Padriiii... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Padriiii...

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by The Boss, Dec 26, 2009.

 1. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Padri afumaniwa na kudai ametumwa na roho mtakatifu.

  Vichekesho na Udaku [​IMG]Pafri mmoja aliyekuwa na tabia ya kutembea na mke wa mtu kila mumewe alipokuwa kazini, siku moja siri ya uzinzi ilimfikia mwenye mali na kutakiwa arudi nyumbani ghafla. Jamaa alifanya hivyo na kukuta mlango umefungwa kwa ndani. Aligonga mkewe kwa woga wa kufumaniwa akachanganyikiwa, lakini Padri kwa kujiamini alivaa nguo na kujining’iniza dalini huku miguu ikionekana kwa chini.
  Jamaa alipoingia alianza kumshutumu mkewe;
  Jamaa: Nasikia unatembea na Padri?”
  Mke: Watu waongo mume wangu, huyo Padri yupo wapi?”
  Jamaa alianza kumtafuta kila kona lakini hakumuona alisahau kuangalia juu zaidi ya uvunguni na ndani ya kabati. Baada ya kuridhika kweli hakukuwa na mtu ndani, walikaa kitandani huku mkewe akiomba asiangalie juu.
  Padri aliyekuwa akining’inia juu ya kenchi mikono yake ilichoka na kujikuta akidondoka toka na kuanguka mbele ya yule mwanaume na mkewe. Wote walishtuka kumuona Padri, jamaa aliuliza;
  “Si huyu?”
  Padri: “Huyu nani, nimesikia mkiniteta kuwa natembea na mkeo, lakini kwa uwezo wa roho mtakatifu amenileta ndani mwako ili unithibitishie kuwa mimi natembea na mke wako”
  Jamaa alipoangalia juu hakuona sehemu yenye tundu alipopitia padri.
  Jamaa: “Umepitia wapi?”
  Padri: “Ni uwezo waroho mtakatifu aliyeniingiza kwa uwezo wake bila kuharibu bati wala kitu chochote”
  Jamaa: “Samahani baba Padri”
  Padri: “Nimekusamehe wewe na mkeo kwa kuwa hamkujua mtendalo”
  Jamaa: “Asante baba Padri walimwengu ni wagombanishi”
  Baada ya kusema hayo Padri alimfungulia mlango na kutoka huku mume akiamini kuwa ni kweli Padri kaletwa na roho mtakatifu. Kweli mjini shule.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Woow!....Angempekua mkewe kwenye dudu angepata ukweli..lol!
   
 3. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
   
Loading...