Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Dkt. Charles Kitima, amesema kikao chake na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, kilichofanyika Novemba 20, 2025 katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni mkoani Dar es Salaam kilikuwa cha binafsi na si mazungumzo ya Baraza la Maaskofu.
Akizungumza na wanahabari siku ya Jumatatu Desemba 1, 2025 juu ya masuala mbalimbali yanayohusu hali ya nchi baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Padri Kitima amesema alikwenda kwa Waziri Mkuu baada ya kualikwa binafsi, na si kama mwakilishi wa TEC.
Padri Kitima amesema hakupokea barua, ajenda wala maelekezo kutoka TEC kabla ya kwenda kwenye mazungumzo hayo, jambo ambalo linaonesha kuwa hakwenda kama sehemu ya taasisi.
Ameeleza kuwa Waziri Mkuu alimuita kupitia simu yake binafsi na akamweleza kuwa angependa wazungumze “kama watu wanaofahamiana”, akibainisha kuwa wamekuwa na uhusiano mzuri kwa muda mrefu.
Katika mazungumzo yao, Padri Kitima amesema waligusia pia matukio ya baada ya uchaguzi kwa namna ya kawaida ya kibinadamu, akisisitiza kuwa hayo si mazungumzo ya kitaasisi.
Amefafanua kuwa kama kungekuwa na mazungumzo ya kitaasisi, basi angeomba kibali kwa Rais wa TEC ambaye ndiye msemaji rasmi wa TEC na mwenye mamlaka ya kutoa tamko la baraza.