bless on
JF-Expert Member
- May 22, 2026
- 797
- 1,861
Leo pambano ni kati ya Habiba, mshambuliaji hatari mwenye chenga za maudhi, dhidi ya Sele, ambaye leo anaonekana kulegeza ulinzi makusudi!
Dakika ya kwanza, Sele anaanza kwa pasi fupi fupi za Salamu Habiba anaipokea, anaituliza kifuani kwa tabasamu pana.
Anampiga chenga ya jicho moja, Sele anayumba! Sele anarudi tena, anafanya 'pressing' ya karibu, ananong'ona neno moja sikioni mwa Habiba... Hatari hapa! Habiba anacheka kwa sauti ya chini, anautoa mpira nje, ni kurusha kwa mahaba!
Habiba anaingia ndani ya boksi la hisia. Anaachia shuti la manukato makali, Sele anadaka! Sele anaikumbatia ile hali, anagoma kuachia.
Hapa hakuna refarii, hapa hakuna kadi nyekundu! Sele anapiga pasi ndefu ya Sifa, anamsifu Habiba jinsi alivyopendeza usiku wa leo. Habiba anainama kwa aibu, anacheza 'tiki-taka' ya vidole mkononi mwa Sele.
Sele sasa anamiliki dimba la mazungumzo.
Anapiga krosi ya Ahadi za Baadaye', Habiba anaruka juu, anaipiga kichwa kwa upole, anamtazama Sele machoni... Ni goli? Hapana! Ni 'save' ya hatari kutoka kwa Sele, anashika mikono ya Habiba na kuibusu kwa ufundi mkubwa.
Sele anasonga mbele, anapiga shuti la nguvu la 'Nakupenda', Habiba anashindwa kuzuia, mpira unazama wavuni! Ni goli la ushindi! Habiba anamkumbatia Sele, Sele anamnyanyua juu, pambano linaisha kwa sare ya furaha na upendo.