PAC ilivyowajaza hasira wananchi

PAC ilivyowajaza hasira wananchi

Watetezi wote wa hizi fedha wamejiunga humu kwa ajili hii tu, karibuni JF maana hata hodi hamjapiga. Ila msitumike sana...
 
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliwajaza hasira wananchi pale ilipotoa taarifa potofu bungeni kuwa fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya Escrow ya Tegeta zilikuwa zimechotwa. Wananchi walikuwa na haki ya kujawa na hasira kwa sababu walilishwa taarifa iliyoonyesha kuwa fedha zao (za umma) zimechotwa na wajanja wachache. Hata baada ya Mkuu wa Nchi kubainisha kuwa fedha hizo hazikuwa za umma, inashangaza kuona wanasiasa wengine, akiwemo mwenyekiti wa PAC, bado wanaendelea kuwachochea wananchi kwa kurudia kuwalisha taarifa potofu.

Ulelema Ulelema unafikili kwa kutumia ushuzi kwa nini unataka kutuaminisha huo upuuzi wako kama huna lolote la kuandika humu nibora ukamsaidia mkeo kumenya vitungu au kumbadilisha mtoto permpus!yaani umebitia hasila sana nyambafuu wewe!!
 
Ninapenda sana mchezo wa Kung Fu, maana mtu ukiwa tofauti nae (kimkanda) huruhusiwi kupigana nae. Suala la ESCROW lahitaji weledi ili kulitolea ufafanuzi maridhawa. Kusema ZZK kapotosha kisa Rais katoa ufafanuzi ni kichekesho. Dunia ya leo watu huhitaji kulinganisha mantiki. Kwani kila mtu kwa mfano akipewa asome "BOQ" ataweza kuielewa na kuitolea ufafanuzi?
 
fedha za Escrow hazikua za uma, hata hivyo kuna kodi ambayo haikulipwa"-JK.
Sasa sijui hiyo kodi ni hela ya escrow au muhongo hapo ndio sielewi

mkuu, mijizi utaiweza kwa kujichanganya?

hukumsikia JK alivyokuwa anajiumauma wakati alipokuwa anataka kufafanua bila mafanikio kauli yake hapo juu? aliishia tu kutamka.. "haya mambo yanaleta mkanganyiko kweli kweli...".
sasa hapo kuna mkanganyiko gani wakati kitu ni black n white kabisa??

nchi hii imejaa ujanjaujanja tu... hadi kwenye corridors of power!!
 
Last edited by a moderator:
Haya ni mwazo na hisia zako. Sababu za AG kujiudhuru
ziliwekwa wazi. Ulizozitaja humu ndiyo kwanza tunazisikia. Wewe pia ni mzushi ndiyo maana unamuamini Zito moja kwa moja.

Kila unapojibu unaanzisha mjadala mpya. Niwezaje kumuamini ZZK? Ninaamini yaliyofanywa na CAG, PAC na Bunge la Jamhuri ya Muungano. Kama una ugomvi na individuals usiufanye kuwa ni wa taasisi. Nahisi unadhani watanzania hawawezi kutofautisha simba na mbuzi aiyevaa ngozi ya simba.
 
Ninapenda sana mchezo wa Kung Fu, maana mtu ukiwa tofauti nae (kimkanda) huruhusiwi kupigana nae. Suala la ESCROW lahitaji weledi ili kulitolea ufafanuzi maridhawa. Kusema ZZK kapotosha kisa Rais katoa ufafanuzi ni kichekesho. Dunia ya leo watu huhitaji kulinganisha mantiki. Kwani kila mtu kwa mfano akipewa asome "BOQ" ataweza kuielewa na kuitolea ufafanuzi?

Jenga hoja kuhusu Ripoti ya CAG kwa kufanya rejea na kuipa PAC uhalali. Hiyo mifano ya Kung fu na wengine kuandika maneno machafu na kukasirishwa na hoja za wengine, hayatawasaidia kabisaa.
 
Haya ni mwazo na hisia zako. Sababu za AG kujiudhuru
ziliwekwa wazi. Ulizozitaja humu ndiyo kwanza tunazisikia. Wewe pia ni mzushi ndiyo maana unamuamini Zito moja kwa moja.

Ni kweli naandika kwa mawazo yangu na hisia zangu kwa yale ninayoyajua. Sitegemei kuandika kwa kutumia mawazo ya na hisisa za mtu mwingine.
 
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliwajaza hasira wananchi pale ilipotoa taarifa potofu bungeni kuwa fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya Escrow ya Tegeta zilikuwa zimechotwa. Wananchi walikuwa na haki ya kujawa na hasira kwa sababu walilishwa taarifa iliyoonyesha kuwa fedha zao (za umma) zimechotwa na wajanja wachache. Hata baada ya Mkuu wa Nchi kubainisha kuwa fedha hizo hazikuwa za umma, inashangaza kuona wanasiasa wengine, akiwemo mwenyekiti wa PAC, bado wanaendelea kuwachochea wananchi kwa kurudia kuwalisha taarifa potofu.
Vilaza wahedi!
Kwa hiyo iliwachukua muda gani na nyie kuzinduka?
Nyiwe wezi wa kuku hadi mali ya umma!
 
Kila unapojibu unaanzisha mjadala mpya. Niwezaje kumuamini ZZK? Ninaamini yaliyofanywa na CAG, PAC na Bunge la Jamhuri ya Muungano. Kama una ugomvi na individuals usiufanye kuwa ni wa taasisi. Nahisi unadhani watanzania hawawezi kutofautisha simba na mbuzi aiyevaa ngozi ya simba.
Pole sana kiongozi, msingi wa hoja za PAC haukujengwa juu ya ripoti ya CAG pekee, kuna ripoti ya TAKUKURU pia. Ndio maana nasema Kung Fu ni mchezo mzuri.
 
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliwajaza hasira wananchi pale ilipotoa taarifa potofu bungeni kuwa fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya Escrow ya Tegeta zilikuwa zimechotwa. Wananchi walikuwa na haki ya kujawa na hasira kwa sababu walilishwa taarifa iliyoonyesha kuwa fedha zao (za umma) zimechotwa na wajanja wachache. Hata baada ya Mkuu wa Nchi kubainisha kuwa fedha hizo hazikuwa za umma, inashangaza kuona wanasiasa wengine, akiwemo mwenyekiti wa PAC, bado wanaendelea kuwachochea wananchi kwa kurudia kuwalisha taarifa potofu.

Mnadhani wananchi watatulia? subirini kiama uchaguzi mkuu mtatafutana
 
Toeni Nuksi zenu hapa JF kama si za UMMA Werema anakubalije kujiuzuru kwa ushauri wake? Na kama si za Umma Benki Kuu zinatafuta nini badala kuwekwa kwenye account ya IPTL? na kama hakuna fedha za Umma kwa nini wasisitizwa kulipa kodi?
Kwa Taairfa palikuwepo Pesa za Umma, Pesa IPTL na Fedha za Serikali kupitia tozo TRA.
 
1. Unaweza kuthibitisha tuhuma zako?

2. Hii inakumbusha jana kwenye BBC Dira ya Dunia, nilisikia mwanafunzi mmoja nchini Kenya, amehukumiwa kifungu jela kwa kumdhalilisha Rais Uhuru Kenyatta.

3. Inaweza kuwa kwa kutokujua ukatenda kosa ambalo unaweza kulijutia maisha yako yote. Tusitumie vibaya Uhuru wa habari. Tuvitumie kwa kuheshimu uhuru na haki za watu wengine. Rais, asikashifiwe hovyo hovyo. Kama wewe unajiamini kwa tuhuma zako, itisha mkutano mtaani kwako uzitoe zote bila kificho na siyo kujificha hapa JF.
Wacheni wizi , ufisadi na rushwa.
Subiri hao watawala watoke madarakani uone kama ushahidi utakosekana.
Kenyata mwenyewe ni walewale na ana kesi ya mahakama ya kimataifa , hata huyo kijana kahukumiwa huko Kenya kwasababu mahakama zipo corrupted vile vile.
Kwahiyo kakojoe ulale.
 
Ni wazi kwamba anachokifanya Zitto sasa ni uchochezi. Baada ya Rais kutamka wazi kwamba pesa zile kwenye Akaunti ya Escrow sio za umma, kwa nini yeye aendelee kuwatia hasira wananchi, ambao wengi wao hawaelewi undani wa suala hili? Huu ni uchochezi, tena wa hali ya juu.

jaribu japo kumuiga mbayuwayu. kwanini sasa maswi kasimamishwa kazi?? kwann ana tibaijuka kapigwa chini. kwanini muhongo yuko under investigation. wewe ni zerro la kutupwa
 
fedha za Escrow hazikua za uma, hata hivyo kuna kodi ambayo haikulipwa"-JK.
Sasa sijui hiyo kodi ni hela ya escrow au muhongo hapo ndio sielewi
Sheria ya kodi ya ongozeko la thamani VAT iko wazi kwa kuwafanya wafanyabiashara wakubwa kuwa mawakala wa kukusanya kodi kwa niaba ya TRA. IPTL alipeke invoice zake Tanesco zikiwa na VAT ndani yake na Tanesco alilipa invoice zile pamoja na VAT hivyo hii ilipeleka jukumu la kulipa VAT TRA kwa IPTL na CAG kwenye report yake ameweka wazi ni nani aliyekuwa na jukumu la kulipa kodi ile TRA. Kwangu mimi binafsi naona hapa PAC walipotosha umma sijui kwa lengo lipi na kwa faida ya nani.
 
Back
Top Bottom