Panya Road wamerudi, tuchukue tahadhari, Polisi Dar wafanya msako wawanasa waliowapiga watu mapanga

Kiminyio 01

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
1,352
1,933
Wana Jf Wasalaam,

Tukielekea katika kipindi hiki cha kufunga Mwaka pamoja na kusheherekea Christmas & Mwaka Mpya Tuchukue Tahadhari hasa kuhusiana na kundi la vijana wahalifu wanaotembea kwa Makundi (Panya Road)

Update;
-Jana wamefanya Ukabaji Maeneo ya Karakata Airport ,mmoja Kati ya panya road aliuliwa na Wananchi na kuchomwa moto.

Hata hivyo Askari wetu walijitahidi kufanya Doria maeneo mbalimbali Amani ikarejea na Utulivu

-Leo Hadi hivi Sasa Vijana wapatao 15&26 Wanaendelea na Ukabaji wakiwa Ktk kikundi.Wananchi wanakimbizana Ovyo ,Eneo Ni Karakata Mtaa wa Majukumu..

Ukabaji Bado Unaendelea ..

=====

POLISI WAANZA MSAKO WA WEZI WALIOJERUHI WATU CHANIKA
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeanza kuwasaka wahalifu wanaodaiwa kuvamia nyumba zaidi ya 20 zilizopo Chanika na kuwajeruhi watu kwa mapanga kisha kufanya uporaji wa mali na fedha.


===========================


Operesheni yanasa ‘Panya Road’ waliovunja nyumba 23

Kundi la watoto wenye umri kuanzia miaka minane hadi 12 maarufu ‘panya road’ wamepita nyumba kwa nyumba maeneo ya Zingiziwa kata ya Chanika, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wakiwa na mapanga na kujeruhi kisha kupora mali na fedha.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, aliyasema hayo jana na kueleza kuwa tukio hilo limetokea Jumapili usiku baada ya kundi hilo kuvamia nyumba 23.

“Vitoto vidogo sitaki kuviita ‘panya buku’, ‘panya road’ vinapita kwenye nyumba za watu kuvunja vioo, kuiba kujeruhi nimeagiza Jeshi la Polisi wafanye operesheni wengi wamekamatwa.

“Niwaase wazazi, Mkuu wa wilaya ulitoa tamko mara baada ya tukio, niwaase wazazi muulize mwanao anaporudi jioni, ulikwenda kufanya kazi gani leo au anaporudi asubuhi ulikuwa wapi na nani, asije akarudi nyumbani na TV akakwambia amebeti, asije akarudi na simu akakwambia amepata kwenye promosheni mwongo.”

Makalla alisema katika msako huo wamekamata simu nyingi, runinga karibu 13 na fedha 1,260,000.

“Watoto wenyewe ni wengi, operesheni iliyofanyika jana (juzi) na leo (jana) wazazi mkawatambue watoto wenu kule, wengi wamekamatwa halafu miaka minane mpaka 12 huyu si bado anasoma, wazazi muwe walinzi wa kwanza wa kuwalinda watoto,” aliagiza.

Mkuu huyo wa mkoa aliwataka wawaulize watoto wao shughuli wanazozifanya na wasipokee mali wanazokwenda nazo nyumbani.

Chanzo: Nipashe
 
Mtaa mzima mnakimbizwa na vitoto vya miaka 15 na 16 mnashindwa vipi vidhibiti.
Nawapa mbinu.
Nunue speaker zile za betri
Nunueni mishale yenye sumu
Nunueni asidi
Wakija tena hao mende wapigieni yowe kutumia speaker KILA mmoja aandae mshale wake achague mtu wake hakikisheni wote wamelala chini ni kumkosea Mungu kuwaacha hao mende hai.
Ina maana karakata nzima Hakuna hata mwenye bastola wakija unavaa soksi ya ninja unahakikisha mizoga kama 20 ipo chini,waliopona wakawasimulie wenzao na awatorudi tena mbona huku kitunda ujinga huo haupo acheni uzembe karakata mnafunga maduka mtaa mzima Ina maana hata kuwapiga na chupa zenye bia amuwezi? Nyie ndo mnafanya wanaume wa dar tunadharaulika.
 
Speaker kupigia yowe zinafanya Kazi nzuri Sana usiku nazitumia Sana speaker ni sh elf 20 tu unapata, sauti yake usiku inasambaa mbali na zinawachanganya Sana vibaka na wezi maana awajui wakimbilie upande upi.
Nunueni speakers kupigia yowe hata vijijini huko zinawaamsha wengi usiku kutoa taarifa.
Wezi wanaogopa Sana yowe.
 
Wana Jf Wasalaam,
Tukielekea katika kipindi hiki cha kufunga Mwaka pamoja na kusheherekea Christmas & Mwaka Mpya Tuchukue Tahadhari hasa kuhusiana na kundi la vijana wahalifu wanaotembea kwa Makundi (Panya Road)

Update;
-Jana wamefanya Ukabaji Maeneo ya Karakata Airport ,mmoja Kati ya panya road aliuliwa na Wananchi na kuchomwa moto
Hata hivyo Askari wetu walijitahidi kufanya Doria maeneo mbalimbali Amani ikarejea na Utulivu

-Leo Hadi hivi Sasa Vijana wapatao 15&26 Wanaendelea na Ukabaji wakiwa Ktk kikundi.Wananchi wanakimbizana Ovyo ,Eneo Ni Karakata Mtaa wa Majukumu..

Ukabaji Bado Unaendelea ..
Nyie nao acheni kulia kulia, vijana 15 wanafunga mtaa eti panya Road, nyie si mjikusanye mapanya house wa kutosha mmalizane nao. Maeneo yote ya mjini unakuta nyumba moja ina familia kadhaa, au wapangaji kadhaa mnashindwa kushughulika na hao wahuni.
 
Back
Top Bottom