TANZIA Padre Wilbald Mashauri wa Jimbo la Moshi Afariki Dunia

Mwanaukweli

JF-Expert Member
May 18, 2007
4,786
1,710
Mhashamu Askofu Ludovick Minde wa Jimbo la Moshi anasikitika kuwajulisha kwamba usiku wa kuamkia leo Jumapili tarehe 7 Machi 2021, Jimbo Katoliki la Moshi limepata msiba mwingine wa kuondokewa na Padre ambaye alikuwa bado kijana, Padre Wilbald Mashauri.

Taratibu za maziko mtajulishwa!

Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!

Padre Wilbald Mashauri Apumzike kwa amani Amina.

Mashauri.jpg
 
Apumzike kwa amani mja huyu wake mola.

Roho nyingine ambayo ingeweza kuokolewa kwa matumizi ya chanjo inayopatikana bure yapotea.

Ewe mwenye ufunguo bado haikufikirishi tu?
 
Nimesikitika kupewa taarifa ya kifo chake. Alikuwa mlezi wetu vijana pale Moshi wakati nasoma. Alikuwa anatoa semina kadhaa, mafundisho, anakuja maafari, tafrija na elimu ya dini.

Muda wake mwingi aliutumia kwa vijana ingawa sina hakika sana ila pia nakumbuka alikuwa anahusika na accounting za jimbo.

"Kwa kawaida ya binadamu mambo ya dini hayatuvutii, hatutakiwi kuendekeza starehe za dunia bali tutangulize ufalme wa Mungu" nukuu kutoka mojawapo ya matukio yake pale YCS tulipomaliza sherehe tukaweka mziki.

Aliporudi na gari kuchukua kitu alichosahau akashangaa kuona wanaocheza mziki ni wengi kuliko waliokuwa kwenye tukio. Alafu sasa wimbo wenyewe ulikuwa Tetema kipindi unatrend, kisha akatazama ambako tuliweka altare watu wanabambiana. Ila YCS tulikuwaga wahuni hadi CASFETA waligoma kutukodisha vyombo vyao eti tunavipigia nyimbo za kidunia.
 
Back
Top Bottom