Panya Road ni "Mpango Maalum"

Panya Road ni "Mpango Maalum"

Nchi hii haiishi vituko, nimepata taarifa kutoka ndani kabisa kuwa wale "panya road" ni mpango maalumu uliosukwa kiustadi zaidi ili kuwaamisha wananchi wasijadili ujio na kuzuiwa kwa vijana kutoka Geita kwa miguu kwa nia ya kuonana na Rais.

Mtoa taarifa anasema vijana wakiwa njiani kuja dar. walishawishiwa sana ili wabadili au waahirishe kuonana na RAIS na hata waliwatumia watu wengine kuwashawishi lakini vijana wale waligoma kabisa, ndiyo maana ikabuniwa hii ya panya road ili kuamisha mjadala wa wananchi kwa vijana hawa.


hakika vituko haviishi Tanzania yetu hii na yasiyowezekana duniani kote basi Tanzania ni mteremko haswaaaaaaaa.

we nimjinga sana unafikili kwa kutumia kinyeo hao wasukuma watatu wa chadema wamekuja jana dar panya road wapo kitambo tu.

wasukuma wamesha kamatwa sasa wapi na wapi
 
Wana JF kwanza kabisa ieleweke wazi kuwa kamwe sitetei wahalifu hata siku moja , ila kwa mtazamo wangu kimfumo, makundi ya panya road, mbwa mwitu , watoto wa mbwa na wamarekani weusi ni matokeo ya ufisadi wa muda mrefu unaofugwa na kuenziwa na genge la magamba , ni hivi , kama Anna Tibaijuka,Werema na Chenge wanachota 1.6 billion za umma kila mmoja na kudeposit kwenye akaunti zao binafsi unategemea wabongo wengine 48 millioni people watapataje mzunguko wa pesa walizochukua , kwa kutumia akili ndogo tu ya kukaa kijiweni kwa kukosa ajira unaweza kujiuliza kama genge lina watu lukuki walio ofisini na walistaafu na wote kwa miaka hamsini ya umaskini bongo wanaula bata Masaki kwa kutumia mabilioni ya pesa za umma sasa unadhani dawa zitatoka wapi hospitalini na unategemea wengine watapata wapi hela ya kula? na unategemea pesa za kuwezesha elimu bure zitatoka wapi? na hawa watoto wa mbwa tuliowanyima elimu bora technically watakosa na ajira na sasa ndo hao wanaturudi mchana kweupe! hawana cha kupoteza manake wana njaa na hawana namna ya kupata chakula kihalali! kwa mawazo yangu sera za magamba zimeshindwa kufanya kazi! nafikiri huu ni wakati watanzania wanatakiwa wasifanye kosa uchaguzi mkuu ujao, tujaribu na wengine hawa wameshindwa kwa miaka hamsini! inatosha! Nyerere alisema nchi ina maadui watatu, ujinga , maradhi na umaskini , na sasa maadui badala ya kupungua wameongezeka, adui wa nne ni ufisadi! watanzania tuamke tuseme imetosha. nitafurahi watanzania wenzangu tukijaribu wengine! amini nawaambia wana JF wenzangu, magamba wameiba sana na walifikiri hakuna kitakachotokea na sasa wanajionea kwa macho matokeo ya wizi wao kwa kuzalisha watoto hawa wa mbwa! haya sasa na tuwapige mabomu na tuwafunge watoto wetu wenyewe tuliowanyima elimu na ajira kwa kuiba mali zao za umma kwa miaka hamsini ya umaskini! ninaamini safari ni ndefu , kwa tathmini zangu ndogo za sosiolojia ya Mlimani bomu ni kubwa sana hapa bongo kuliko tunavyodhani na sio kwamba ninaombea itokee ila kimantiki na tutegemee makubwa zaidi ya sasa ya watoto wa mbwa kama social and economic conditions za bongo hazitachange hasa this unequal distribution of resources iliyokithiri bongo manake gap la walio nacho na masikini ni kubwa sana kwa sasa! hebu angalia mtu ana 1.6b na mwingine hana 200 ya kunywa chai asubuhi! nadhani kama hatutadeal na current situation kwa namna inavyopasa na si kinafiki na kwa jazba basi huko tuendako tutahitaji wanajeshi kabisa kuingia vitani kushughulikia na kudhibiti watoto na vijana wasio na elimu na ajira! ni mtazamo tu!

escrow ya ipo kitambo hao panya road wamekuja lini
 
Nchi hii haiishi vituko, nimepata taarifa kutoka ndani kabisa kuwa wale "panya road" ni mpango maalumu uliosukwa kiustadi zaidi ili kuwaamisha wananchi wasijadili ujio na kuzuiwa kwa vijana kutoka Geita kwa miguu kwa nia ya kuonana na Rais.

Mtoa taarifa anasema vijana wakiwa njiani kuja dar. walishawishiwa sana ili wabadili au waahirishe kuonana na RAIS na hata waliwatumia watu wengine kuwashawishi lakini vijana wale waligoma kabisa, ndiyo maana ikabuniwa hii ya panya road ili kuamisha mjadala wa wananchi kwa vijana hawa.


hakika vituko haviishi Tanzania yetu hii na yasiyowezekana duniani kote basi Tanzania ni mteremko haswaaaaaaaa.

Serekali imechoka
 
Hii inawezekana kabisa, panya road tunaowajua wanavamia mtaa mmoja kama so miwili kwa siku, lakini wajana takribani mitaa kumi tena IPO mbalibali sana
 
Hamna mpango maalumu... bali vijana waliokosa ajiri na wanaoishi kwenye poor government wameamua kutumia fursa ya udhaifu wa serikali yako kufanya maovu kujiingizia kipatokwa njia isiyo ya halali. Kama wao wanaona serikali ina tetea wezi wa mali za umma...kwa nn wasijiingize huko
 
Back
Top Bottom