Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Kashfa ya jinsi ambavyo mabeberu wanavyoficha fedha zao kwenye taasisi za fedha za Panama, ndio habari ya dunia kwa sasa. Wanaoumbuliwa ni watu wenye heshima zao duniani, ni mafisadi wa kiwango cha kimataifa.
Mmojawao ni Marehemu Baba mzazi wa David Cameron, waingereza wanakomaa na Cameron kwa sasa. Wanahoji utajiri wake wa sasa kama hauna uhusiano na fedha zinazowekwa kwenye mabenki ya Panama kwa ajili ya kukwepa kodi.
Huyu David Cameron ndio ambaye kwenye mikutano mikubwa ya kimataifa anawananga kina Robert Mugabe na marais wetu wengine wa Afrika. Anachokifanya Cameron kwa sasa ni sawa sawa na miaka ile ya 90 wakati George Bush alipomnyanyasa kisaikolojia aliyekuwa rais wa Ukraine Leonid Kuchma kwenye mkutano mmoja wa kimataifa, akawaambia waandaaji kwamba anataka amuone Kuchma amekaa kwenye kiti kinachotazamana na cha kwake kwa sababu tu Kuchma alienda kinyume na maslahi dhalimu ya Marekani.
Mungu hamfichi mnafiki, siku zote huhakikisha anamuanika hadharani ili watu wajifunze kutokana na unafiki wake. Leo hii David Cameron anapohutubia hainui tena shingo yake kwa mbwembwe huku akiwatazama wale anaowahutubia, leo anainama chini katika muda mwingi wa hotuba zake.
Mabeberu hawana haki ya kimaadili ya kutupangia masharti mengi ya kutupatia misaada. Kama vigezo vya kutunyima misaada ni unyama wetu, basi wanapaswa kutambua kwamba huo unyama tumejifunza kwao, huo ufisadi wa mitandaoni tumejifunza kwao. Wizi wa ten percent waalimu wetu ni wao.
Na wao kama waanzilishi wa yale yanayoonekana kuwa sababu ya sisi kunyimwa misaada, wanao wajibu wa kukumbuka kuwa dunia ni duara, lazima ipo siku ambayo uchafu wao utajionyesha dhahiri kwa kila mwenye akili timamu.
Pole sana David Cameron, na kama sio kiburi cha ule u-uingereza wako, ingefaa sana kama ungewaandikia barua binafsi marais wote uliowakwaza, huku ukiomba msamaha, na sababu ya kufanya hivyo ni ukweli kwamba utajiri wako wa leo unao uhusiano wa moja kwa moja na ufisadi, tabia ambayo waafrika tumeirithi kwenu nyinyi watawala, mfano hai ni Baba yako mzazi.