Padri Karugendo: Spika huyu si bora kwa Bunge la Wananchi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Padri Karugendo: Spika huyu si bora kwa Bunge la Wananchi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sumaku, Jul 9, 2009.

 1. S

  Sumaku Member

  #1
  Jul 9, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta, amesema kuwa hoja ya Mbunge wa Nzega, Lucas Selelii (CCM), kwamba fedha za ujenzi wa barabara ya Chalinze, Segera hadi Tanga, zilianza kutumika kabla ya kuidhinishwa na Bunge, ni ya msingi kutokana na utata wa takwimu uliojitokeza : “ Selelii, alipopitia kitabu cha miradi ya maendeleoeo kwa mwaka huu wa fedha 2009/2010, ukurasa wa 189, item 4189, inaonyesha kuwa kwa miaka ya nyuma, hakuna fedha zilizotengwa, jambo lililomfanya aamini kuwa matengenezo yanayoendelea hivi sasa yanatokana na fedha zinazoombwa kwa mwaka huu wa fedha na ambazo hazijaidhinishwa na Bunge hili”.

  Ufafanuzi wa Spika ni kwamba mchakato wa kutengeneza barabara hiyo, ulianza mwaka 2006 na fedha zake jumla ya shilingi bilioni 10.4 ziliidhinishwa na Bunge mwaka 2006/2007, kwa matarajio ya kukamilisha usanifu na kuanza ukarabati wa barabara hiyo. Na kwamba kazi ya ukarabati inayoendelea sasa ,fedha zake ziliidhinishwa na Bunge katika mkutano wa 12 na fedha zilioombwa katika mwaka ujao wa fedha 2009/2010 shilingi 22,844,500,000 ni kwa ajili ya kufanyia ukarabati mkubwa wa barabara hii kwa fedha za DANIDA ambazo ni sh bilioni 17.6 na sh milioni 50 fedha za ndani; na kwamba ukitazama ukurasa husika wa 189, alioutaja Selelii,mradi wa ukarabati wa barabara Chalinze-Segera-Tanga kwa mwaka wa fedha 2007/2008 na 2008/2009, hakuna fedha ziizotengwa ila mwaka huu wafedha 2009/2010, inaonyesha kiasa cha fedha kilichotengwa ni sh 22,844,500,000.

  Kwa maelezo ya Spika, utata huu unatokana na mabadiliko ya miundo katika Wizara. Miundo inabadilika ndani ya wizara bila Bunge kutaarifiwa! Na Mheshimiwa Spika, analiona hilo ni jambo la kawaida; analiona si jambo la kuwajibishana, analiona si jambo la kuiambia Serikali imekosea! Na bado anataka aonekane ni Spika wa kasi na viwango!

  Kwa uangalifu mkubwa, ili isionekane anaikosoa serikali, Spika alitoa ushauri: “ Kwa kuwa utata huo unatokana na mabadiliko ya miundo, ni ushauri wangu kuwa ili kuondokana na matatizo kama haya kunapotokea na mabadiliko ya miundo ndani ya wizara, hasa mabadiliko yale yanayohusiana na miradi mikubwa, ni vyema fedha zinazotengwa katika miradi ya aina hiyo, zikabainishwa kwa uwazi zaidi katika vitabu vya bajeti”.

  Spika, anaogopa nini kuiambia serikali kwamba imekosea? Ni wazi serikali yenyewe inaongozwa na chama chake cha CCM, lakini Spika si wa CCM, hata kama yeye ni Mbunge wa CCM, lakini baada ya kukalia kiti cha spika, yeye ni “mali” ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; ni wajibu wake kulitendea haki taifa maana yeye anasimamia “sauti ya uwakilishi” ya taifa zima. Kati ya kazi za Bunge, ni kuisahihisha serikali; kama spika anaogopa kufanya kazi hiyo ni dalili tosha kwamba kazi hiyo iko juu ya uwezo wake!

  Kuna maswali mengi ya kuuliza juu ya mwongozo wa Spika: Je kama Selelii, angekuwa ni Mbunge wa upinzani, uamuzi wake ungekuwa kama huu alioutoa? Endapo Selelii angethibitika kusema uongo, alikuwa akikabiliwa na adhabu ya kusimamishwa kuhudhuria mkutano mmoja wa Bunge, kama ilivyotokea mwaka 2007 kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), aliyesimamishwa kuhudhuria mkutano mmoja wa Bunge baada ya Bunge kubaini kuwa alisema uongo kuhusu kusainiwa kwa mkataba wa mgodi wa madini wa Buzwagi nje ya nchi katika mazingira ya rushwa.

  Kama Zitto, angekuwa CCM, hapana shaka ujanja ungetumia kusudi Zitto asionekane ana kosa la kulidanganya Bunge na Buzwagi ingeshagiliwa! Kumekuwa na mwelekeo wa Spika Sitta, kuwalinda kwa gharama kubwa wabunge wa CCM na kuikingia kifua serikali. Tuna mifano mingi: Juzi Zitto, aliposema Naibu waziri Sumari, alijibu hovyo hovyo, Spika alimlazimisha kufuta usemi, maana kanuni za Bunge zinazuia lugha ya kuudhi;
  lugha hiyo ikitumiwa na wabunge wa CCM hakuna mwongozo wa Spika.

  Badala ya kuweka mbele maslahi ya Taifa, Spika anashughulika na Chama chake; anaweka mbele maslahi yake binafsi badala ya kuyatanguliza ya taifa. Ukweli ni kwamba akikilinda Chama chake, na chama chake kitamlinda wakati wa uteuzi kugombea tena kiti cha ubunge na labda kama ana matumaini ya kupanda zaidi, kuwa mwenyekiti wa Chama chake au kugombea urais. Hivyo kwa mtizamo wa kina, msimamo wake wa kukilinda chama na serikali una manufaa zaidi kwake kuliko kitu kingine kile. Spika wa namna hii si bora kwa Bunge la wananchi!

  Swali jingine ni je kwanini imechukua siku nyingi Serikali kutoa jibu. Mbunge Selelii, aliuliza swali tarehe 15.6.2009 jibu limepatikana tarehe 30.6.2009, kama tatizo lilikuwa ni kukosea takwimu kwanini ichukue siku zote hizo? Takwimu zote zinakuwa kwenye kompyuta, ni kiasi cha kubofya na kufanya masahihisho.

  Inawezeka Serikali imechelewa katika harakati za kujipanga kuandaa jibu? Kama barabara hii bado ina masalio ya fedha, ambazo tunaaminishwa kwamba ndo zinatumika hivi sasa kabla Bunge halijabariki matumizi ya mwaka 2009/2010; kwanini zitengwe tena fedha kwa barabara hii? Nafikiri hili ndilo swali la mheshimiwa Selelii na ndilo swali la Watanzania. Bila kuwa makini kwenye bajeti ni kuliangamiza taifa letu. Fedha zitatengwa na kuishia kwenye mifuko ya watu au kuelekezwa kwenye uchaguzi wa 2010.

  Na je kama kweli kulikuwa na kosa la takwimu, kwanini alione Selelii, peke yake? Alipata taarifa mapema? Inawezekana kwenye wizara hiyo kuna vijana wanaochukia ufisadi na kuamua kuvujisha habari hizo kwa Mbunge anayeweza kusimama na kupinga ufisadi? Selelii, ni kati ya wabunge watano wa CCM, wanaoaminika kusema bila kuogopa, jimbo lake ni kati ya yale yaliyotangazwa kuwa wazi na gazeti mojawapo hapa nchini hadi Mheshimiwa Anna Kilango Malecela, akapiga kelele.

  Au Selelii ndiye mbunge makini peke yake ndani ya bunge? Yeye, alikuwa na maslahi gani kufuatilia takwimu za barabara. Inawezekana wabunge wengine waliziona kasoro hizo wakamezea au hawakuwa na muda wa kupekuwa bajeti ukurasa hadi mwingine? Inawezekana hata takwimu za wizara nyingine zina makosa, kwa vile wabunge hawazichunguzi kwa makini – zinapita hivyo hivyo?

  Je, kama si Mheshimiwa Selelii, takwimu hizi zingesahihishwa lini? Au kosa hili halina athari kwenye bajeti na utendaji mzima wa kujenga Barabara, si ya Chalinze peke yake, bali hata na barabara nyingine? Kwa vyovyote vile, kama Mheshimiwa Selelii, yuko sahihi, basi serikali ina makosa. Haiwezekani serikali kuandaa bajeti yenye makosa: Hata kama makosa hayo yameandaliwa kwa makusidi mazima, kwa lengo la kuingiza kwenye bajeti fedha zinazoelea tu bila kuwa na lengo maalum ili zichotwe kiulaini, bado ni kosa kubwa maana huo ni udanganyifu na uhujumu uchumi.

  CHANZO:
  kwanzajamii.com
   
 2. B

  Bontowar JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 524
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Hao mapandri sasa wataka kuwapanda watu vichwa
   
 3. B

  Bull JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2009
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mapadre wanakosa muelekeo, wanaingilia siasa wanshindwa kutekeleza wajibu wao makanisani, kukosa mwelekeo wanashindwa hatakuelewa kua u-gay nilaana ya mungu na kubaka watoto ni dhambi. Put your houses in order kabla ya kuingilia siasa. Malabouk
   
 4. B

  Bontowar JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 524
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Badala wainangalie biblia kama kweli inasema wasioe wanaleta siasa kwenye dini

  inashangaza saana sijui huwa hawaisomi yote
   
 5. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Wakuu, Binafsi sioni kosa lolote alilofanya huyu Padri kuhoji kwa manufaa yetu sote. Kwani naye si Mtanzania Bana? Mbona mnaleta chuki ambazo hazina msingi?

  Padri Karugendo tupo pamoja katika kufichua maovu yanayotendeka Serikalini na kwenye vyombo vya uwakilishi wa wananchi.

  Ubarikiwe sana
   
 6. B

  Bull JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2009
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Siasa na dini havichanganywi, bora ajiunge kwenye siasa mja kwamoja, kwa sababu shughuli ya kanisa pekee nikazi kubwa kunauchafu mwing kule, sasa wanasiasa nao waingilie kanisa ? sinachuki anatakiwa awajibike kwake kwanza kunauchafu mwing tu, nahao wasiasa wanakuja kila J'pili awavute awekemee kama anataka kukataza maovu, He should clean his house first, asilete blablaa
   
 7. B

  Bontowar JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 524
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Anatakiwa kufuta utafu wape na waumini wake Au aende chimwaga akawahubirie dini huko
   
 8. idumu

  idumu Member

  #8
  Jul 10, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu ni mwandishi wa makala za RAIA MWEMA HAMJUI nini?? Na huyu si padri maana aliachishwa upadri miaka ya nyuma huko. Huyu ni sawa na Dr Slaa. Naye alikuwa padre na akaaomba yeye mwenyewe kwa Papa kuacha updre.
  Habari ndo hiyo na msikasirike bila kujua, Jina tu hilo na si padre. MSOME MAGAZETI YA TZ, MTAWAJUA WAANDISHI WA MAKALA

  Tembelea Raia Mwema - Muungwana ni Vitendo
   
 9. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Biblia haijasema wasioe. Huo ni utaratibu waliojiwekea wenyewe kama mapadre wa kanisa katoliki.
   
 10. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #10
  Jul 10, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Uchafu upi huo mkuu? Unaweza kufafanua?
   
 11. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #11
  Jul 10, 2009
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Kivipi? Hii ni hoja yake kama mwandishi ,mtanzania , na ukitaka sana X priest. Usirukie treni kwa mbele mjomba.
   
 12. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #12
  Jul 10, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Kupanda watu vichwa kivipi, hawatakiwi kuhoji ama kukosoa? Wao si waTZ? Inaelekea unachuki binfsi na mapadre na kwamba kwa kiasi kikubwa wanagusa maslahi yako km sio yenu?
   
 13. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #13
  Jul 10, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Those who say religion has nothing to do with politics do not know what religion is. "Mohandas K. Gandhi"
   
 14. n

  nyakyegi Member

  #14
  Jul 10, 2009
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  ''thinking outside the box''
  kuwa padre haimanishi kutoyaona yanayoendelea nchini mwako.
   
 15. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #15
  Jul 10, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwani nyinyi mnamsema mtu au hoja hapo huu mbona sisi Wana JF tunaelekea kubaya nasi
   
 16. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #16
  Jul 10, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  asante mkuu kwa kutoa muongozo maana naona waungwana walikuwa wanapotoka katika kujadili hili
   
 17. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #17
  Jul 10, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli Padri Privatus karugendo ni mchambuzi mzuri sana wa masuala ya kijamii. Yeye ni mkaazi wa kule kayanga, Karagwe Bukoba. Na Mola ameibariki familia yote ni waandishi ukianzia na kaka yao Primus vile vile Prudence karugendo wote ni wachambuzi wazuri wa mambo ya jamii na wanatumia sana kalamu zao kupinga ufisadi huko Tanzania.

  Tumekusikia Padre Privatus karugendo
   
 18. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #18
  Jul 10, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  NAITAMANI signature ya Nyani Ngabu................
  Watu tumajeaa FITINA, UDINI, DHARAU, UJUAJI mpaka tunashindwa kuona POINTS muhimu, haya bwana alafu mkija mnailaumu CCM, kwa strahili hii tunastahili tunayoyapata......
   
 19. K

  Kieleweke Member

  #19
  Jul 10, 2009
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Idumu,
  Inaelekea wewe ni mkatoliki na unajua vizuri historia za Karugendo na Dr. Wilbroad Slaa.

  Lakini inaelekea wewe ni mkatoliki usiyejua kinachofundishwa na imani kanisa lako.
  Toka lini kanisa katoliki likawa na uwezo wa kumvua mtu upadri. Eti Dr. Wilbroad Slaa si padri tena. Wala Karugendo si padri unataka tumuite ni mwandishi wa makala tu.

  Nyinyi ndiyo wale walioandika askofu Jacob Koda avuliwa uaskofu wakati upadri na uaskofu ni madaraja ya sakramenti.

  Hebu elimika kwa kusoma makala ifuatayo kwa kuclick hapa kwenye mabano ( Blog Archive Padri akiachishwa upadri tujiadhari nini toka kwake?)

  Ukishaelimika ndiyo turudi kwenye mada iliyopo jamvini.
   
 20. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #20
  Jul 10, 2009
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huwa ukiingia humu janvini ukweli unabakia pale pale kuwa watanzania twadandia sana. Karugendo namjua ni mwandishi wa miaka zaidi ya kumi akiwa kama mwandishi wa makala magazetini.

  Hapa kumbe hatusomi magazeti ni madomo kaya tu.
   
Loading...