Pancakes

farkhina

Platinum Member
Mar 14, 2012
14,568
16,906
Mahitaji....

1) Unga wa ngano kikombe 1
2) Baking powder 1teaspoon
3) Sukari 2 tablespoon..
4) Maziwa kikombe 1
5) Yai 2
6) Chumvi 1/4 teaspoon
7) Siagi iliyoyayushwa 2 tablespoon au vegetable oil...

Namna ya kutaarisha.

1) Changanya unga, sukari, chumvi, baking powder na weka pembeni

2) Kwenye bakuli jengine weka mayai, maziwa, siagi au vegetable oil.... changanya vizuri

3) Mimina mchanganyiko wa maziwa katika unga... changanya vizuri hadi kupata uji mzito

4) Weka pan yako jikoni moto kiasi.... then weka mafuta kidogo sana ili pancakes sizigande..

5) Chukua upawa chota mchanganyiko na mimina taratibu kwenye pan acha yenyewe itawanyike...

6) Subiria hadi ukiona pancake inatoa mapovu juu then geuza...fanya hivo hadi kumaliza

7) Pancake tayari kwa kuliwa....waweza mimina asali juu yake kwa ladha nzuri zaidi...
1387376554728.jpg
1387376568993.jpg
1387376587837.jpg
 
farkhina asante kwa tutorial ya pishi hili,nina swali kuna tofauti gani ya pancakes na crepes??
Maana siye husema chapati za maji lakin menu za mahotel makubwa huandika crepes wakati nilijua ni pancakes!!!:confused:
 
Last edited by a moderator:
asante sana huwa natengeneza hizo ila siweki bakin powder just mayai tu na chumvi sukari kidogo na zinatoka vizuri am the best kwenye pancake ila nitajaribu kuweka bakin powder siku moja
 
Pancake ni nene kuliko crepes kutokana kuumuka kwake kutokana na kuwekwa baking powder....
Crepes ndio sawa na chapati za maji.....
 
Last edited by a moderator:
asante sana huwa natengeneza hizo ila siweki bakin powder just mayai tu na chumvi sukari kidogo na zinatoka vizuri am the best kwenye pancake ila nitajaribu kuweka bakin powder siku moja

Ukiweka baking powder yaumuka na kuwa laini....
Je unaweka flavor yeyote mfano vanilla essence?
 
Thanx mamito, napenda pancakes. Mimi huwa nafanya simple yani unga wa ngano, maziwa na mayai vilevile sukari kwa mbali sana au bila sukari. Halafu nina-top up na pancake syrup au nikaweka strawberries. Tamuuu!!
 
Yeah tamu sana...
 
Nimeshangaa unaweka na siagi na maziwa. Mie huweka chumvi na sukari kidogo afu naongeza hoho, vitunguu, na carrots kwenye mchanganyiko. Situmii baking powder, maziwa wala siagi.

Kuna aina moja inaitwa veffel, ni asili ya norway. Naipenda kweli manake same mix naweka kwenye jiko lake maalum na sikaangi na mafuta.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom