PAC imeudangaya umma?

PAC imeudangaya umma?

PAC imetoa taarifa juu ya fedha za escrow kwa umahili mwingi sana. Wametoa vielelezo vingi. Kwa weledi wao ilikuwa rahisi kutuaminisha. Mimi sikutegemea kabisa kuwa vielelezo vile si vya kweli.

Prof. Muhongo metuletea taarifa kinzani. Hoja za akina zitto na mheshimiwa Filikunjombe zimepanguliwa kwa ustadi na umahiri mkubwa tena kwa kujiamini. Tutaujua ukweli? PAC ina taarifa za kweli kuliko serikali? Je Muhongo anaweza kusema ukweli kuhusu Taarifa za PAC au amesema mambo yale tetezi kwa kujitetea tu?

Tito

Muongo yule prof uchwara,mbona hajagusa waliopata mgao?tusidanganywe kirahisi ivo!
 
Inategemea ulivyoelewa Ripoti ya CAG na TAKUKURU na utetezi wa WNM.Nimeangalia hoja zake na namna alivyozijenga.Zaidi zimeelemea kwenye tuhuma iliyojengwa kwenye tuhuma.

Siwezi kukulazimisha kuelewa namna nilivyoelewa.Siwezi kujua taaluma yako sababu taaluma yangu imenifanya nijiulize maswali mengi zaidi na zaidi.
mkuu Tetty iwapo uelewa wa hizi taarifa unaendana na taaluma ya mtu, basi inawezekana kabisa wengi watakuwa wameachwa na wanasubiri matokeo
 
Last edited by a moderator:
Muhongo kama lilivyo jina lake kadanganya umma leo bila chenge. Eti pesa za escrow sio za umma, kwani zilitoka wapi? Hii ni aibu kubwa sana kwa profesa mzima kusema uongo mchana kweupe!
 
Hoja ni kuwa kama PAC ilidanganya kwa nini muhongo & co walihangaika sana mahakamani na usiku kucha kuitafuta ripoti mpaka jamaa (Zitto&co) hawakulala wakakesha kuilinda?

Kumbuka kaka pesa hizi zimekuwa ndiyo kichochoro cha kuficha ukweli.Hongo zimetumika sana,na hata wabunge wenyewe kunabaadhi yao wamepata,hivyo kwa sasa kuna ugomvi kati ya wale waliopata na ambao hawakupata?

Na kama ilikuwa uwongo kwa nini kutumia nguvu nyingi ya kuwachafua Zitto & Coy?

Tatizo serikali yetu inafikiria kuwa wataendelea kutudanganya mpaka kiama.Wamesahau kuna kizazi kipya kisichotaka ubabaishaji,kizazi cha vijana ambao wapo bungeni,wamepigika,hawa wanaoangaliwa na vijana wenzao wanaopanga hoja zao.

Kizazi cha kidigitally ni hatari kinafanya utafiti wa kina,kina majibu kabla hujaanza kuwadanganya,kinahoji,kinataka kujau kwanini,kinahitaji FACTS na siyo SIASA ,kinachohoji kwanini RAIS asiwajibike kwa UZEMBE,hakina uwoga kuwa kitapoteza kitu,hiki ndicho kizazi tulichonacho.

Watawala wetu wamejisahau.
 
Unaonaje ukirudi kwenye hoja ya msingi ndugu. Nakushauri ujibu hoja kwa hoja siyo matusi. Hii haina tofauti na wapiga klele bungeni.

Hayo umwambie Muhongo na wote mnaoishikwa makalio na ---------.. Hoja ni kwamba wamekwepa kodi, wamtakatisha fedha, wametumia ofisi vibaya wamehujumu uchumi.. Hayo ndo makosa yao.. Sasa kama huelewi kwa kuwa unashkwashikwa na Singasinga endelea.. Watz ndo tumeamka hivyo
 
mkuu Tetty iwapo uelewa wa hizi taarifa unaendana na taaluma ya mtu, basi inawezekana kabisa wengi watakuwa wameachwa na wanasubiri matokeo

Umenijibu vyema sana.Hint tu,Mkaguzi wa mahesabu na Muhasibu watu hawa wataelewa tofauti na injinia na watu wengine wenye taaluma nyingine.

Wenye taaluma za Ukaguzi wa mahesabu na Muhasibu wanaelewa nini maana ya CAG na ripoti zake,hasa pale anapofanya Independent Investigation au auditing,watu hawa wanajua vigezo vitumikavyo mpaka kupata FACTS.Hawamuangalii mtu wala kusikiliza unasema nini.Wanatafuta FACTS za kubainisha kama kuna wizi au la.Na ndiyo maana imeelezwa wamepeleka information TAKUKURU ifanyiwe kazi,sababu siyo field yao kutafiti kama kuna RUSHWA au la.Wameona kuna FACTS za RUSHWA lakini mwenye taaluma hiyo yupo,wamempelekea FACTS azifanyie kazi.

Wametafuta FACTS kama kuna wizi wameziainisha vyema na kuzitoa kwa lugha nyepesi kwa wale waliowatuma wakiamini kuwa kuna wasiyo wahasibu au auditors na lugha yao ya kitaaluma ingekuwa ngumu kueleweka.

Wahasibu na auditors hakika watajua nini kichambuliwe vipi,na wataoanisha facts zilizotolewa ili wapate uhakika.Hivyo basi kwa uhakika kabisa ripoti ya CAG ndiyo yenye UKWELI USIOKUWA NA PINGAMIZI,wameweka FACTS zilizofanyiwa kazi kwa UTAALAMU wa hali ya juu bila kuweka visasi,uzushi,uwongo nk nk.

Nadhani utakuwa umenielewa japo kidogo.
 
Nikweli hata mimi katika hili nahisi kulogwa. Ila mlozi wangu ni kati ya PAC au watendaji wakubwa wa serikali. Tutajua tu, tuvute subira
Kapime vizuri ubongo wako si bure nahisi umelogwaaaaaaaaaaa
 
PAC imetoa taarifa juu ya fedha za escrow kwa umahili mwingi sana. Wametoa vielelezo vingi. Kwa weledi wao ilikuwa rahisi kutuaminisha. Mimi sikutegemea kabisa kuwa vielelezo vile si vya kweli.

Prof. Muhongo metuletea taarifa kinzani. Hoja za akina zitto na mheshimiwa Filikunjombe zimepanguliwa kwa ustadi na umahiri mkubwa tena kwa kujiamini. Tutaujua ukweli? PAC ina taarifa za kweli kuliko serikali? Je Muhongo anaweza kusema ukweli kuhusu Taarifa za PAC au amesema mambo yale tetezi kwa kujitetea tu?

Tito
Mijizi hata upati tabu kuifahamu.
 
Muhongo hamna kitu ni dalali tu.hata mmtetee vpi nyie vimada wake hachomoki pale...
 
PAC ni Mengi tu huyo hamna issue.

Muhongo kafanya mambo angalia umeme vijijini sasa. acheni ushabiki wa matajiri uku nyie munakufa njaa
 
Hayo umwambie Muhongo na wote mnaoishikwa makalio na ---------.. Hoja ni kwamba wamekwepa kodi, wamtakatisha fedha, wametumia ofisi vibaya wamehujumu uchumi.. Hayo ndo makosa yao.. Sasa kama huelewi kwa kuwa unashkwashikwa na Singasinga endelea.. Watz ndo tumeamka hivyo
Una matatizo makubwa sana ndg. Na kama kuamka kwenyewe ndio huku afadhali ungeendelea kulala tu.
 
PAC imetoa taarifa juu ya fedha za escrow kwa umahili mwingi sana. Wametoa vielelezo vingi. Kwa weledi wao ilikuwa rahisi kutuaminisha. Mimi sikutegemea kabisa kuwa vielelezo vile si vya kweli.

Prof. Muhongo metuletea taarifa kinzani. Hoja za akina zitto na mheshimiwa Filikunjombe zimepanguliwa kwa ustadi na umahiri mkubwa tena kwa kujiamini. Tutaujua ukweli? PAC ina taarifa za kweli kuliko serikali? Je Muhongo anaweza kusema ukweli kuhusu Taarifa za PAC au amesema mambo yale tetezi kwa kujitetea tu?

Tito
Naomba nikuulize ndugu yangu toka lini mwizi au mhalifu akakubali moja kwa moja kuwa ameiba bila mbinyo kupita? Kwa uzoefu hii nchi hakuna uwajibikaji hata siku moja. Na mfumo uliopo wa utawala ni wakihalifu kupindukia. Nachotaka kusema ni kuwa huo utetezi ni intentionally prepared kupotosha ukweli kwa kuwa kila kitu wanacho na mwingine wanaweza kumyima kwa maslahi yao anapohitaji taarifa.
 
Umenijibu vyema sana.Hint tu,Mkaguzi wa mahesabu na Muhasibu watu hawa wataelewa tofauti na injinia na watu wengine wenye taaluma nyingine.

Wenye taaluma za Ukaguzi wa mahesabu na Muhasibu wanaelewa nini maana ya CAG na ripoti zake,hasa pale anapofanya Independent Investigation au auditing,watu hawa wanajua vigezo vitumikavyo mpaka kupata FACTS.Hawamuangalii mtu wala kusikiliza unasema nini.Wanatafuta FACTS za kubainisha kama kuna wizi au la.Na ndiyo maana imeelezwa wamepeleka information TAKUKURU ifanyiwe kazi,sababu siyo field yao kutafiti kama kuna RUSHWA au la.Wameona kuna FACTS za RUSHWA lakini mwenye taaluma hiyo yupo,wamempelekea FACTS azifanyie kazi.

Wametafuta FACTS kama kuna wizi wameziainisha vyema na kuzitoa kwa lugha nyepesi kwa wale waliowatuma wakiamini kuwa kuna wasiyo wahasibu au auditors na lugha yao ya kitaaluma ingekuwa ngumu kueleweka.

Wahasibu na auditors hakika watajua nini kichambuliwe vipi,na wataoanisha facts zilizotolewa ili wapate uhakika.Hivyo basi kwa uhakika kabisa ripoti ya CAG ndiyo yenye UKWELI USIOKUWA NA PINGAMIZI,wameweka FACTS zilizofanyiwa kazi kwa UTAALAMU wa hali ya juu bila kuweka visasi,uzushi,uwongo nk nk.

Nadhani utakuwa umenielewa japo kidogo.
nimekupata, sasa turudi nyuma kwenye swali langu la awali, je ni maswali gani bado hayajajibiwa?
 
Hee kumbe Lizaboni na GSU ni CCM Maslahi sio CCM Imani kama Kingwangwala na Fulikunjombe Deo etc..
 
Back
Top Bottom