Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,476
- 4,755
Halafu hii picha chanzo chake ndo mimi, nina hardcopy yake, kuna mshikaji aliiomba mwaka jana mara ghafla bin vuu ikatapakaa kila mahali kwenye internet. Dang, shoulda copywritten it!!
Tunaweza kuirudisha Pamba. Tunaweza kuanzaia humu humu kwa sababu kukutana wote itakuwa ngumu. Harakati zinaweza kuanzia hapa kisha tukapata mwakilishi akajaribu kuongea na wahusika. Kwa mkoa wa Mwanza na 'diaspora' yake tunaweza kabisa kufanikisha kuifufua timu. Nashauri tuchague siku na muda mwafaka tukutane humu JF, tujaribu kujadiliana jinsi ya kuweza kuifufua Pamba. Najua hatuwezi kubeba mzigo wote wa kuendesha timu lakini tunaweza kuwa chanzo/catalyst ya kuhamasisha wana Mwanza kuifufua hii timu.Wana Mwanza wote. Turudisheni timu yetu ya Pamba kwenye Super League. Je, tuanzie wapi?
Wanakishamapanda ni Toto Africans mkuu...TP LINDANDA WANAKAWEKAMO, WANA KISHAMASHAMAPANDA. napendekeza J.mosi tukutane humu. inaniuma sana kuona timu ambayo mwaka 1990 nilikimbia kwa miguu kutoka Pasiansi hadi CCM Kirumba tukisindikiza timu yetu ikitoka Uganda.
Wanakishamapanda ni Toto Africans mkuu...
Pamba ndio walikuwa Tout Puisant Kawekamo......R.I.P Domonick Chilambo
Mkuu wa mkoa ni mtu wa kupita, unaweza kuzungumza naye leo kesho akahamishwa.Inatakiwa jitihada za wananchi wa kawaida tu, naamini tupo wengi wenye kupenda kuona hadhi ya Pamba ikirudi.Zungumzeni na mkuu wa mkoa muanzishe account maalum halafu mnaandaa mpango wa kuchangia tigo pesa, mpesa etc tutawachangia
Mkuu wa mkoa ni mtu wa kupita, unaweza kuzungumza naye leo kesho akahamishwa.Inatakiwa jitihada za wananchi wa kawaida tu, naamini tupo wengi wenye kupenda kuona hadhi ya Pamba ikirudi.
Zungumzeni na mkuu wa mkoa muanzishe account maalum halafu mnaandaa mpango wa kuchangia tigo pesa, mpesa etc tutawachangia
Sijui iko chini ya nani. Tuchagueni siku na muda tukae humu tujadili kisha tunaweza kupata wawakilishi wa kwenda kuwasaka wahusika na kuongea nao. Kampeni inaweza kuanzia humu, tusiishie tu kutaja majina ya wachezaji wa zamani. Njia bora ya kuwaenzi hao nyota wa zamani ni kuifufua timu na kuhakikisha inarudisha hadhi yake na hadhi ya mkoa.Hiyo timu iko chini ya akina nani siku hizi? Niko tayari kushiriki kwenye kuifufua.
Msimsahau na yule Bubu mtunza kiwanja-CCM KIRUMBA....!
Sijui iko chini ya nani. Tuchagueni siku na muda tukae humu tujadili kisha tunaweza kupata wawakilishi wa kwenda kuwasaka wahusika na kuongea nao. Kampeni inaweza kuanzia humu, tusiishie tu kutaja majina ya wachezaji wa zamani. Njia bora ya kuwaenzi hao nyota wa zamani ni kuifufua timu na kuhakikisha inarudisha hadhi yake na hadhi ya mkoa.
OK. Mimi ndio Mleta Mada hii. Kwanza kabisa niwashukuru wote mliochangia kwa kutoa maoni na kuonyesha upendo na hamu kubwa ya kuirejesha timu yetu ya Pamba. Nafikiri JUMAMOSI HII, KUANZIA SAA NNE ASUBUHI TUKUTANE WOTE HAPA JF ILI TUJADILI HILI SUALA. Pia wataarifu Wananzengo wote na wale wote wanaopenda soka lenye kiwango cha kimataifa wawasiri kikaoni bila kukosa. Kama unamawasiliano na wachezaji wa Pamba Soccer Team wa zamani (walio Hai), basi wape taarifa. Mimi binafsi naanza na rafiki wangu Nteze John Lyungu ambae anaishu USA kwa sasa hivi. Nia tunayo, Uwezo tunao, na sababu tunayo ya Kuirudisha Timu yetu na heshima ya mkoa wetu. TAHADHARI... HAKUNA ULAJI HAPA. NGUVU YA WANANZENGO IPO IMARA KUHAKIKISHA TUNAJITOLEA KIMAWAZO, KIFIKIRA, NA HATA KIFEDHA IKIBIDI. Lakini sharia mkononi...PERIOD
Naziumbuka jezi zao nyeupeeeeee, halafu zimeandikwa kifuani Pamba kwa Thiodan. Kuna mchezaji wa pamba alikuwa mwembamba sana wakimuita mbu ila akiweka stendi baba huchukui mpira, jina limenitoka