Panama papers na jinsi Mungu anavyomuumbua mnafiki

Panama papers na jinsi Mungu anavyomuumbua mnafiki

Mada inamhusu Cameron na unafiki wake, muingereza huyo alikuwa akipiga kelele sana huku akijifanya yeye ni kioo cha maadli kwa viongozi wote wa Afrika. Sio suala la baba na mtoto kama unavyoongea wewe. Kwa waingereza kitendo cha Cameron ni kashfa kubwa sana, baba yake ni mkwepa kodi, ni fisadi, wazungu siku zote wamelelewa katika misingi ya kuheshimu ulipaji kodi. Baba yake cameron kaenda kuficha fedha panama ili akwepe kodi, kimaadili ni kosa kubwa hata kwa mtoto wa marehemu baba yake Cameron kutumia au kufaidika na fedha ambayo imetokana na kutolipwa kwa kodi.
Hayo China na siasa ulizoziongelea sio sehemu ya mada. Mada inamhusu Cameron ambaye anapokuwa kwenye mikutano anajifanya yeye ndio bingwa wa maadili lakini kumbe baba yake mzazi ni fisadi kama wale waliopo kwenye zile nchi ambazo huwa anawasimanga viongozi wake kila anapopata nafasi ya kuongea hadharani.

Unayako tu na cameroon kamwe sikio halizid kichwa utegemez mbaya ndo mana unalilia hata pasipotakiwa kuliliwa kama ni historia na mabaya bas hatufai kuwaunga mkono mataifa ya ulaya
Kwa jinsi walivyowafanya mababu zetu na rasilimali zetu wasingeweza kutukosoa kwa matendo ya babu zao na baba zao had wakina mkwawa walijiua.
 
Sina sababu ya kujipoza machungu, misaada imekuwepo kabla mimi na wewe hatujazaliwa. Ninaikumbusha dunia kwamba mnafiki huumbuliwa na Mungu. Wapo viongozi wa mataifa yanayotupatia misaada lakini huwa hawajifanyi kuwa waalimu wetu wa maisha. Cameron huwa hachoki kujifanya mtakatifu kumbe ni mtoto wa fisadi. Kama wale mafisadi wanaochangia kuifanya Afrika ikawa masikini ilhali wengine wanaendelea.

Hata china ni mnafiki ananyonga wa hujumu uchumi kwake huku anajidai mwema hamna kitu hapo.
 
Hata china ni mnafiki ananyonga wa hujumu uchumi kwake huku anajidai mwema hamna kitu hapo.
Waingereza walikataa wakimbizi kutoka nchi za kiarabu wasiingie nchini mwao wakati sababu ya ukimbizi wao ni vita ambayo wao waingereza wamechangia katika silaha kwa kiasi kikubwa sana. Ni baada ya presha za nchi nyingine za Ulaya kuwa kubwa ndipo waingereza wakaruhusu wakimbizi kutoka middle east waingie nchini mwao. Nadhani umegundua kuwa chini ya jua hakuna aliyekamilika. China wananyonga watu, muingereza mbaguzi na mnafiki wa kiwango cha juu.
 
Putin ni mnyama, na habari zote zinazohusu hii kashfa wala hazitasikika kwenye vyombo vya habari vya Russia. Jamaa ni mafia kupita maelezo, anajua sana kumminya mtu, na ukijifanya kiburi basi lazima ufe.
NIMEONA NDUGU WA KARIBU WA VIONGOZI WA JUU CHINA KWENYE ''POLITBRO'' WAMO PIA, KATI YA MEMBER 7, NDUGU WA VIONGOZI 3 WAMO, AKIWEMO NDUGU WA RAIS XI JINPING.
 
Waingereza walikataa wakimbizi kutoka nchi za kiarabu wasiingie nchini mwao wakati sababu ya ukimbizi wao ni vita ambayo wao waingereza wamechangia katika silaha kwa kiasi kikubwa sana. Ni baada ya presha za nchi nyingine za Ulaya kuwa kubwa ndipo waingereza wakaruhusu wakimbizi kutoka middle east waingie nchini mwao. Nadhani umegundua kuwa chini ya jua hakuna aliyekamilika. China wananyonga watu, muingereza mbaguzi na mnafiki wa kiwango cha juu.

Acha hizo china mwenyewe ni mnafiki sna watu weusi wanateseka kule kwa ngoz zao had wametengewa maeneo yao duniani ubaguzi upo tena mkubwa kila taifa linajiona bora sio uk tu tafuta nyuz humu unazungumzia hayo mambo narudia tena unajipoza machungu tu kupitia cameroon na ndo lengo lako ukrein mwenyewe anafunga mipaka yake ugirik hivo hivo kuhusu wakimbiz we jamaa ni noma sna tena mpotoshaji ishaur serikali ijitegemee ili hao unaowaita wanafik waone aibu sio kutuaminisha uongo hapa.
 
..kwa nini pm Cameron aandamwe kwa makosa ya baba yake?

..ukatili wa Mugabe na serikali yake ufumbiwe macho kwasababu baba yake Waziri mkuu wa uingereza amekwepa kodi?

Kuna watu inaelekea hawaelewi hii kitu Na wanataka kuitumia hiyo nafasi kuwatakasa watawala wetu. Kosa ni kosa bila kujali limefanywa Na nani. David Cameroon zile pesa ziliwekwa Na baba Yake sio yeye Na interest Yake Na hiyo pesa ilikoma 2010. Sasa tumhukumu David kwa makosa ya baba Yake?

Tuache propaganda zisizo tusaidia chochote.

Tiba
 
babake alimwacha na urithi wa dola laki 5,sasa amekutwa na dola milion 5 zimejiongeza kwa njia ipi ndio swali
Huyu bwana ni mtuhumiwa wa wizi wa raslimali za wananchi wake na ni kweli mungu hamfichi mnafiki wale SFO wanatakiwa wamshughulikie ili kubaini siri ya mchezo.
 
Acha hizo china mwenyewe ni mnafiki sna watu weusi wanateseka kule kwa ngoz zao had wametengewa maeneo yao duniani ubaguzi upo tena mkubwa kila taifa linajiona bora sio uk tu tafuta nyuz humu unazungumzia hayo mambo narudia tena unajipoza machungu tu kupitia cameroon na ndo lengo lako ukrein mwenyewe anafunga mipaka yake ugirik hivo hivo kuhusu wakimbiz we jamaa ni noma sna tena mpotoshaji ishaur serikali ijitegemee ili hao unaowaita wanafik waone aibu sio kutuaminisha uongo hapa.
Hilo la kujitegemea ndio la maana zaidi, ila pointi yangu inabakia pale pale, kabla hujafa haujaumbika. Marehemu Baba yake Cameron amemuumbua mwanae.
 
Hilo la kujitegemea ndio la maana zaidi, ila pointi yangu inabakia pale pale, kabla hujafa haujaumbika. Marehemu Baba yake Cameron amemuumbua mwanae.

JIPOZE MACHUNGU KUPITIA CAMEROON PESA INA NGUVU SANA ZINGETOKA USINGESEMA WANAKASHFA,,,,,,,,, CHINA ASINGEUNGANA NA TZ NN KINGEFUATA ? JIBU NI UADUI. KUMBUKA BADO ANAENDELEA KUISAIDIA TZ HUYO CAMEROON KTK BAADHI YA MIRADI ISHAURI SERIKALI IKATAE KWA KUWA BABA YAKE ANA KASHFA.
 
Acheni kubwabwaja! Hata kama wzungu ni wezi lkn Kwako watoto. Hawakai chini darasani, kuna umeme, kuna maji na kuna bima za matibabu , kuna barabara , kuna haki za binadamu kwa kila raia.
 
Hawa lengolao kutukandamiza sie
Ila mengi mabaya wanayafanya
 
Atawananga vp wakat mhujumu uchumi? tena kafanaya yy kwani baba yake cameroon yupo madarakani? Baba yake cameroon kawah kuwaponda viongoz wa tz? Mada yako ingekuwa na nguvu endapo baba yake cameroon angenyima hizo pesa kwa tz sasa mtu mwenyewe hayupo unajipoza machungu tu ndo mana hata inshu yenyewe uk haina mashiko.
Kuna kitu kinaitwa moral authority.hata mahakamani ushaidi wa convict hauna nguvu sana.
 
angalau wazungu wanastaha ya kuwajali wananchi wao sio huku kwetu tumekosa ubinadamu ,,ubinafsi na madharau kati yetu vimetawala,,hasa ukute kapata viela vya dili
 
Mzee naona taratiiiiibu unaanza kuhama kwenye mada husika, umeanzia na Israel halafu unakwenda kwenye CCM. Nazungumzia jinsi viongozi wa kibeberu wanavyokosa hoja za kuwageuza viongozi wetu kuwa watumwa wa fikra zao. Naongelea ukosefu wa usafi wa kimaadili wa viongozi katika dunia ya kibepari, dunia ambayo kampuni au taasisi moja inatoka nje ya mipaka ya nchi na kwenda kutafuta sehemu ya kuweka fedha kwa nia ya kukwepa kodi.
Hii mada ina muelekeo wa nje ya nchi moja, kina David Cameron wamejaa dunia nzima lakini hao hao viongozi wanafiki ndio huwa wanajifanya kana kwamba wao ndio wenye viwango vya ustaarabu ambao viongozi wetu eti wanawajibika kuviheshimu. Tafadhali tusihame kwenye mada husika na kuanza kujadili mambo ya siasa za ndani za CCM na mahusiano yake na vyombo mbalimbali vya kijamii.

..samahani nilikuwa " nachomekea" tu.

..lakini viongozi wetu nao ni wanafiki na wakosefu wa maadili kuliko viongozi wa nje unaowalaumu.
 
..samahani nilikuwa " nachomekea" tu.

..lakini viongozi wetu nao ni wanafiki na wakosefu wa maadili kuliko viongozi wa nje unaowalaumu.
Haha ha nimeipenda sana hiyo "nachomekea tu". Ni kweli kabisa mkuu, katika maisha haya ukikitazama kitu kwa nje mara nyingi sivyo kilivyo kwa ndani. Wabunge wanaongea kwa mikwara mingi bungeni mpaka wanataka kuvaa mask usoni eti wasiwaonee aibu wala rushwa, halafu wanakuja kuingia kwenye mtego huo huo wa rushwa!!
 
babake alimwacha na urithi wa dola laki 5,sasa amekutwa na dola milion 5 zimejiongeza kwa njia ipi ndio swali

Waafrica ni shwaini kabisa sisi, unahoji ongezeko la pesa za Cameron unashindwa kuhoji raslimali za Tanzania zinakopelekwa na majambazi ya ccm, all in all, bado UK hao hao mnaowazodoa sasa hivi ndo mnawategemea wawasaidie tena, ujinga uliokithiri
 
Hizo rasilimali za Tanzania zimeanzishiwa thread nyingi sana humu jamii forum ndio maana TAKUKURU imepata bosi mpya na imekuwa ikijipanga upya. Majambazi hata kwenye upinzani yapo mengi tu, fedha inayotolewa hao hao kina Cameron imekuwa ikiliwa na viongozi wa CDM, nadhani ukweli huo unaufahamu. Ukiyatazama mambo kitaifa basi uwe tayari kuyatazama kimataifa.
 
Huwajuia waingereza na majivuno yao ndio maana una maoni ya aina hii. Waingereza ni watu ambao kwa fikra zao binadamu wa kwanza ni muingereza halafu wanafuata watu wa mataifa mengine. Kashfa ya baba yake Cameron inatosha kabisa kumnyima usingizi yeye kama kioo cha jamii ya kiingereza, inatosha kabisa kuwapa uhalali waingereza kumuuliza maswali Cameron kila atakapokwenda kufanya shughuli za kijamii na kisiasa.
Ndo maana nawapenda waarabu
 
Back
Top Bottom