Future Bishop
Member
- Dec 4, 2009
- 75
- 15
Kama kweli umeoa mke wa kukaa naye na siyo kwamba mna mkataba wa muda ni muhimu sana yeye kujua vyanzo vya mapato yako. Kumbukeni uwazi na mwasiliano mazuri ndani ya nyumba ni mojawapo ya mambo muhimu yanayofanya nyumba kusimama.
Ninamshukuru Mungu katika hili ametuponya mimi na mke wangu. Nina faili nyumbani ambalo lina nakala zote za mikataba yangu ya ajira toka nilipoanza kuajiriwa na humo ndani ndimo tunaweka salary slips. Kila mmoja wetu ana acess na faili hilo kwa hiyo mimi najua mshahara wake na yeye anajua mshahara wangu.
Kwa wale wenye kuhofu kuwa akijua mshahara wako atazipangia bajeti mpaka ziishe nadhani siyo , kama kweli mnakaa na kukubaliana matumizi yaweje. Ni ninyi wawili mnaopaswa kukaa na kukubaliana bajeti ya mwaka, mwezi, wiki na ikiwezekana hata siku iweje.
Wanaume naomba msiwafiche wake zenu mishahara yenu kwa hofu kuwa watamaliza fedha, amua kumshirikisha na uone ana hekima ya namna gani katika kushauri suala zima la bajeti na matumizi. Ukiona hekima yake ni ndogo unachoweza kufanya ni kusimamia wewe bajeti nzima na kumuacha yeye ni mtekelezaji lakini akiwa anajua unapata kiasi gani. Naamini hii itasaidia kuifanya ndoa yenu isimame vizuri.