"Paka mtamu asikuambie mtu mjomba"

kaeso

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
551
96
Hii nimekutana nayo mtaani kwetu jana jioni wakati narudi toka kibaruani. Jamaa alikuwa anawasimulia wenzake namna paka alivyomtamu na namna anavyoandaliwa...............

"yaani yule unachemsha maji katika sufuria then unafunika, yakishachemka unamtumbukiza mzima mzima bila kumchinja kisha unafunika sufuria likiwa bado motoni, kwa sababu kumchinja ni kazi ngumu. Na pia tumboni mwake kuna sumu, kwa hiyo anapolalamika maji yataingia mdomoni kwenda kusafisha ile sumu...."

Ilibidi niondoke ili nisisikie ukatili zaidi anaofanyiwa paka. Watetezi wa wanyama wana kazi aisee!!!!
 
tan taraaaa!!
hii ndo naickia hapa leo...
cna wazo hata la uongo!
 
Acheni ushamba hamna kitu ambacho hakiliwi . Hata binadam ukikaa vibaya kule kongo unatafunywa. Ndio ije kuwa paka ?
 
Hatukatai kuwa paka analiwa(bado sina hakika) tatizo ni hayo maandalizi ya kwenda kumla yanavyokuwa ya kikatili!.. Kutumbukiza kiumbe chenye uhai kwenye maji yaliyochemka wewe unaona ni sawa?
 
Hii nimekutana nayo mtaani kwetu jana jioni wakati narudi toka kibaruani. Jamaa alikuwa anawasimulia wenzake namna paka alivyomtamu na namna anavyoandaliwa...............

"yaani yule unachemsha maji katika sufuria then unafunika, yakishachemka unamtumbukiza mzima mzima bila kumchinja kisha unafunika sufuria likiwa bado motoni, kwa sababu kumchinja ni kazi ngumu. Na pia tumboni mwake kuna sumu, kwa hiyo anapolalamika maji yataingia mdomoni kwenda kusafisha ile sumu...."

Ilibidi niondoke ili nisisikie ukatili zaidi anaofanyiwa paka. Watetezi wa wanyama wana kazi aisee!!!!

Mungu wangu, kweli dunia imeisha. Ni kwamba umaskini umezidi sana kiasi cha kukosa hela ya kwenda kununua nyama buchani na kuamua kuchinja paka au?
 
Hatukatai kuwa paka analiwa(bado sina hakika) tatizo ni hayo maandalizi ya kwenda kumla yanavyokuwa ya kikatili!.. Kutumbukiza kiumbe chenye uhai kwenye maji yaliyochemka wewe unaona ni sawa?

huyu mnyama ana roho saba bila kutumia maarifa haliki mpnz .
 
Ni zaidi ya ukatili Erickb52, sijawahi kusikia...daaah kama ni kweli hiyo ni dhambi isiyosameheka! Yanini kujitengenezea Karma mbaya hivyo?.
Ni kweli...tumeambiwa tuvitawale viumbe ila si kwa kiwango hicho...mtu wa hivyo anaweza mfanyia hata binadamu mwenzie.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom