Padri Kawonga: Binti kusubiri upepo wa Kisulisuli ukuletee Mume ni ndoto za Alinacha

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,835
18,248
NA : PADRI KAWONGA

Katika nchi yetu Tanzania kuna uhuru wa kuabudu, lakini kwa namna moja au nyingine uhuru huu unatumiwa vibaya na baadhi wa watumishi wa Mungu. Baadhi ya watumishi nyakati za hivi karibuni wanatumia matatizo ya watu kama msingi wa kuanzisha au kuimarisha makanisa yao.

Ukienda katika makanisa hayo waabuduo wengi wao ni wajane, wagonjwa, wagani, waathirika wa HIV/ AIDS, wapweke, walioachwa, waliotendwa, waliofanyiwa ukatili, watu wenye matatizo ya kisaikolojia na misongo ya mawazo n.k

Ukitazama makundi haya ni ya watu wanaohitaji msaada wa haraka, lakini baadhi ya watumishi wa Mungu makundi haya ndio limekuwa shamba lao la kujivunia pesa.

Hivi karibuni wamesikika wachungaji fulani wakikusanya kundi la mabinti wasioolewa, walozalishwa na kuachwa, walotendwa, wanaotafuta waume wa kuwaoa na kuwaamisha kuwa wataletewa waume kwa upepo wa kisulisuli. Huku ni kutiana ujinga katika hali ya matatizo.

Hapa kilichohitajika ni hawa wachungaji kuwafanyia ushauri wa kiroho na kujua wanakosea wapi hadi wasiolewe. Pia sasa hivi katika nchi yetu tatizo hili ni kubwa, suluhu ya kudumu ni kuangalia malezi ya vijana na watoto katika familia.

Sio siri ukiona mabinti hawaolewi ujue kuna tatizo la mfumo wa malezi katika familia, jamii na ngazi za majifunzo. Nyanja hizo ndio watumishi wa Mungu jikiteni huko na sio kuwapumbaza mabinti zetu kuwa watapata waume kwa upepo wa kisulisuli.

Sasa hivi mtawaaminisha na kuwaozesha mabinti hao kwa watu ambao sio sahihi na madhara yake yatakuwa makubwa kama vile magonjwa kuongezeka, kupata walemavu wengi kwani wengi wa mabinti hao wanaenda kuozwa kwa wazee au watu ambao akili hazipo sawasawa.

Binti usiaminishwe habari ya upepo wa kisulisuli kuwa utakuletea mume bali fanya yafuatayo utapata mume, angalia tabia zako, uvaaji wako, mawasiliano, status yako ya mahusiano, uchumi wako na utegemezi, usafi wako, kubwa zaidi Ucha-Mungu wako.

Inawezekana mabinti wanakosea kwa kuhitaji mume mwenye sifa fulani aliyeandaliwa, lakini kumbuka sifa zingine unaweza kuzitengeneza wewe mfano mume mwenye pesa unaweza kumtengeneza wewe, mume mtanashaji, mnene au mwembamba, msomi, mtafutaji n.k

Wachungaji tuwasikilize kwanza matatizo yao kwanini hawaolewi, tukianzia hapo tutakuwa msaada mkubwa sana kwao, lakini kinyume na hapo ni ukandamizwaji na unyanyasaji na unyonyaji, tusiwageuze shamba la bibi kutokana na matatizo yao.

Nilipenda sana tamko la Mkuu wa nchi fulani Afrika Mashariki kwamba Watumishi wa Mungu wote lazima wawe na elimu ya dini kuanzia ngazi ya Diploma, na alifunga makanisa na misikiti yote ya watumishi wa Mungu wasio na Diploma. Hilo ni jambo litakaloondoa udanganyifu na unyanyasaji kwa miamvuli ya dini.

Ukifanya tathmini katika nchi yetu, wengi wa Watumishi wa Mungu si msaada kwa matatizo ya watu wa sasa bali tunawatia ujinga na kuwaaminisha miujiza. Hatuwahimizi waende hospitali wakapate tiba sahihi na yenye miujiza ya kweli kupitia Hospitali na Madaktari wenye hofu ya Mungu, hatuwahimizi kujitegemea bali tunawaombea miujiza ya kupata hela wakati sisi wenyewe tukitaka hela tunawaambia watuchangie.

Tunalo la kutafakari juu ya elimu ya watumishi wa Mungu katika nchi yetu.
Baadhi ya watu wanatumia vibaya vipaji walivyopewa na Mungu kama vile Sauti, Umbo, Sura, Ushawishi kujipachika miavuli ya watumishi wa Mungu kwa lengo la kujipatia fedha na hayo ndiyo matokeo ya kutiana ujinga kama vile upepo wa kisulisuli unaowachanganya mabinti zetu sasa.

Mwisho mwishoni Afrika tujikaze, Tanzania tujikaze katika kuabudu na kumwamini Mungu wa kweli.

By Fr. Kawonga
Holy Family Parish-Mkongo
 
Asante sana Padri, watasubiri mpaka mwisho wa dunia. Lakini Dr Lwakatare ni PhD holder hata kwa vigezo vya Fr Kawonga hawezi kufungiwa.
Umepona makombora ya juzi mdogo wangu? Hapo ndo utajua kuwa watu wanapenda uandike wanachokitaka wao, ukigeuka, wanakugeuka. Keep it up huwajui hawakujui watajijuuuuuuu.
 
Dada ningeyasoma ningepata depression
Kuna watu wakinijibu kunya nakaa kama masaa bila kuingia halafu sababu ya addiction naingia nawablock nimeshablock watu wengi tu sababu ya comments zao lakini inanipa faraja. We live today not tomorrow why be forced to choose for the future?

Nimechoka sana. Nawahurumia hao watu tunaotaka kuwajengea maisha mema. Hawajui kuwa sasa mabadiliko ni mitandaoni siyo barabarani kama haiwezekani. Ona watoto wa HK wanavyopigwa mabomu lakini wamelazimisha mpaka serikali ikaridhia kutoa ule mswada.

Sis thubutu uingie barabarani hata kudai kubdili maandishi ya kwenye khanga, utapata kipigo mpaka usahaulike kwa mme wako.
We live in primitive world.
 
Ulokole unauaibisha mwili wa Kristo
NA : PADRI KAWONGA

Katika nchi yetu Tanzania kuna uhuru wa kuabudu, lakini kwa namna moja au nyingine uhuru huu unatumiwa vibaya na baadhi wa watumishi wa Mungu. Baadhi ya watumishi nyakati za hivi karibuni wanatumia matatizo ya watu kama msingi wa kuanzisha au kuimarisha makanisa yao.

Ukienda katika makanisa hayo waabuduo wengi wao ni wajane, wagonjwa, wagani, waathirika wa HIV/ AIDS, wapweke, walioachwa, waliotendwa, waliofanyiwa ukatili, watu wenye matatizo ya kisaikolojia na misongo ya mawazo n.k

Ukitazama makundi haya ni ya watu wanaohitaji msaada wa haraka, lakini baadhi ya watumishi wa Mungu makundi haya ndio limekuwa shamba lao la kujivunia pesa.

Hivi karibuni wamesikika wachungaji fulani wakikusanya kundi la mabinti wasioolewa, walozalishwa na kuachwa, walotendwa, wanaotafuta waume wa kuwaoa na kuwaamisha kuwa wataletewa waume kwa upepo wa kisulisuli. Huku ni kutiana ujinga katika hali ya matatizo.

Hapa kilichohitajika ni hawa wachungaji kuwafanyia ushauri wa kiroho na kujua wanakosea wapi hadi wasiolewe. Pia sasa hivi katika nchi yetu tatizo hili ni kubwa, suluhu ya kudumu ni kuangalia malezi ya vijana na watoto katika familia.

Sio siri ukiona mabinti hawaolewi ujue kuna tatizo la mfumo wa malezi katika familia, jamii na ngazi za majifunzo. Nyanja hizo ndio watumishi wa Mungu jikiteni huko na sio kuwapumbaza mabinti zetu kuwa watapata waume kwa upepo wa kisulisuli.

Sasa hivi mtawaaminisha na kuwaozesha mabinti hao kwa watu ambao sio sahihi na madhara yake yatakuwa makubwa kama vile magonjwa kuongezeka, kupata walemavu wengi kwani wengi wa mabinti hao wanaenda kuozwa kwa wazee au watu ambao akili hazipo sawasawa.

Binti usiaminishwe habari ya upepo wa kisulisuli kuwa utakuletea mume bali fanya yafuatayo utapata mume, angalia tabia zako, uvaaji wako, mawasiliano, status yako ya mahusiano, uchumi wako na utegemezi, usafi wako, kubwa zaidi Ucha-Mungu wako.

Inawezekana mabinti wanakosea kwa kuhitaji mume mwenye sifa fulani aliyeandaliwa, lakini kumbuka sifa zingine unaweza kuzitengeneza wewe mfano mume mwenye pesa unaweza kumtengeneza wewe, mume mtanashaji, mnene au mwembamba, msomi, mtafutaji n.k

Wachungaji tuwasikilize kwanza matatizo yao kwanini hawaolewi, tukianzia hapo tutakuwa msaada mkubwa sana kwao, lakini kinyume na hapo ni ukandamizwaji na unyanyasaji na unyonyaji, tusiwageuze shamba la bibi kutokana na matatizo yao.

Nilipenda sana tamko la Mkuu wa nchi fulani Afrika Mashariki kwamba Watumishi wa Mungu wote lazima wawe na elimu ya dini kuanzia ngazi ya Diploma, na alifunga makanisa na misikiti yote ya watumishi wa Mungu wasio na Diploma. Hilo ni jambo litakaloondoa udanganyifu na unyanyasaji kwa miamvuli ya dini.

Ukifanya tathmini katika nchi yetu, wengi wa Watumishi wa Mungu si msaada kwa matatizo ya watu wa sasa bali tunawatia ujinga na kuwaaminisha miujiza. Hatuwahimizi waende hospitali wakapate tiba sahihi na yenye miujiza ya kweli kupitia Hospitali na Madaktari wenye hofu ya Mungu, hatuwahimizi kujitegemea bali tunawaombea miujiza ya kupata hela wakati sisi wenyewe tukitaka hela tunawaambia watuchangie.

Tunalo la kutafakari juu ya elimu ya watumishi wa Mungu katika nchi yetu.
Baadhi ya watu wanatumia vibaya vipaji walivyopewa na Mungu kama vile Sauti, Umbo, Sura, Ushawishi kujipachika miavuli ya watumishi wa Mungu kwa lengo la kujipatia fedha na hayo ndiyo matokeo ya kutiana ujinga kama vile upepo wa kisulisuli unaowachanganya mabinti zetu sasa.

Mwisho mwishoni Afrika tujikaze, Tanzania tujikaze katika kuabudu na kumwamini Mungu wa kweli.

By Fr. Kawonga
Holy Family Parish-Mkongo
 
Watu kiiiila kitu
I receive
Hata yanayohitaji utoke ukafanye jambo wao ni NAPOKEA!
kutwa kucha NAPOKEA!
tunaandaa kizazi cha maomba omba wavivu na wajinga
 
Asante father, mfumo wa malezi una tatizo. Nasubiri wale wa "na wanaume je, mbona huja wasema!
 
Kwamba Watumishi wanawaaminisha watu watapata Pesa kwa njia za Miujiza wakati wao wwnyewe wakitaka pesa wanataka wachangiwe.
Hivi kweli hii ni ajabu ya karne.....kuna mwingine yupo Arusha ....kama unahitaji upate fedha anakwambia mrushie 10% au 20% kwenye simu fasta
 
Back
Top Bottom