PAC imeudangaya umma?

PAC imeudangaya umma?

titomganwa

Senior Member
Joined
Oct 12, 2010
Posts
126
Reaction score
62
PAC imetoa taarifa juu ya fedha za escrow kwa umahili mwingi sana. Wametoa vielelezo vingi. Kwa weledi wao ilikuwa rahisi kutuaminisha. Mimi sikutegemea kabisa kuwa vielelezo vile si vya kweli.

Prof. Muhongo metuletea taarifa kinzani. Hoja za akina zitto na mheshimiwa Filikunjombe zimepanguliwa kwa ustadi na umahiri mkubwa tena kwa kujiamini. Tutaujua ukweli? PAC ina taarifa za kweli kuliko serikali? Je Muhongo anaweza kusema ukweli kuhusu Taarifa za PAC au amesema mambo yale tetezi kwa kujitetea tu?

Tito
 
Hicho kimugao kidogo ambacho umekombeleza kitakutokea puani. Kama unadhani unaokoa jahazi fahamu limeshazama siku nyingi
 
Tito,ungelifanyia kazi hoja za Muhongo kama ukiwa na fikra huru bila kuweka urafiki au upenzi basi ujue,hakuna cha maana zaidi ya kujitetea kwa watawala wetu.

Kuna maswali mengi ambayo kuna watanzania wengi tunayo yamekosa majibu.Ukiliangalia sakata zima halina tofauti na namna ambavyo pesa za EPA zilichotwa kwa kisingizio mwenye nazo hajulikani.Na njia ni ile ile iliyotumika kuzikwapua.

Ukiwa mjanja utaelewa vyema zaidi kwa kujiuliza maswali mengi zaidi.Imenifanya nimdharau hata rais wangu,kuwa ni rais mdhaifu sana na yupo kwa maslahi zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Kama PAC tutaamini tu pale CAG, PCCB na TRA watakapoitwa kuja kukana vielelezo ilivyotumia kamati ya zitto kwamba si vyao
 
Akina Zitto fedha za ufisadi zimewatokea puani
 
Vyanzo vya taarifa za Kamati ya PAC ni CAG, TRA na PCCB.

Ulisema PAC ni waongo, basi CAG, TRA na PCCB nao pia ni waongo.

Kwani kipi kinashindikana hapo? Kama Ofisi Kubwa inaweza hata kutiliwa mashaka ktk utendaji wake wa kazi sembuse hao?
 
Tetty na Mwanahaki, nilidhani ukweli ni rahisi. Kumbe hata vigezo (facts) mara nyingine havisaidii kuujua ukweli. Jambo kubwa kwangu ni moja tu whether zile hela zilikuwa za umma, kwasasa tumefumbwa macho

Nachelea kuchukua upande. Ngoja nijipe raha ya subira ....with time ukweli utadhihirika

Hicho kimugao kidogo ambacho umekombeleza kitakutokea puani. Kama unadhani unaokoa jahazi fahamu limeshazama siku nyingi
 
PAC imetoa taarifa juu ya fedha za escrow kwa umahili mwingi sana. Wametoa vielelezo vingi. Kwa weledi wao ilikuwa rahisi kutuaminisha. Mimi sikutegemea kabisa kuwa vielelezo vile si vya kweli.

Prof. Muhongo metuletea taarifa kinzani. Hoja za akina zitto na mheshimiwa Filikunjombe zimepanguliwa kwa ustadi na umahiri mkubwa tena kwa kujiamini. Tutaujua ukweli? PAC ina taarifa za kweli kuliko serikali? Je Muhongo anaweza kusema ukweli kuhusu Taarifa za PAC au amesema mambo yale tetezi kwa kujitetea tu?

Tito

kwa swala hili ni hoja muohongo kapangua kwa fact but that one was arranged thus way makinda liruhusu PAC itangulie
 
Vyanzo vya taarifa za Kamati ya PAC ni CAG, TRA na PCCB.

Ulisema PAC ni waongo, basi CAG, TRA na PCCB nao pia ni waongo.

mkuu acha utoto bana sote tumesoma ripoti ya CAG haijasema aliyosema zitto mengi katunga yake.
 
PAC haijadanganya UMMA isipokuwa professor MUONGO anadhihirishia umma kwa kujitetea maana siku zote mfa maji hata kama prof haachi kutapatapa
 
PAC wamedanganya umma. ufafanuzi na ukweli tumeupata kutoka serkalini leo.
 
PAC imetoa taarifa juu ya fedha za escrow kwa umahili mwingi sana. Wametoa vielelezo vingi. Kwa weledi wao ilikuwa rahisi kutuaminisha. Mimi sikutegemea kabisa kuwa vielelezo vile si vya kweli.

Prof. Muhongo metuletea taarifa kinzani. Hoja za akina zitto na mheshimiwa Filikunjombe zimepanguliwa kwa ustadi na umahiri mkubwa tena kwa kujiamini. Tutaujua ukweli? PAC ina taarifa za kweli kuliko serikali? Je Muhongo anaweza kusema ukweli kuhusu Taarifa za PAC au amesema mambo yale tetezi kwa kujitetea tu?

Tito

Soma taarifa zote harafu anzisha uzi ambao unakuwa na utafiti kamili si hiki kituko.
 
Tusubiri wachangiaji baadaye. Acheni kutapatapa. Mhongo ni Tapeli tu huyo. Nina shaka na Spika.
 
Yes, umesema kweli. Vyanzo vya taarifa ya PAC ni CAG, TRA na PCCB na kama ni uwongo, hawa ndio waongo.

VYANZO VYA UKWELI WA MHONGO NI VIPI ILI TUWATAMBUE HAO WAKWELI WALIOMPA MHONGO TAARIFA HIZI SAHIHI?

Kweli ujinga wa Watanzania ndilo kaburi lao!.

Back
Top Bottom