Padri adaiwa kumlawiti mtoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Padri adaiwa kumlawiti mtoto

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BONGOLALA, Nov 4, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  Imeandikwa na Nakajumo James, Moshi; Tarehe: 4th November 2010

  JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linamsaka Padri Stanslaus Sala wa Kanisa Katoliki jimbo la Moshi, Parokia ya Mtakatifu Theresa Lego Muro kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa miaka 14 kwa ahadi ya kumpa rosari na mche wa sabuni.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Lucas Ng'hoboko, alisema jana kwamba, Padri huyo mkazi wa kata ya Kilema Kusini, Moshi Vijijini, inadaiwa alifanya tendo hilo Oktoba 30, saa 2 usiku.

  Alisema, kiongozi huyo wa dini, alimtendea hayo mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa ambaye alikuwa mfanyakazi wa kuhudumia mifugo katika Parokia hiyo, baada ya kumaliza elimu ya msingi mwaka huu.

  Kamanda Ng'hoboko alisema, Polisi ilipokea taarifa za tukio hilo Oktoba 31 katika kituo kikuu cha Polisi Moshi na mtoto huyo kupewa hati maalumu ya matibabu (PF3).

  Alisema, mtoto huyo alifanyiwa uchunguzi katika hospitali ya mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi na kwamba mtuhumiwa ametoroka.

  "Tangu tumepata taarifa za tukio hili la kikatili, askari wangu wamekuwa wakifanya msako dhidi ya Padri huyo ili akikamatwa sheria iweze kufuata mkondo wake," alisema.

  Kwa upande wake, akizungumzia tukio hilo, baba wa mtoto huyo, Amati Lyamuya, alisema kitendo hicho ni cha kikatili na kimeidhalilisha familia yake.

  Mtoto huyo alidai kwamba, Padri alimchukua na kudai kuna makosa ameyafanya na kwamba alistahili adhabu ingawa hakumweleza aina ya kosa, lakini hakukataa akiamini hana kosa.

  Alidai kuwa waliondoka na Padri na kuelekea seminari ya Karumali walipofika Kisanja msituni, Padri alimwamuru ashuke kwenye gari na kumlaza mlango wa mbele na kumwingilia kimwili.

  "Tukiwa njiani kuelekea eneo hilo aliniambia kuwa baba yangu ameagiza nipewe adhabu … tulipofika kwenye ule msitu, alinivua nguo na kuniingilia, nilipiga kelele bila mafanikio na tuliporudi Parokiani, alinipa rozari na sabuni ili nisiseme," alidai mtoto huyo.

  Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kilema Kusini, Adamu Mbuya, naye alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo.

  source: www.habarileo.co.tz
   
 2. Meale

  Meale Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 24, 2009
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeisikia hii habari leo redioni, yaani ukifuatilia maisha binafsi ya baadhi ya hawa viongozi wetu wa dini mpaka unachoka kabisa , unatamani hata usiwe na dini.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Huyu ni jambazi aliyeingia kwenye kazi ya upadri kwa kufanikisha malengo binafsi...Hana wito!
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  JK in business
   
 5. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Duh!jamani mapadri mbona mnapenda kubashia wenzenu hivi mnaona ufahari gani!!!
   
 6. Mahai

  Mahai JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hawa viongozi wa dini hawafai!!!! Kwa nini wasiruhusiwe kuoa kabisa?
   
 7. Andrew Kellei

  Andrew Kellei JF Gold Member

  #7
  Nov 4, 2010
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Katika msafara wa mamba na kenge pia wanakuwepo.
  Huyo ni MBWAMWITU ALIYEVAA NGOZI YA KONDOO.
  Hastaili kuitwa Mwanakondoo na amelidhalilisha kanisa.
  Ni bora hawa wachunga kondoo wakaanza kuangaliwa upya.
   
 8. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Baada ya kusoma seminary na kukaa na mapadre kwa karibu sana, nilikuja kugundua mambo mengi ambayo mwanzoni sikuyajua. Nilitamanai sana kuwa padre wakati niko mdogo lakini baada ya kupita seminarini nilikuja kuona kumbe ni upuuzi tu, ila ninacho wasifu, elimu ya kanisa ni nzuri sana kiasi kwamba ukiingia mtaani lazima usumbue sana watu.

  Ni wakati sasa kwa Vatican kuitafakari upya doctrine ya kanisa katoliki na ikiwezekana hawa watu waruhusiwe kuoa. Umekuwa ni mchezo wao sasa wa kawaida kufanya maovu ya aina hiyo. Lakini Mt. Paulo anaendelea kuwakumbusha kuwa wale ambao hawataweza kuwa kama yeye Paulo (kukaa bila kuoa) basi na waoe. Celibacy inaonekana kuwashinda wengi sana. Mnamkumbuka Fr. Kimaro............naye alichakachua mtoto hivyo hivyo!

  God have mercy on us!
   
 9. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #9
  Nov 4, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Masikini jamani tuwafiche wapi watoto wetu? mitaani hakufai, mashuleni ndo usiseme sasa hata huku ambako ndio tegemeo letu kuwa ni mahali pema??? Eh MUNGU tunusuru waja wako.

  Halafu hapo kwenye red......sio Child labour hii?
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,373
  Likes Received: 19,612
  Trophy Points: 280
  wtakwambia ni mtumishi wa kanisa anamtumikia Mungu
   
 11. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Hapana Mkuu. Usifike hapo pa blue. Ifanye dini kuwa uhusiano kati yako na Mungu - padre asikukwaze.
   
 12. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2010
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Kwani hakuna waliooa wanaowalawiti watoto wao hata mabinti zao? Tatizo la kimaadili ni la kila mtu na hivyo inabidi jamii iangalie jinsi gani tuweze kurudisha maadili yetu.
   
 13. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #13
  Nov 5, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  mimi nilifikiria gonjwa hili la kulawiti watoto liko ulaya na amerika tu! Kumbe hata huku kwetu lipo? Ee mola wetu wanusuru watoto wetu na hawa mafataki wa kanisa!!!

  ili kudhibiti uhalifu huu kanisa linalazimika kuwa hasi mapadri na maaskofu wake ili wapoteze nguvu zao za kiume na kuwanusuru watoto wetu!!!


  hatuwezi kulalamika kila siku na kuwaacha hawa wachungaji wa kondoo waendeleze ufataki wao!! Ni lazima tuje na hatua za kuchukua kwa sababu sioni kwanini kanisa liajiri mwanaume mzima aliekamilika kiume halafu haruhusiwi kuoa!!! Huku ni kumpa adhabu ambayo hataweza kuvumilia na mwisho wake akizidiwa kama akimkosa mtoto basi anaweza hata kumfataki bata au kuku atakaepita mbele yake!!!!


  chonde chonde kanisa chukueni hatua sasa kuruhusu ndoa kwa viongozi wetu sababu ukisoma biblia takatifu hakuna mahali yesu anaharamisha ndoa za mume na mke ila ni kanuni za kanisa iliyojipangia yenyewe ndio inayowakataza mapadri na maaskofu wasioe sasa mimi hili la askofu wa huko moshi kumfataki mtoto halinishangazi!!!
   
 14. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #14
  Nov 5, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  :A S angry: madhara ya kukatazwa kwao kuoa ndio chanzo cha hayo. na kama wanafanya hivi wakiwa nje je wanapokuwa ma-brother kwenye mahema yao inakuwaje? tusiliangalie tatizo likiwa nje embu tulifuate huko ndani ndipo tuje na majawabu na nini kifanyike ili kuepuka matatizo hayo.:tape:
   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Nov 5, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Na hao wazazi hawajifunzi tuu?? wazazi nao waunganishwe kwene kesi.ala!
   
 16. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #16
  Nov 5, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  ushawishi mkuu unatokana na athari za kimazingira, embu tazama hao wanaofanya matendo hayo....
   
 17. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #17
  Nov 5, 2010
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Kama mazingira ndiyo yanaleta ushawishi, utaelezeaje mtu mwenye wake 8 na bado anaenda nje? Nina mifano kutoka ndugu wa karibu, ambao ni polygamists kuanzia wake 5-8 lakini bado wanaenda nje. Je, ni mazingira gani unayoyasema?
   
 18. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #18
  Nov 5, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  jamani mlioko moshi jee huyu padri amekamatwa au bado anafichwa?
   
 19. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #19
  Nov 5, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  JK?? anahusika na nini ktk hii story!! eeemmm!:focus:celibacy is always a challenge ktk maisha ya kial siku ya binadamu BUT this shouldn't be taken as an excuse! something is gotta be done! i agree, pontiff aipitie hii doctrine! its' gettin ugly now!!
   
 20. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #20
  Nov 5, 2010
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli hii ni hatari.

  Tuishi kwa matumaini tu sasa
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...