Pale sayansi inapokutana na upendo wa kindoa…….!

Paspii0

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2020
Posts
638
Reaction score
1,043
Katika maisha ya sasa, ambapo kila mtu anatafuta afya, amani, na kizazi chenye matumaini kuna jambo moja la msingi tunalopaswa kulizingatia kwa umakini mkubwa, uchaguzi wa mwenzi wa maisha.

Kwa muda mrefu, tumekuwa tukioana ndani ya koo na jamii zilezile. Ingawa ni kawaida, sayansi ya kisasa ya vinasaba (genetics) inatufundisha kuwa njia hii imechangia kwa kiasi kikubwa kurithisha maradhi ya kurithi kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Maradhi haya ni kama….

  • Sickle Cell (chembechembe za upungufu wa damu)
  • Shinikizo la damu
  • Kansa ya kurithi
  • Makundi ya damu yasiyooana
  • Urefu au ufupi uliopitiliza
  • Albinism, na mengine mengi
Lakini kuna suluhisho rahisi ambalo lipo ndani ya uwezo wetu. Kuoana kati ya jamii na kanda mbalimbali nchini.Kwa mfano…..

  • Mwana wa Mtwara aoe Mwanza
  • Binti wa Tanga aolewe Kigoma
  • Mwana wa Kigoma aoe Mbeya
  • Msichana wa Songea aolewe Moshi
Kwa kufanya hivi, tunakuwa tunachanganya vinasaba vya makabila na maeneo tofauti, jambo ambalo huongeza kinga ya mwili na kupunguza uwezekano wa matatizo ya kigenetic kuonekana. Sayansi inaonesha kuwa vinasaba visivyoonekana (unexpressed genes) vinaweza kutulia kabisa visipopewa nafasi ya kujitokeza kwa kukutana na vinasaba vya aina nyingine kutoka eneo tofauti.

Kwa maneno mengine,
Kuoana na mtu kutoka mbali kunaongeza nafasi ya kupata watoto wenye afya bora, akili nzuri, mwili wenye nguvu, na maisha marefu.

Fikiria hili,
Unapooa au kuolewa na mtu kutoka kabila au kanda nyingine, haujengi tu familia, bali unachangia kujenga kizazi kipya chenye mchanganyiko mzuri wa damu, akili, na nguvu mpya. Hii ni silaha ya kuondoa magonjwa ya kurithi taratibu kwenye jamii.

Hebu tujiulize, Je, tunataka kuona watoto wetu wakiteseka na maradhi ya kurithi kwa sababu ya kushikilia mila bila kuuliza?
Au tuko tayari kuvunja mipaka, kuunganisha damu, na kujenga taifa lenye afya bora kwa vizazi vijavyo?

Ndugu zangu, huu ni wito wa mabadiliko.
Wazazi wape watoto wao uhuru wa kuchagua wachumba kutoka mikoa mingine. Vijana tupanue mitazamo yetu. Viongozi wa dini na jamii wahimize mchanganyiko huu wenye tija.

Kwa pamoja, tunaweza kuandika historia mpya ya kizazi chenye afya, nguvu, na mshikamano wa kweli wa kitaifa.

Mwanenu
Chavalikungu
 
Ngoja uyasikie ma Kataa Ndoa! Ka majinga vile! Hili la kwako mkuu umesema ukweli wa moyo wangu! Ndiyo maana hata mimi nilivuka Wilaya kadhaa! Mandugu yanabaki yanapiga kelele za kijinga wala siyasikilizi maana mengine yamefyatua maandazi!
 
Kwani lazima mkoa mwingine hata jamii tofauti ndani ya Mkoa mmoja si fresh tu ...Kama mimi msambaa nikioa mdigo si fresh ,mimi wa milimani yeye wa pwani.
 
Unaoa mdigo 🤓 unataka kumeza ulimi, ni kweli ila vizazi viwe tofauti tofaut
 
Back
Top Bottom