Paramount Chief Thomas Marealle katika nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama 1950s

Uchaga ni pana sana ikiwa imetawaliwa na Ukristo hivyo siafiki kwamba ushawishi wa huyo sheikh Kirama ulimsaidia Thomas Mareale kushinda uchaguzi.

Ikumbukwe Mareale alikuwa mtu msomi jambo ambalo lilimjengea 'exposure' kwa watawala wa Kiingereza tofauti na Shangali. Ni wazi kwa wapiga kura wa kipindi hicho kuona faida ya kuwa na kiongozi mwenye elimu na ushawishi kwa Waingereza kama Mareale.

Ikumbukwe Mareale kushinda uchagani hajashida kwa kura za wamachame tu, Rombo pia ni uchagani.







Kilicho mpa Mareale ushindi dhidi ya Shangali ni ushawishi wake kwa Wachaga, sio kwa sababu alisaidiwa na Sheikh wa Nkuu.
 
walikuwa wangapi? Kipindi hicho Kilimanjaro hata sasa waislam Uchaggani ni wachache ukiacha upande wa Upareni! Hata sasa nadhani ukristo tena Ulutheri ndo upo zaidi ukifuatiwa na Ukatoliki halafu makanisa chungu nzima ya Kilokole!
 
Who is shekhi Haruna?H

You have minimized your world kama chungu

Can’t even extend beyond your virtual wings
Janja...
Haruna ni Mwalimu wangu aliyonisomesha ilm ya kufanya mijadala na masomo mengine madogo madogo kama mantiki nk.

Hayo usemayo ya udogo wangu ndiyo niliyojaaliwa.
Nashukuru kwa hiki kidogo nilichopewa kwani wapo wadogo zaidi yangu.
 
sawa ila influence huko Machame sidhani kama Uchaggani kotee yaani Marangu, old Moshi na Rombo! Mbona asiwepo kwenye Chagga Council kuna picha za Uongozi wote na Kabunge chao zimo humu JF mzee Kirama hayupo!
 
Under...
Sikusema kuwa Chief Marealle alishinda kwa kuungwa mkono na Mzee Rajabu.
Nimesema kuwa Mzee Rajabu alimuumga mkono Chief Marealle.
 
walikuwa wangapi? Kipindi hicho Kilimanjaro hata sasa waislam Uchaggani ni wachache ukiacha upande wa Upareni! Hata sasa nadhani ukristo tena Walutheri ndo ipo zaidi ikifuatiwa na Ukatoliki halafu makanisa chungu nzima ya Kilokole!
Geza...
Umesema kweli.
 
Under...
Sikusema kuwa Chief Marealle alishinda kuungwa mkono na Mzee Rajabu.
Nimesema kuwa Mzee Rajabu alimuumga mkono Chief Marealle.
Hapa nakuelewa na hata ukisema alimnadi kwa influence yake Machame nakuelewa ila sehemu nyingine sidhani kama Uislamu ulikuwa umejikita hivyo!
 
Hapa nakuelewa na hata ukisema alimnadi kwa influence yake Machame nakuelewa ila sehemu nyingine sidhani kama Uislamu ulikuwa umejikita hivyo!
Geza...
Hali ya Uislam miaka ya 1950 ilikuwa kama hivi:

''Maulid ya Mfungo Sita Moshi Uislam ulipopata nguvu Machame na vijiji vingine Kilimanjaro kwa kuleta walimu kutoka Zanzibar kuja kufundisha dini Usangi, Ugweno na sehemu nyingine za Upare, Maulid yalibadili sura ya mji wa Moshi.

Kuanzia asubuhi mabasi yaliyobeba Waislam yaliingia mjini kutoka milima ya Kilimanjaro na Upare yakiteremsha wake kwa waume na watoto wa madrasa waliokuja maulidini.

Hali hii ilifanya Uislam utawale Moshi mjini ambako ndipo Waislam walipojumuika kwanza katika zafa jioni wakizunguka mjini huku matari yakipigwa na kasida zikiimbwa barabara zikiwa zimejaa watu na mbele zikiwa zimetangulizwa bendera za rangi ya kijana zimeandikwa ‘’La Ilaha Ilallah,’’ yaani ‘’Hapana Mungu ila Allah.’’

Mji uligubikwa na hali ya furaha na misikiti miwili ya Moshi mjini, Msikiti wa Riadha na Misikiti wa Ijumaa ilijaa waumini kuhudhuria sala.''

(Kutoka kitabu cha Rajabu Ibrahim Kirama)
 
Moshi mjini pia kuna Uislam muda ila kumbuka Moshi Town ni part of Old Moshi na density kubwa ya watu ipo nje ya Moshi town! Na pia Moshi town kama makao makuu ya mkoa ni mchanganyiko wa Makabila! Demographic ya Mkoa mzima una watu zaidi ya milioni mbili huku Moshi mjini ina less than 200,000.
 
Usipofanya hivyo jamii itakuhukumu, utashusha hadhi ya elimu unayoitoa kwasababu inaelemea upande fulani, utakuwa predictable na hadhira itakuchoka.
Mix...
Sijapata kuchokwa.
Kitabu changu cha kwanza cha Abdul Sykes (1998) kinakwenda chapa ya tano.

Hapa Jukwaa la Historia sema mwenyewe.
Naisomesha upya historia ya Mwalimu Nyerere na uhuru wa Tanganyika.

Vyombo vya habari electronic na print media vinapishana mlangoni pangu kutafuta mahojiano na mimi.

Hujui nimezumgumza vyuo vingapi Afrika, Ulaya na Marekani baada ya kutoka kitabu kile.
Hujui nimeandika vitabu vingapi na makala ngapi achilia research papers.

Nashukuru sana.
 
Geza...
Sitafuti ushindi ila naieleza mabadiliko yaliyotokea.
 
Hebu tuletee ile historia ya Muslim Welfare Society na jinsi ilivyopigwa vita na kufutiliwa mbali na Papa Pius XIX kabla hajafariki. Pia kwenye hilo usiwasahau wale Nshomile waislamu walivyodanganywa na marehemu Cardinal laurian Rugambwa.
 
Hebu tuletee ile historia ya Muslim Welfare Society na jinsi ilivyopigwa vita na kufutiliwa mbali na Papa Pius XIX kabla hajafariki. Pia kwenye hilo usiwasahau wale Nshomile waislamu walivyodanganywa na marehemu Cardinal laurian Rugambwa.
ksk,
Hii ni mada nzito sana katika historia ya Waislam wa Tanganyika.

Watu wawili tu ndiyo waliofanya utafiti na kuandika kuhusu EAMWS - Dr. Mayanja Kiwanuka ‘'The Politics of Islam in Bukoba District’' (1973) na Mohamed Said '‘Islam and Politics in Tanzania’' (1989).

Bahati mbaya ni lugha ambayo umetumia.
Mathalan, ''kufutiliwa mbali,'' ''Nshomile.''

Hii mijadala ni mijadala inayohitaji utulivu wa akili na lugha zetu ili zivutie wasomaji makini na kupata michango ya maana.

Lete upya hili ombi lako katika lugha ya kistaarabu In Shaa Allah nitakujibu.
 
Mzee Mohamed Said aslmyaleikum nakupongeza kwa makala zako ni nzuri unatupa elimu kubwa tunashukuru Sana kwa Hilo,Lakini nakuomba utupe mchango wa Ukerewe na chifu wa wakerewe nadhani anaitwa Chief Gabriel Lukumbuzya kwenye harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.Nilishawai sikia huyu chifu alikua anatumiwa na Mwalimu Nyerere katika kuongoza Nchi.Tafadhali kama unajua naomba utusaidie na pia nasikia hadi Leo hii Kuna mambo alimwambia Mwalimu Nyerere ayazingatie kwenye kuongoza nchi na inavosemekana ni kwamba alikua kama mtabili kuhusu mambo ya kiutawala
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…