Wolle Melkas Fernando
JF-Expert Member
- May 4, 2016
- 218
- 297
Namalizia sehemu ya mwisho ya andiko langu lenye kichwa cha Habari hapo juu.
Andiko lililopita nilieleza sisi Watanzania tulivyopambana na mawimbi yote ya maambukizi ya corona na namna wananchi walivyoitikia na nikaeleza kuwa Kati ya njia mbili za kujikinga yaani njia ya Kiasili na ya Kisasa sisi tuliitumia ya asili na ndio maana tulisisitizwa na serikali chini ya Rais Magufuli kwamba tujifukize ama tupige nyungu. Na kwa mujibu wa taarifa ya serikali tulisalimika kwa kiasi kikubwa sana yaani athari zilikuwa ndogo sana.
Sasa tupo WIMBI LA TATU, serikali iliyopo si ile ya WIMBI LA KWANZA NA LA PILI. Serikali ya mama Samia Suluhu Hassan, inapendelea kutumia njia za Kisasa ikienda kinyume na ile ya kwanza.
Njia ya Kisasa hasa ni kwenye uvaaji wa barakoa na Wito wa kupatikana kwa chanjo na kuzitumia. Serikali imeenda mbali zaidi ambapo sasa kupitia Wizara ya afya na viongozi mbalimbali kama wakuu wa Mikoa likiwemo jiji la Dar es Salaam ambalo liko chini ya Amos Makalla, barakoa ni LAZIMA kwenye sehemu ya msongamano.
Tukumbuke tu kwamba serikali ya Magufuli ilichukia uvaaji wa barakoa ikidai kwamba ni kuleta taharuki na kuwatishia watu ingawa serikali haikuzuia uvaaji wa barakoa, watu walikuwa huru kuvaa ama kutokuvaa, serikali ilisisitiza barakoa za kutengenezwa na wananchi wenyewe au zile za MSD zilizotengenezwa Tanzania.
Mpaka sasa Watanzania walio wengi wanaamini barakoa za dukani zina madhara, pili corona haipo, tatu chanjo zote za corona zina madhara na hivyo kusisitiza barakoa na chanjo ni mbinu ya serikali kutaka kukidhi vigezo vya kimataifa ili iweze kuapata mikopo.
Ugumu wa kulazimisha wananchi kuvaa barakoa unatokana na serikali kubadilishia gia angani ya kupambana na ugonjwa huu wa COVID-19 kutoka njia za asili kwenda njia za Kisasa.
Hivyo serikali ikitaka kufanikiwa isiwalazimishe wananchi kuvaa barakoa wala chanjo badala yake itoe elimu ya kutosha na kuwaacha raia wenyewe wachague.
Ikumbukwe kwamba katikati ya WIMBI la KWANZA la corona Rais wa Tanzania hayati JPM, alisema Watanzania wajifunze kuishi na ugonjwa huu kama yalivyo magonjwa mengine kauli ambayo ilifuatiwa na Shirika la Afya Duniani WHO kwamba Dunia ijifunze kuishi na ugonjwa huu kama yalivyo magonjwa mengine kwasababu hakuna matumaini ya kumalizika kwa ugonjwa huu leo wala kesho.
Lakini ni siku moja tu sasa Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema sasa Uingereza itaondoa tamko lake la ulazima wa kuvaa barakoa na kuishi kwa kuzingatia umbali na badala yake watu wajifunze tu kuishi na ugonjwa huu.
Tunasema Ilipotoa mguu Tanzania, Dunia ndio inaweka mguu wake. Tusirudi Nyuma.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.View attachment 1843175