Grader
JF-Expert Member
- Feb 23, 2009
- 445
- 65
Nilipewa taarifa tangu wiki iliyopita ya kuwa aliyekuwa muasisi wa panya road Mkoa wa Dar es salaam ambaye amekufa kwa kupigwa risasi Afrika Kusini akiwa anaiba kwenye duka huko Johanesburg . Taarifa zaidi zikaletwa huku Dar nami zikanifikia nikaona nifuatilie kwa karibu kwani hawa panya road walishawahi kutingisha jiji letu japo kwa kiasi fulani wamezibitiwa na jeshi letu la kamanda Kova.
Kikundi cha panya road chenye uongozi thabiti kikatoa kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kumsafilisha mwasisi wao aliyefia bondeni, kijana huyo ana umri wa miaka 30 na jina lake anaitwa HAMISI SEIF alikuwa anakaa Telaviv Buguruni kwa wale wanaojua Buguruni wanatambua eneo korofi kwa uharifu kwa magenge ya walevi, watumiaji wa dawa za kulevya,ukahaba,bangi,ukabaji,wizi na mengine mengi.
Taarifa ikatoka ya kuwa mwili wa marehemu ungewasili Dar ijumaa lakini wakashindwa kupata usafiri badala yake ukawasili leo na shirika la ndege la South Africa Airline na baada ya uchunguzi wa kipolisi ili kuhakiki haukubeba madawa ya kulevya then ulikabidhiwa kwa jamaa hawa kwa mazishi.
Mazishi yalifanyika Buguruni Ghana kwenye makabuli karibu na kwa Mzee maarufu sana Mtaa huo anayeitwa Mzee Shauri (Fundi redio), mazishi hayo yalifanyika kwa mkusanyiko wa vijana wengi sana wa Buguruni na sehemu nyingine za Dar kwa kuletwa na mabasi ya kukodi na bodaboda. Mazishi yalianza saa 2 usiku mpaka 3 usiku.
Kwenye mazishi hayo nimeshuhudia watu wakipora sana watu wanaopita mbele yao na kuzua tahatuki ndani ya muda huo mpaka muda wa mazishi kwisha na hali kurejea kawaida.
Maswali mazito yafuatayo nilitafakari sijayapatia majibu ni mtandao huu bado upo hivi jeshi letu la polisi na usalama wa taifa wapo wapi?, je kikundi hiki kinapata wapi ufadhili?,je sheria iko wapi na taratibu za kuzika muda wa usiku,mbona polisi hawaonyeshi ushirikiano kwenye vitendo vya kudhibiti uharifu pindi wanapotoa taarifa za kiharifu,kwa nini matukio haya yapo sana uswahilini, hivi hawa viongozi wa mitaa wana kazi gani kuhusu kuzuia uharifu kwenye maeneo hayo. Tujadiliane ili tupate suluhisho.
Najua wengi wangependa kuona picha za eneo la tukio lakini nilishindwa kufanya hivyo kwani simu yangu pamoja na kamera yangu nilifungia ndani ya gari na kupaki Buguruni sheli na nikaenda kuzika kwa ajili ya kuogopa kuporwa.