TANZIA Padri wetu mpendwa Ernest Donald Boyo wa Jimbo Kuu la Dar, Afariki Dunia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
2689073_TANZIA__Mhashamu_Askofu_Jude_Thaddaeus_Ruwaichi__Askofu_Mkuu_wa_Jimbo_Kuu_Katol__649_X...jpg

Wapendwa Mapadri, Mashemasi, Watawa na taifa lote la Mungu, Kristo.

Kwa masikitiko makubwa napenda kuwataarifu juu ya kifo cha Padri wetu mpendwa Ernest Donald Boyo wa Jimbo Kuu la DSM, aliyekuwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Chang'ombe.

Padri Boyo amefariki leo tarehe 10 Februari 2021 saa 1:30 usiku katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa akitibiwa. Taarifa zaidi juu ya taratibu za Mazishi zinapangwa na tutawataarifu. Tumuombee Pumziko la Milele Mbinguni.

ASANTENI.

+ Jude THADDAEUS Ruwa'ichi
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la DSM

 
Mwendo ameumaliza salama, na imani ameilinda.. Mbele yake nyuma yetu, tangulia padre. Pumzike kwa amani, Amina.
 
Rip padre
13. Naye Mungu akaendelea kumfanya Mfalme wa Wadanganyika awe na shingo ngumu asiweze hata kung'amua hatari iliyoko mbele yake. 14. Hayo yote yalifanyika ili anguko lake litimie kwa wakati, naam nalo anguko hilo liwe anguko kuu. 15. Hata waliokuwa wakimdanganya mfalme watamcheka na kusema hawakuwa pamoja naye katika maamuzi yake yenye kukosa hekima.
Chato 3:13-15
 
Back
Top Bottom