Padri amkimbia muumini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Padri amkimbia muumini

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Parachichi, Aug 1, 2011.

 1. P

  Parachichi JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2011
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Padri amekaa katika chumba cha kuungamisha, kanisani hakuna mtu. Mara muumini mmoja
  akaingia, akapiga magoti upande wa pili wa meza na kufanya ishara ya msalaba
  akaanza kuungama.

  Akisema "Padri naungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana"

  Padri "endelea"

  "Bosi wangu aliniita nyumbani kwake akaniambia amegundua nimeiba shilingi milioni
  50, akasema nisipotoa maelezo ya kutosha atanipeleka polisi , ukweli mimi naogopa
  kufungwa, nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikachomoa
  bastola nikamuua.
  Je ! Yesu atanisamehe?"

  Padri "utasamehewa"

  "Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa, kutazama loh, mke wa
  bosi. Akaniuliza nimemfanya nini mume wake. Kutazama huku na huku nikagundua tuko
  wawili peke yetu, nikamuua na yeye.
  Je ! Yesu atanisamehe na hiyo?"

  Padri "utasamehewa"

  "nikatoka nje, nikawasha gari niondoke lakini mlinzi akakataa kufungua geti akasema
  amesikia kama kishindo hivi! Nikaona ananiwekea kiwingu. Kutazama huku na huku
  nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua.
  Je ! Yesu atanisamehe?"

  Padri "utasamehewa"

  "nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati napanga kuja kanisani
  kuungama dhambi mtoto wa bosi akabisha hodi nikawaza mambo gani tena ! Akasema
  amefika nyumbani na kukuta yaloyotokea, lakini akanionyesha diary ya baba yake
  inayoonesha kuwa nilikuwa na appointment naye kabla hajafa. Nikamuuliza nani
  mwingine anajua? akasema ameanzia kwangu kisha atakwenda polisi. Nikatazama huku na
  huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Diary nikaichoma moto.
  Je ! Yesu atanisamehe na hilo?"

  Padri - kimya.......................................

  "Padriiii, Je Yesu atanisamehe kwa hilo?"

  - kimya..................................

  Jamaa kutazama kwenye box la maungamo padri hayupo.
  Lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo za mapadri kama linatikisika!
  Kufungua akamuona padri kajificha katikati ya majoho anatetemeka sana.

  "Sasa baba Paroko mbona umenikimbia?"

  Padri kwa taabu akajibu ;

  "nilitazama huku na huku nikagundua kuwa tuko wawili peke yetu........"
   
 2. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  hahahahahahahahahaha!!!!! Nikaangalia huku na huku tukajikuta tuko wawili!!!! Nilijua ungenimaliza na mimi!!
   
 3. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Teh teh teh....
   
 4. Janja PORI

  Janja PORI JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 808
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  hi kali
   
 5. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  hahahaaa, kwani alisahau kuwa na Muumba alikua pamoja nao? mmmh huyu Padre atakua mchina huyu si bure..........ok, ngoja nikapate lunch hapo Bulukutu Bar...aaahaaa astakafyulilahi kumbe nimefunga jamani ningeharibu swaumu yangu...hahaaaa padre bana
   
 6. A

  Aine JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mbona hii ilisharushwa hapa jamvini? sikumbuki ilikuwa na heading gani
   
 7. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
   
 8. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  hehehehehe.. lol
   
 9. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Angalau hata stress zinapungua kwa staili hii
   
 10. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Padri angefyatuliwa
   
 11. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Teh teh teh
   
Loading...