Mkare
JF-Expert Member
- Dec 21, 2010
- 504
- 79
Padri amekaa katika ki-box cha kuungamisha, kanisani hakuna mtu.
Mara muumini mmoja akaingia, akapiga magoti upande wa pili na kufanya
ishara ya msalaba akaanza kuungama.
"padri naungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana"
"endelea"
"bosi wangu aliniita nyumbani kwake akaniambia amegundua nimeiba
shilingi milioni 50, akasema nisipotoa maelezo ya kutosha atanipeleka polisi.
Sasa ukweli mimi naogopa kufungwa, nikatazama huku na huku nikagundua
tuko wawili peke yetu, nikachomoa bastola nikamuua. Yesu atanisamehe?"
"utasamehewa"
"Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa, kutazama
loh, mke wa bosi. Akaniuliza nimemfanya nini mume wake. Kutazama huku
na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua na yeye. Yesu atanisamehe
na hiyo?"
"utasamehewa"
"nikatoka nje, nikawasha gari niondoke lakini mlinzi akakataa kufungua geti
akasema amesikia kama kishindo hivi! Nikaona ananiwekea kiwingu. Kutazama
huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Yesu atanisamehe?"
"utasamehewa"
"nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi akabisha hodi nikawaza mambo gani tena. Akasema amerudi nyumbani na kukuta yaloyotokea, lakini akanionyesha diary ya baba yake inayoonesha kuwa nilikuwa na appointment naye kabla hajafa. Nikamuuliza nani mwingine anajua, akasema ameanzia kwangu kisha atakwenda polisi. Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Diary nikaichoma moto. Yesu atanisamehe na hilo?"
- kimya........
"padri, Yesu atanisamehe kwa hilo?"
- kimya.........
Jamaa kutazama kwenye kibox padri hayupo. Lakini kwenye kona moja akaona
kabati la ngou za mapadri kama linatikisika. Kufungua akamuona padri kajificha
katikati ya majoho anatetemeka.
"sasa baba mbona umenikimbia?"
padri kwa taabu akajibu
"nilitazama huku na huku nikagundua kuwa tuko wawili peke yetu........"