hili swala la pesa za umma au sio za umma ni kuwaondoa watu kwenye mada! hapa issue ni kuwa watumishi wa umma wamelipwa mabilioni ya pesa , Chenge 1.6, Mhongo 1.6 na Anna Tibaijuka 1.6 , je wamefanya biashara gani au wametoa consultancy gani kuwa na uhalali wa kupewa hayo mabilioni? na huo msururu wa watu wengine waliogawana pesa? kama zingekuwa si za umma na ni za mtu binafsi au mfanyabiashara kweli angeweza kugawa pesa yake bure? kuna mfanyabaishara gani anagawa pesa bongo niende na familia yangu kuchukua? zile pesa za Tegeta Escrow hazikuwa na mwenyewe (ni za umma) ndo maana watu waligawana na kubeba na viroba! pesa za umma bongo ni shamba la bibi!
1. Mbona umejichanganya mwenyewe? Umeanza kwamba "fedha ni za umma au siyo za umma ni kuwaondoa watu kwenye mada". Lakini hitimisho lako limekuwa "hazikuwa na mwenyewe (ni za umma)!
2. Mjadala wako umeuchanganya na kukosa kueleweka hasa ulichotaka kuongea ni kitu gani! Umetumia hisia zaidi ya kujenga hoja ili utushawishi tukuamini.
3. Hizi hisia siyo mpya na hazibadilishi ukweli kwamba fedha zilizokuwemo kwenye Tegeta Escrow Account zilikuwa siyo za UMMA.
4. Ukizungumzia kugawa fedha, bila shaka unamzungumzia Mkurugenzi wa VIP Engineering and Marketing Ltd., Fr. James Rugemalira, mtu aliyeuza hisa zake kwa njia halali kuliko maelezo, kwani mkataba wake uliridhiwa na Mahakama Kuu katika shauri la wazi.
4.1 Pamoja na kuuza hisa zake, akaweka masharti yaliyoridhiwa na mnunuzi ili kuhakikisha maslahi ya umma yanazingatiwa, ikiwa ni pamoja na (a) mmiliki mpya wa IPTL kupanua uzalishaji kutoka 100MW hadi 500MW ili kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa Umeme kwenye gridi ya Taifa. (b) kubadilisha mitambo kutoka kutumia mafuta mazito kwenda kwenye matumizi ya gesi asilia (rasilimali ambayo sasa tunayo hapa hapa nchini). Hatua ambayo itapunguza/ kukata kwa kiasi kikubwa gharama za uzalishaji na matumizi ya pesa nyingi za kigeni kuagiza mafuta mazito. (c) kupunguza/ kushusha gharama ya kuuza Umeme hadi kati ya senti za Dola ya Kimarekani kati ya Senti 6 mpaka Senti 8, kiwango ambacho kitaipatia TANESCO unafuu mkubwa na hata mpaka mtumiaji wa mwisho.
4.2 VIP Engineering and Marketing Ltd., ya Fr. James Rugemalira, ikaenda mbele ikalipa kodi ya (Capital Gains Tax) kiasi cha Sh. 38Bilioni TRA.
5. Kwa mtu yeyote MAKINI lazima aishangae sana Kamati ya Zito yaani PAC kama hayo mazuri yote haikuyaona! Na mshangao zaidi ni pale Zito na PAC walipohoji kwa nini bei ya umeme ishushwe na Mahakama Kuu! Huu wote ulikuwa ni upotoshaji mkubwa, wakijua kabisa hayo yalikuwa ni masharti ya VIP/Rugemalira kuuza hisa zake. Huu ndiyo ukweli mwingine unaodhihirisha Zito na genge lake hawakuwa wanazingatia maslahi ya taifa na UMMA kwa ujumla, bali maslahi ya waliokuwa wamewatuma.
6. Nipende tu kutoa RAI kwa Watanzania wenzangu kwamba tujaribu kuwa na subira kidogo. Tujizuie kuwa watu wa mkumbo. Tujadili mambo kwa nia ya kuangalia picha pana, tuwe "objective na siyo subjective". Hivi, kweli kwa hayo yaliyoekezwa hapo juu ambao ni ukweli mtupu ambao unaweza kwenda Mahakama Kuu ukaomba nakala ya maamuzi na TRA wakakupatia, na mengine yamo kwenye Ripoti ya CAG hatuweze kuona kwamba kila mmoja amenufaika au atanufaika kutokana na uuzaji wa share za VIP kwa njia moja au nyingine?
7. Kwa kuwa kila mmoja amenufaika au atanufaika kutokana na VIP/ Fr. James Rugemalira kuuza shares zake, kwa nini tunajiingiza kuangalia nani kanufaika zaidi? Je, tunafahamiana naye, kwamba tulikuwa tumewahi kumpelekea mapendekezo ya miradi tunayoifanya yenye uhitaji wa fedha kama alivyokuwa amefanya Mh. Prof. Anna Tibaijuka kwa mfano? Miradi ambayo bado inakwenda kusaidia watu wengi zaidi, kwa mfano elimu. Je, kuna ubishi kwamba msaada mkubwa kuliko unaoweza kumpatia binadamu ni elimu? Kama kuna atakayekataa basi huyo ni mtu wa aina yake.
8. Ninaamini tukijifikirisha kidogo baada ya kuyafahamu haya itaweza kutusaidia zaidi kumuangalia VIP/Fr. James Rugemalila kama Mtanzania mzalendo mwenye kuzingatia maslahi ya UMMA kuliko ambavyo imewahi kutokea. Pengine ndiyo maana wengi wetu bado tunamshangaa na hatujamuelewa! Yametokea kweli, tusiendelee kushangaa, tumuamini, tumuunge mkono, tusonge mbele maisha yaendelee. Fr. James Rugemalira ameweza kufanya watanzania wengine pia wawekezaji IGENI MFANO WAKE.