Pamba FC mkombozi wa soka la Mwanza

Torra Siabba

Senior Member
Jul 24, 2016
105
102
Jana kulikua na mechi ya Kuwania kupanda daraja Mwanza, ambapo Pamba fc walikua wakicheza na Kitayose fc, huo mchezo ulimalizika kwa Pamba kutoka sare ya bila kufungana na Kitayose ya Tabora, Mwamuzi kwenye mchezo huo Emmanuel Safari alishindwa kuumudu mchezo huo baada ya kushindwa kutoa penati tatu kwa Pamba fc na moja kwa Kitayosa.

Mbali na hilo kilichonivutia zaidi ni watu zaidi ya 2000 waliojitokeza kuutazama mchezo huo jambo ambalo linaonyesha kwamba ipo haja kwa Mkoa wa Mwanza kuisaidia Pamba ili ipande daraja maana Watu wale wanaonyesha kwamba imewachosha kukaa bila timu ya ligi kuu.

Hivyo Serikali ya mkoa na Chama cha SOKA MKOA, Bila kusahau wadau muiangalie Pamba Tp lindanda wana kawekamo iweze kupanda daraja msimu huu.


 
Kama Pamba wangeshinda jana Walikua wanamshusha Kitayosa nafasi ya pili lakini kwakua walitoka sare Kutayosa anabaki nafasi ya pili kwa pointi 50 pamba nafasi ya tatu pointi 48 huku Jkt Tanzania wakiongoza ligi kwa pointi 59
 
Team ya Mwanza hata ikipanda inakaa msimu mmoja inashuka nadhani Mwanza mtafute mchezo mwingine muukuze mf kuendesha baiskeli basi
 
Back
Top Bottom