Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliwajaza hasira wananchi pale ilipotoa taarifa potofu bungeni kuwa fedha zilizokuwa kwenye Akaunti ya Escrow ya Tegeta zilikuwa zimechotwa. Wananchi walikuwa na haki ya kujawa na hasira kwa sababu walilishwa taarifa iliyoonyesha kuwa fedha zao (za umma) zimechotwa na wajanja wachache. Hata baada ya Mkuu wa Nchi kubainisha kuwa fedha hizo hazikuwa za umma, inashangaza kuona wanasiasa wengine, akiwemo mwenyekiti wa PAC, bado wanaendelea kuwachochea wananchi kwa kurudia kuwalisha taarifa potofu.