P.e.n.d.o...!

Menyous

Senior Member
Joined
Mar 17, 2009
Posts
136
Reaction score
43
Ukijua pendo ukaishi na pendo, ni vigumu sana kuja ishi bila pendo. Ukiweza...usivue pendo, maana kuishi bila pendo ni kazi kama mtu mzima kuishi bila kipato. Maisha bila ya pendo baada ya kujua pendo, ni utumwa mkubwa moyoni na nafsini, haijalishi una nini vingine. Ukilijua pendo na kuishi na pendo maisha yako hupata maana mpya na bora zaidi. Tunza pendo ulipatapo, maisha bila ya pendo baada ya pendo ni jela ya nafsi na moyo.
 

Naomba huu ujumbe mzuri uandkwe kwa kingereza pia
 

Ngoja niongezee, ...
Ukijilijua pendo, kisha ukapata pendo na kutoa pendo kwa yule anayejua maana ya pendo hapo ndiyo maisha huwa yana pendo. Lakini ukitoa pendo kwa asiyejua pendo wala kukupa pendo, basi wewe ni mtumwa wa pendo lako mwenyewe. Kwa kifupi, namaanisha usipende wala kupendwa bali pendaneni!
 

Haya ni malenga, mashairi, utunzi au taarabu?
 

Hiyo haswaa ndio maana ya kuishi na Pendo!

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums
 

tumeingiliwa na mwasiti
nn?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…