasilishe kwa partner wako kama wazo tu ili naye awe na nafasi ya kulichanganua. Pia uwe tayari kupokea mawazo mapya maana mwisho wa yote ni pesa haijalishi zimepatikanaje.

Aiseee ahsante sana mkuu CORAL , umenipa wazo zuri sana kwakweli. Nakubaliana na ushauri wako kaka.
 
Una idea nzuri bro mm nmesomea mifugo tena shahada ya sayansi ya mifugo. Sema elimu ya tz haitujengi kujitegemea bali imetujengea dhana ya kuajiliwa alafu ukizingatia kipind hki cha mpito ambapo hamna ajira.
Ngoja nirejee mafa kuu
Mm wazo langu n kwamba tayarisha mbegu bora ya kuku pind upatapo mtaji maana kufuga kuku kunahitaj chakula bora
Hvyo bas zingatia
Mtaj
Mbegu bora
Dawa ya kuku
Chakula cha kuku well formulated balanced diet
Banda bora
Zen tafuta soko
Bila kusahau kununua vitabu vya ufugaj wa kuku kisasa
Natumai nimejatibu kukupa mwanga

Shukrani mkuu kwa ushauri mzuri. Barikiwa sana
 
NAKODISHA ENEO KWAAJILI YA UFUGAJI LIPO MPAKANI MWA KIBAHA NA KISARAWE SI PORINI NI JIRAN NA CENTER MAJI YAPO KIBAO 0624078252 AU 0764726071
 
Wazima wote? Jaman kuna kipind cha tambuka kinaonyeshwa EATV kuna siku alionyeshwa mjasiliamal mmoja anafuga kuku wa kienyeji na anatengeneza machine ya kutotoresha kwa njia ya asil ni baba. Ambae ana mawasiliaono/namba zake za simu naomba anisaidie.
 
Back
Top Bottom