Panama papers na jinsi Mungu anavyomuumbua mnafiki

Panama papers na jinsi Mungu anavyomuumbua mnafiki

Hizo rasilimali za Tanzania zimeanzishiwa thread nyingi sana humu jamii forum ndio maana TAKUKURU imepata bosi mpya na imekuwa ikijipanga upya. Majambazi hata kwenye upinzani yapo mengi tu, fedha inayotolewa hao hao kina Cameron imekuwa ikiliwa na viongozi wa CDM, nadhani ukweli huo unaufahamu. Ukiyatazama mambo kitaifa basi uwe tayari kuyatazama kimataifa.

Kama huna akili, tafuta hata za kuazima kisha uje ujibu vizuri
 
Kashfa ya jinsi ambavyo mabeberu wanavyoficha fedha zao kwenye taasisi za fedha za Panama, ndio habari ya dunia kwa sasa. Wanaoumbuliwa ni watu wenye heshima zao duniani, ni mafisadi wa kiwango cha kimataifa.

Mmojawao ni Marehemu Baba mzazi wa David Cameron, waingereza wanakomaa na Cameron kwa sasa. Wanahoji utajiri wake wa sasa kama hauna uhusiano na fedha zinazowekwa kwenye mabenki ya Panama kwa ajili ya kukwepa kodi.

Huyu David Cameron ndio ambaye kwenye mikutano mikubwa ya kimataifa anawananga kina Robert Mugabe na marais wetu wengine wa Afrika. Anachokifanya Cameron kwa sasa ni sawa sawa na miaka ile ya 90 wakati George Bush alipomnyanyasa kisaikolojia aliyekuwa rais wa Ukraine Leonid Kuchma kwenye mkutano mmoja wa kimataifa, akawaambia waandaaji kwamba anataka amuone Kuchma amekaa kwenye kiti kinachotazamana na cha kwake kwa sababu tu Kuchma alienda kinyume na maslahi dhalimu ya Marekani.

Mungu hamfichi mnafiki, siku zote huhakikisha anamuanika hadharani ili watu wajifunze kutokana na unafiki wake. Leo hii David Cameron anapohutubia hainui tena shingo yake kwa mbwembwe huku akiwatazama wale anaowahutubia, leo anainama chini katika muda mwingi wa hotuba zake.

Mabeberu hawana haki ya kimaadili ya kutupangia masharti mengi ya kutupatia misaada. Kama vigezo vya kutunyima misaada ni unyama wetu, basi wanapaswa kutambua kwamba huo unyama tumejifunza kwao, huo ufisadi wa mitandaoni tumejifunza kwao. Wizi wa ten percent waalimu wetu ni wao.

Na wao kama waanzilishi wa yale yanayoonekana kuwa sababu ya sisi kunyimwa misaada, wanao wajibu wa kukumbuka kuwa dunia ni duara, lazima ipo siku ambayo uchafu wao utajionyesha dhahiri kwa kila mwenye akili timamu.

Pole sana David Cameron, na kama sio kiburi cha ule u-uingereza wako, ingefaa sana kama ungewaandikia barua binafsi marais wote uliowakwaza, huku ukiomba msamaha, na sababu ya kufanya hivyo ni ukweli kwamba utajiri wako wa leo unao uhusiano wa moja kwa moja na ufisadi, tabia ambayo waafrika tumeirithi kwenu nyinyi watawala, mfano hai ni Baba yako mzazi.
Wanamuonea mmiliki wa wikiLeak Julian Assange sababu wanajua wikiLeak itaendelea kufichua maovu yao
 
Kama huna akili, tafuta hata za kuazima kisha uje ujibu vizuri
Kwa nini wewe usitafute akili za kuazima?. Unajiona kama vile upo sawa kumbe ni punguani namba moja!!. Unachokiongea kimezoeleka kusikika miongoni mwa wajinga wengi wa aina yako, watu ambao wanashindwa kuelewa maana ya forum. Wapuuzi wanaoshinwa kuelewa kuwa kwenye mitandao ya kijamii lazima mtu ajifanye mjinga ili aweze kufaidika kupitia maarifa ya wengi.
 
Umemshamshauri Jecha na Shein kuandika barua kama hiyo kwa Wazanzibar na Watanzania wote kwa ujuma?

Charity begins at home.
Uvyama ni moja kati ya majanga yatakayoliangamiza Taifa letu mungu tuepushie mbali,kila tukio watu wanalihusisha na siasa za vyama kama kwamba mtu akifa ataulizwa chama chake ni gani?
 
Umeanza vema lakini kuanzia katikati nikagundua nia yako ni kutetea uovu wa ccm na viongozi mavi wa afrika. Basi, your whole post is nothing but a zero contribution to our beloved african family. Wenzetu wazungu hata wakiiba hela za mradi wa daraja wanahakikisha daraja linajengwa, lakini mccm and the likes inaiba chooote hata nondo hukuti. Bora wizi mdogo kuliko wizi mkubwa wa kuangamiza jamii. Huku ccm aliyeiba mabilioni anaishia kutozwa faini au kufagia zananati, lakini mwizi wa bata la elfu kumi na tano anafungwa miaka saba mpaka 15. To hell ccm and the likes.

Sasa wewe si ndio ungetililika bila kuonyesha kuwa uko UKAWA? unamlaumu mwenzio kuegemea katika chama flani lakini wewe mwenyewe haionyeshi kama uko nyutro.
 
Back
Top Bottom