Part 2:mpenzi wangu wa zamani kaokoka

Part 2:mpenzi wangu wa zamani kaokoka

Misa

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2013
Posts
838
Reaction score
135
Jana nilikuja na habari hizo mtu wa zamani kaokoka,watu walitoa comments zao na wengine waligusa penyewe sababu za mtu huyu kuokoka, ila kwa vile kuzitaja hadharani inakuwa sio heshima nafikiri kila mtu ana deserve privacy yake,ila kuokoka huku kwa wadada wa siku hizi tumeona wengi huwa ni sababu zilezile mambo ya maisha,hata huyu mtu aliponiambia ameokoka nilicheka kwanza,halafu ndio akili ikarudi,nikasema kama kaokoka ni sababu ambazo nazijua wazi.Ila jamani hii topic yangu ni kama wosia vilevile hasa sisi kwa wanaume,dunia ya leo sio wanawake wala wanaume hatuna maadili kabisa ya kutafuta mke aka mchumba,mimi naheshimu sana wazee wetu walivyokutana na mama zetu huko bush mpaka wakaoa na wakaanza maisha hawana kitu na wengi wakafika mbali na wakawa succesfull tu,sisi siku hizi tunataka vya kung'aa mtoto unakutana naye barabarani ama bar,baada ya miezi unatuchangisha michango harusi,Common guys!tunachemka wenyewe,ndio huchelewi kusikia majanga baada ya muda na mifano mingi tunaiona humu jf.Wacha niende kwenye topic yangu story isije ikawa ndefu itachosha kusoma,jamani wakaka inabidi tuwe makini, yaani siku hizi sisi wanaume tunavyobambakiwa watoto ambao sio wetu hata wale waliomo kwenye ndoa,mimi haki ya mungu nilishasema nikipata mtoto yaani namchukua taratibu huyo kwenye DNA kieleweke.Nilikuwa na mpenzi fulani wakati tumemaliza secondary nikawa naye kwa kama miaka 2 baada ya hapo tukapotezana kwa miaka 10.Ikatokea kwa sababu moja ama nyingine tukakutana,alifurahi sana na akaanza kuniambia alikuwa anaitafuta muda wote hakujua niko wapi,mh mimi rohoni nikasema huu ni uongo maana angetaka kunipata na kuwasiliana na mimi anajua ndugu zangu na marafiki angewauliza,basi akadai bado ananipenda na anapenda tuwe kitu kimoja,dada wa watu ooh twende tukapime tujue status zetu baada ya hapo tuoane,nikasema rohoni wait a minute! huyu ananiona wa kuja 10 yrs hatujaonana,kuoana?Ni mzuri huyu dada,ukimuona utasema mashallah mungu akupe nini,mke ni huyu na mtoto ni huyu,nikajiuliza rohoni mhh. jiji lote hili kwanini hajaolewa?Maana papa walivyo wengi humu mjini lazima asingekuwepo,basi mimi sikuogopa kwenda kupima, akanichukua kwenda kwenye Hospital anayotaka yeye,ila mimi nilikuwa najiamini status yangu,la sivyo ingekuwa kimbembe kwenda kunitoboa damu yangu hv hv najiona,pressure ya nini maisha yenyewe mafupi,hao tukaenda kupima mimi akili kichwani,tukapima matokeo yakaja fresh,basi nikagegeda mzigo,mtoto wa kike anataka ndoa,turudi nyuma point ni hivi nimemkuta na yeye kaokoka,kanisani kila siku asubuhi kabla ya kwenda kazini,Jamani wacha niikatishe hii story itaendelea baadae leo,muone jinsi wanaume tunavyoingia mkenge.Maadili jamani ya kutafuta mke yazingatiwe wakaka!Mchana Mwema!to be continued...Bon Appetit!!!
 
Agggrr.. tumeshachoka stori hizi za kuendele kila siku
 
Napenda hadithi ila hii nimeshindwa kusoma kwa kweli!!!
 
Sasa hii nayo ni story ya mwendelezo au unalazimisha hako kastyle
 
Sasa hii nayo ni story ya mwendelezo au unalazimisha hako kastyle
si utulie kama inakuboa iache,huyo wa zamani ana 39 yrs,kuokoka si lazima tu mjini.
 
Tunatiana njaa tu hapa daah.
 
misa ndugu yangu ukitaka tukusaidie/nikusaidie we sema tu anasali wapi, tupe tu jina la kanisa lake hapo tutakusaidia, dar kuna makanisa mengine wanajifanya wameokoka wakati wanaruhusu maovu.mf.siloamu
 
kwi kwi kwi utafikiri bongo muvi kila kitu part one na part two? tuwe wavumilivu ni upepo tu utapita.
wacha ni summerise kwako,-Ndoa hakuna mjini,umri umeyoyoma,39 yrs mtoto wa kike,Unamaliza shule unajiamni kazi utapata kesho yake,utembee na mtu wenye ngoma,una la zaidi Demba,ilipunguzwa makali huko juu,usiifuatilie ila ndio hiyo habari
 
kwi kwi kwi utafikiri bongo muvi kila kitu part one na part two? tuwe wavumilivu ni upepo tu utapita.
Upepo utapita tu kweli lakini umri hausubiri,hivi mwanamke ukiwa na miak 39 unaweza kuzaa na huna ndoa,na mume gani utapata?Serengeti,wajane ama anarudi kwa waume za watu tena waliompeleka mpaka akaokoka,waume za watu sumu jamani,mke wake nyumbani anakula maharage na watoto,wewe nyumba ndogo unajirusha guest elfu 50 kwa masaa.Kuokoka huyo yesu tutamsubiri sana arudi.
 
wacha ni summerise kwako,-Ndoa hakuna mjini,umri umeyoyoma,39 yrs mtoto wa kike,Unamaliza shule unajiamni kazi utapata kesho yake,utembee na mtu wenye ngoma,una la zaidi Demba,ilipunguzwa makali huko juu,usiifuatilie ila ndio hiyo habari
mmh mie slow learner kweli jamani hata hapa bado sijaelewa!!!!!. mmh nisikusumbue bana. bye
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom