Mambo ambayo Viongozi wanapaswa kujifunza kutoka kwa panya Magawa

Newbies

JF-Expert Member
Jul 13, 2018
1,476
2,148
MAMBO AMBAYO VIONGOZI WANAPASWA KUJIFUNZA KUTOKA KWA MAGAWA.

Kwanza nianze kutoa pole kwa wale wote walioguswa na kifo cha panya shujaa Magawa aliyekuwa mahiri katika kazi yake ya kutegua mabomu yaliyotegwa ardini. Katika makala haya tutaeleza mambo kadhaa ambayo vionozi wanapaswa kujifunza kutoka katika maisha yalitotukuka ya Magawa, kama ifuatavyo,

Mosi; Ujasiri; Maisha ya panya Magawa yalitawaliwa na ujasiri mkubwa , alifanya kazi katika mazingira hatarishi ambayo yangeweza kumhatarishia uhai wake lakini hayo hayakuzuia yeye kutimiza na kukamilisha majukumu yake tena kwa weledi mkubwa. Hapa tunapata funzo la kuwa jasiri wakati wa kufanya, kutenda, kuishi, na kusimamia yale tunayoyaamini bila kuogopa chochote au yeyote tukiweka maslahi ya taifa mbele.

Pili; Kujituma na kufanya kazi kwa bidii; Maisha ya magawa yanatoa funzo kwa viongozi na kwa mtu yeyote kujituma na kufanya kazi kwa bidii. Katika maisha ya Magawa yalitawaliwa na majukumu lukuki ambayo yote aliyatimiza na ikumbukwe mwaka jana alitunukiwa nishani kutokana na ufanyaji kazi wake. Viongozi hapa wapate somo la kujituma kwaajili ya nchi yao na kufanya kazi kwa bidii usiku na mchana kwaajili ya maslahi mapana ya taifa letu.

Tatu; Utii, Magawa alikuwa mtiifu kwa wale waliomsimamia na kuwa majukumu yote aliyotumwa aliyatimiza hata alipofika umri wa uzee ambapo kasi yake ya kuvumbua mabomu ilipungua. Hivyo ni funzo kwa viongozi kuwa watii katika majukumu yale mema wanayotumwa na wakubwa wao wa kazi pamoja na wananchi kwa faida ya taifa letu.

Nne Uzalendo; Magawa alitanguliza maslahi ya watu wengine mbele. Nimesikitika sana niliposikia kuwa Magawa hakuwahi kupata muda wakupata mpendwa wake, hivyo Magawa hakuwahi kabisa kushiriki mapenzi au kuwa na familia. Muda wote wa maisha yake aliojaliwa kuishi aliutumia katika mafunzo na kutimiza majukumu aliyopewa. Hapa ni funzo kwa viongozi kutanguliza uzalendo kwanza kwaajili ya maslahi ya taifa mengine baadaye.

Mwisho; naomba nitoe pole tena kwa wale walioguswa na kifo cha panya magawa, pia nitoe shukrani kwa mwalimu wake na pia kwa wengine maisha ya panya Magawa yawe ni funzo kwetu.
 
Umesahau hiii mkua waache michepuko yule panya hakua na demu,mke wala mchepuko amekula na kichupa chake
 
Namjua Panya buku wa nchi!😁😁😁
 
Back
Top Bottom