Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,957
- 20,498
Mgogoro na vita baina ya Jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF umeingia siku ya 10 huku kukiwepo na amri ya kusimamishwa mapigano kwa masaa 72.
Amri ya kusimamisha mapigano kuruhusu uokozi wa raia wa kigeni ilianza kutokea siku ya Ijumaa iliyopita ambapo watu waliruhuswa kusheherekea siku kuu ya Iddi. Lakini baadae Jumapili mapigano yakaendelea tena. Juzi kati jeshi la wanamgambo hao wa RSF wakakubali maombi ya mataifa ya kigeni kufanya uokozi wa raia wake.
Mpaka sasa nchi za Misri, Saudi Arabia, Iran, Syria, Ukraine, Hispania, Italia, Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, Marekani na zingine, zimetuma ndege za kijeshi na wanajeshi maalum kufanya shughuli za uokoaji wa raia wake. Djibouti ndo pamekuwa kituo cha kufikia wageni mbalimbali kabla kusafirishwa kwenda nchi zingine.
Watu wapatao 27,000 raia wa Sudan tayari wamekimbilia nchi jirani za Mali, Chad na Misri kwa njia ya barabara ambapo magari na mabasi yamekuwa yakibeba watu kupeleka katika nchi hizo na kuwa wakimbizi. Shirika la UNHCR ambalo lina kambi nchini Chad limekuwa likiendelea kupokea wakimbizi hao ambao idadi yao huenda ikaongezeka na kuzidi 100,000.
Uingereza ambayo imekuwa nyuma ya juhudi za uokozi wa raia wake, leo imenza rasmi zoezi hilo kwa kuwaelekeza raia wake kwenda katika kituo cha kijeshi cha Weid Seidna kilichopo kakazini mwa mji mkuu wa Khartoum. Uingereza imetuma kikosi cha jeshi lake la Raf kutokea kwenye kambi yake ya kijeshi iliyopo nchini Cyprus iitwayo Akrotiri.
Lakini serikali ya Uingereza imesisitiza kuwa ni raia wenye kubeba pasi za kusafiria za nchi hiyo na familia zao tu ndo watoruhusiwa kupanda ndege hizo kuokolewa na si raia wengine ambao ni wakazi wa namna yoyote ile nchini Uingereza kwa mujibu wa serikali ya Uingereza raia wapatao 1,000 tayari walikuwa wamewasiliana na wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo.
Ujerumani imetuma ndege sita za uokozi na kuokoa raia wapatao 500, Italia raia 400, Ukraine raia 138, Marekani zaidi ya raia 3000, India 3000, na raia wengine wametumia bandari ya Sudan au Port Sudani kuvuka kwa meli kwenda nchi za Yemen na Saudi Arabia.
Lakini mapigano hayo yakiwa yaendelea khasa katikati ya Khartoum, tayari kuna taarifa za kutekwa kwa maabara ya taifa ambayo imehifadhi sampuli na dawa za chanjo za magonjwa mbalimbali kama malaria na kipindupindu. Pia kuna taarifa za kuwepo kwa watoto wadogo wabebao silaha aina za AK 47 (watoto wa vita ) au Child Soldiers ambao wamekuwa wakiranda mitaani kutafuta chakula na kuanza kupora katika maduka, majengo na majumbaya watu khasa wale raia wa kigeni wanokimbia.
Watoto hawa ambao wana umri kati ya miaka 13 na 14 ni watoto hatari sana ambao wanapigana upande wa vikosi vya RSF. Kwa kawaida jeshi huwa na komandi moja ambayo hutoa amri wakti vita iikiendelea na hivyo kuwepo nidhamu baina ya wanajeshi. Kwa upande wa wapiganaji wa RSF hali ni tofauti kwani kila mpiganaji ana maamuzi yake na anachokikuta mbele yake huwa na halali kwake na hali hiyo ndo ilopelekea nchi nyingi kutuma vikosi vya jeshi kusaidia uokozi maana tayari kuna taarifa ya kushambuliwa kwa vikosi vy uokoaji.
Lakini yote haya yameanzaje na nini ni chanzo na pengine mwisho wake utakuwaje?
Mazingira khasa ya kuibuka kwa mapagano yaelezwa tofauti na vyombo vingi vya habari vikisema kuwa ni mvutano baina ya majenerali wawili Abdel Fattah-al Burhan na Dagalo au kama alijulikanavyo kama Hemedti. Taarifa zingine zadai kuwa majenerali Al Burhan na Dagalo ni majasusi wa nchi za magharibi na Russia. Zipo taarifa kadha wa kadha kuhusu majenerali hawa na ziara zao nchini Marekani na kule Kremlin.
Jenerali Al Burhan amekuwa akifanya ziara nyingi jijini Washington na ipo ziara ambayo alikutana na waziri wa nchi wa Marekani bwana Pompei mwaka 2020 na waziri wa ujasusi wa Israeli Eli Cohen mwaka 2022.
Lakini kinotokea sasa nchini humo ni kugombania madaraka au "power struggle" ambapo kila upande unashutumu mwenzie kutaka kupindua. Kwa muda mrefu tangia wanamgambo wa RSF ambao kiini chake ni wagamgambo wa Janjaweed washirikiane na jeshi kuongoza Sudan, bado uhusiano baina ya majenerali Burhan na Dagalo umekuwa ni wa kutiliana mashaka.
Jenerali Dagalo atokea Darfur ambayo nayo imekubwa na migogoro na vita kwa miaka 15. Sudan ya Kusini ilipata uhuru wake mwaka 2011 baada ya mapigano ya muda mrefu kati ya wapiganaji wa SPLA/M na majeshi ya serikali ya Khartoum. Sudan ilitawaliwa na Uingereza na katika utawala wake Uingereza iliigawa Sudan katika maeneo mawili ya Kaskazini kwenye waarabu ambako walijenga mashule, mahospitali na miundombinu mingine kama barabara , madaraja na huduma zingine za msingi kama makanisa na misikiti.
Lakini wakoloni hao wa Uingereza walisahau kabisa Sudan ya Kusini ambayo ina waafrika weusi na kuiacha kama ilivyo huku mji yake mkubwa ya Juba ukiwa ndani ya vumbi la jangwa. Hali hiyo ilifanya Sudan Kusini kuendesha kampeni ya vita na serikali ya Khartoum ambayo iliendelea kuwaadhibu wasudani weusi na baadae kuwapelekea kundi la Janjaweed ili kumaliza tatizo la wahamiaji waloitwa haramu ambao walikuwa wakitafuta maisha bira kutoka kaskazini.
Tangu ipate uhuru mwaka 2011 na kujiunga na umoja wa Afrika kuwa nchi ya 54 barani humo, Sudan ya Kusini ni nchi huru na inojitegemea. Sudan ya Kusini ina majimbo 10 ambayo wananchi wake wamekuwa kila mara walipigana kwa kuona hakuna maendeleo ya haraka yanofanywa na serikali ya Sudan ya Kusini.
Lakini ni kitendo cha jenerali Burhan kukubali kuwaleta Khartoum wanamgambo wa RSF kusaidia shughuli mbalimbali za kijeshi na pia kuanza mazungumzo ya kuwarasimisha wanamgambo hao wa RSF kuwa sehemu ya jeshi la Sudan ndicho kilicholeta zogo na vurugu na sasa mapigano makali.
Lakini wadadisi na wachambuzi wengi wanaamini kuwa mapigano ya sasa kati ya majenerali hao wawili Burhan na Dagalo yametokana na majenerali hao (Jenerali Burhan) kuunga mkono nchi za Marekani na NATO ambazo bado zasaidia nchi ya Ukraine ambayo iko kwenye vita na Russia, na Jenerali Dagalo kuwa upande wa Russia ambayo ina vikosi vyake Sudan ya Kusini.
Al Burhani pia asaidiwa na Misri kwa misaada ya vifaa vya kijeshi kutoka kwa raisi Abdel Fattah El- Sisi. Jenerali Dagalo ambae ni tajiri mkubwa wa dhahbu kutoka Sudan ya Kusini anasaidiwa pia na nchi za Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu UAE ambako amewahi kupeleka vikosi vya RSF kusaidia vita vya Yemen.
Kiasi kikubwa cha dhahabu inochimbwa Sudan ya Kusini yapelekwa nchini Russia kupitia UAE na vikosi vya jeshi la kukodi la Wagner vya Russia vipo Sudani Kusini vikilinda migodi ya dhahabu na visima vya mafuta. Russia imekuwa katika mazungumzo na jenerali Dagalo kuhusu kutaka kujenga kituo cha kijeshi katika bandari ya Sudan au Port Sudani kwenye bahari nyekundu.
Itakumbukwa baada ya Russia kuanzisha operesheni maalum ya kijeshi nchini Ukraine umoja wa mataifa uliweka azimio la kulaumu kitendo hicho cha Russia lakini Sudan haikushiriki kupiga kura kuunga mkono azimio hilo. Tangu wakati huo Marekani na washirika wake wamekuwa wakihangaka kuhaikisha Sudani inapata shida kwanza kwa kuondoa misaada ya fedha kutoka IMF na Benki ya Dunia, kuharibu mahusiano ya Sudan na Iran ambayo yaiuzia Sudan vifaa vya kijeshi, Russia na China.
Pia Marekani yaitaka Sudan kufunga mazungumzo na mijadala ya Russia kuweka kituo cha jeshi la majini kwenye bandari ya Sudan, kuimarisha uhasama na Iran na kuharibu uhusiano wa kijeshi kati ya Sudan na Iran na Russia na kuchagiza machakato wa kurudisha serikali ya kiraia chini ya waziri mkuu Abdallah Hamdok ambayo itapunguza usafirishaji wa dhahabu kwenda Russia ambapo yaaminika jambo hilo laisaidia sana Russia kukwepa vikwazo vya kiuchumi vilowekwa na Marekani na washirika wake.
Marekani imekuwa yaishutumu Russia kuwa nyuma ya mapinduzi yalomwondoa madarakani bwana Hamdok ambae kitaaluma ni mchumi na amesoma nchini Uingereza.
Mgogoro wa sasa zaidi umechochewa na majenerali hao wawili Burhan na Dagalo kutokukubaliana kwenye suala la kugawana madaraka na kwa vikosi vya RSF kuingizwa rasmi kwenye jeshi la Sudan. Jenerali Burhan binafsi hakubalini na suala hili lakini baadhi ya wanajeshi ndani ya jeshi wanaamini kuwa kuwaingiza RSF ndani ya jeshi kutapunguza na kuondoa hasira ya vijana wa RSF na pia maandamano yasokwisha mitaani kutoka kwa wananchi ambao wengi hawaungi mkono suala la RSF kuingizwa jeshini.
Jenerali Dagalo hakubaliani na suala la vikosi vya RSF kuingizwa jeshini hadi hapo serikali ya kiraia itapokuwa madarakani na pia anadai kuondolewa kwenye nafasi za kuu za serikali kwa wale viongozi wote wenye ukaribu na aliekuwa raisi Al Bashir ambae alipinduliwa mwaka 2019. Msimamo huu umemfanya jenerali dagalo kuungwa mkono na watu wengi wakiwemo wasomi vikundi mbalimbali vya kijamii ambavyo vimekuwemo katika mazungumzo ya kurudisha serikali ya ya kiraia.
Jumuiya ya kimataifa imekuwa ikionyesha wasiwasi wa kuwaingiza RSF jeshini na imekuwa ikisisitiza kuharakisha harakati za kuirudisha serikali ya kiraia chini ya Hamdok ambayo majenerali Burhan na Dagalo nao wana wasiwasi wa kukamatawa na kuwekwa jela kwa makosa mbalimbali ya uhalifu wa kivita.
Hadi sasa hakuna anaefahamu mgogoro huu utaisha vipi khasa baada ya jenerali Dagalo na vikosi vyake kuahidi kuendeleza mapigano. Hii ni aina ingine ya mifano hai kuwa bara la Afrika kwa sasa lipo katika kugombaniwa na mataifa makubwa. Sudan ya Kusini ina asilimia 75 ya utajiri wa maliasili ya visima vya mafuta, pia Sudan kaskazini ina dhahabu pamoja na madini mengine mbalimbali.
Hakika yanotokea Sudan yatupa funzo kubwa sana sisi waafrika na mstakabali wetu hapa duniani maana waafrika wenye ngozi nyeusi wamekalia maliasili yenye thamani ya mamilioni ya dola lakini ni raia kutoka nchi zingine ambao ndo wenye uwezo wa kuamua hatima ya mwafrika mweusi.