Ukisikia kauwawa muisrael mmoja ujue kesho kifo kinawasubiri wapalestina wanne au zaidi. Lakini kwa sababu ndani ya bunge la Marekani, pentagon, hollywood na kwenye sekta nyingine nyeti za USA wamejaa wayahudi, wala huwezi kusikia wanawekewa masharti ya manyanyaso, wala kusimangwa na kina Cameron na mabeberu wengine.
..kwa hapa Tz nawafananisha wapinzani na wapalestina kwa jinsi wanavyoonewa na ccm.
..hebu chukulia mfano wa Daudi Mwangosi alivyouawa wakati aki-cover mkutano wa wapinzani. Raisi alimpandisha cheo kamanda aliyekuwepo eneo la tukio, na ukiangalia video za eneo la tukio kamanda yule alionekana kabisa kuwa alikuwa mshari-shari.
..pia fuatilia tukio la mabomu ktk mkutano wa chadema arusha. polisi waliua mpaka watoto wa umri wa chekechea na mpaka leo hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya polisi waliofanya vurugu zile, na wananchi waliodhurika hawajalipwa fidia yoyote.
..hivi karibuni, baada ya Raisi Magufuli kuingia madarakani, ameuawa Alphone Mawazo ambaye alikuwa Mwenyekiti wa cdm mkoa wa Geita. Serikali haijatoa tamko lolote lile la kukemea unyama huo. sana sana serikali ilionekana kuwakandamiza hata familia ya wafiwa kwa kuzuia mwili wa marehemu usiagwe kwa kuzingatia matakwa ya familia yake.
..kuna wakati Raisi anasema ataongoza wa-Tz wote bila kubagua. Halafu anatokezea kwenye mkutano wa ccm kule Singida na kuvinanga vyama vya upinzani akiviita vyama vya hovyo-hovyo.
..kwa kweli we have a very long way to go, kuelekea kwenye jamii inayozingatia HAKI SAWA KWA WOTE.