Oyaa!! - Usionyeshe Salary Slip Yako!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,724
Kuna jamaangu alipata kusema kwamba "Ndugu yangu ukimwonyesha mkeo `Salary Slip` umekwisha!, maana atazua matumizi yasiyo ya lazima, hadi ahakikishe fedha zote zimeisha"!

Lakini pia, kwa uchunguzi wangu binafsi kumekuwa na tabia ya watu wengi kuficha kwa wake zao (au waume zao), figures halisi za mishahara yao.

Ukiacha Mishahara, pia kuna marupurupu lukuki ambayo huenda mume au mke anaweza akawa anayapata, lakini yote haya hayasemwi kwa uwazi kwa mwenza.

Kuna vitu kama overtime, tips, bakshishi, commission za manunuzi, allowances kadha na safari packages ambazo wanaume wengi hawaziweki wazi kwa wake zao pindi wazipatapo.

Je kuna ukweli gani kuhusu jambo hili?

Ni halali kuweka hadharani mafao haya kwa mwenza, au ni salary slip tu inayotakiwa kuonyeshwa?
 
nadhani hayo yalikuwa mawazo ya karne ya giza, kwa nini usimshirikishe mke wako katika kuweka sawa bajeti yenu. Unamficha ili ukafanyie nini hizofedha, wakati chake ni chako na chako ni chake. Jee kama naye (Mke) ana shughuli inayomwingizia fedha afiche?.
 
Whoever Knows Everything Is Expert In Nothing!
 
nadhani hayo yalikuwa mawazo ya karne ya giza, kwa nini usimshirikishe mke wako katika kuweka sawa bajeti yenu. Unamficha ili ukafanyie nini hizofedha, wakati chake ni chako na chako ni chake. Jee kama naye (Mke) ana shughuli inayomwingizia fedha afiche?.

Je wewe unaonyesha za kwako?
 
Kama kweli unampenda mwenzi wako kwa dhati, na hukulazimishwa na mtu yeyote kumpenda; BASI una kila sababu ya kumwonyesha salary-slip yako na marupurupu mengine pia.......

UTAKE USITAKE, HABARI NDO HIYOOOO!!!!!!!
 
Are you people really serious, au mnafurahisha wanaJF?

Hivi si nyie ambao mnageukia ukutani hata mnapoacha hela ya mboga?

Lets speak our hearts jameni!
 
...haya, ukiandika wosia je, ...utamuonyesha jinsi ulivyoigawanya mali?
 
Binafsi nadhani hakuna ubaya wowote kwa mwenza kufahamu kipato chako halisi, cha muhimu yawepo makubaliano anuwai ya jinsi gani kipato husika kitumike..
 
Sasa si ni bora usio au usiolewe kabisa kuliko kuficha ficha vitu wakati uko mume au mke wa mtu.
 
Kama kweli unampenda mwenzi wako kwa dhati, na hukulazimishwa na mtu yeyote kumpenda; BASI una kila sababu ya kumwonyesha salary-slip yako na marupurupu mengine pia.......

UTAKE USITAKE, HABARI NDO HIYOOOO!!!!!!!

Ili iweje?......ok isije ikawa ni kama sheria vile kwamba lazima uonyeshe.....ili? au hutakiwi kuonyesha kwa nini?

My point ni kuwa si lazima eti kuonyesha na si lazima au halali kufichana slips na mapene etc......if necessary mwenza anaweza ona kipato cha mwenzi wake and vice versa but isiwe kulazimishana vile!
 
Sasa si ni bora usio au usiolewe kabisa kuliko kuficha ficha vitu wakati uko mume au mke wa mtu.

Komredi nilionyesha kwa sholi mmoja akawa ananikamua balaa kulitachi nywele alikuwa ananilamba 70,000/= kwa wiki bado matumizi mengine. Bora asijue na usijue anacho pata.
 
hivi shori wako akijua salary yako tatizo liko wapi? mie shori akiwa ananikamua mijihela ndio nasikia raha......
 
Are you people really serious, au mnafurahisha wanaJF?

Hivi si nyie ambao mnageukia ukutani hata mnapoacha hela ya mboga?

Lets speak our hearts jameni!

haaa na wewe umeona eeh, naona hao hapo juu hawajaingia ndani bado....
 
Salary ya mtu ni confidential information. Can your spouse treat it as such? Can your spouse use the information in the best interest of your relationship? If the answers to both of these questions is yes, then you dont have any reason to hide your slips. I never hide mine;).
 
Last edited:
Mimi nadhani si vibaya kuonyesha unapata kiasi gani kama ndio utaratibu wenu mliojiwekea lakini kuonyesha haimaanishi kutumia. Unawezaonyesha unapata mil 4 kila mwisho wa mwezi na wife anapata 3.5 mfano then kuna kiwango mnakubaliana kiende wapi, kingine wapi then ni muhimu kubakishiana kidogo kwa ajili ye personal treats jamani sio kila cent inaingia kwenye familia.

kwangu mimi nilijiwekea utaratibu (ingawaje haujamaterialize) kuwa nitawasilisha zote za mshahara na tutapanga zote zote zake na zangu. ISIPOKUWA pesa nitakayo/atakayoipata kama allowances, workshop sitting allowance hizo ni za kwangu/kwake for my/his self treat- kutoka out na friends, kutoka na familia na hata vijizawadi zawadi but nijua anapata ngapi (mwisho wa mwezi) nami ajue napata ngapi.
 
Are you people really serious, au mnafurahisha wanaJF?

Hivi si nyie ambao mnageukia ukutani hata mnapoacha hela ya mboga?

Lets speak our hearts jameni!

...watu kama hao siku ya siku 'yanapowakuta', wanabakia midomo wazi mtalaka wake anapoibua kila kitu ustawi wa jamii!

Dont trust anyone jamani, hata mdomo wako unaweza kukuponza usingizini, ...umelala fo fo fo domo 'linabwabwaja!' siri zote.
 
watu walioana siku zote ninavyojua mimi hakuna siri baina yenu. Kama mwili mmoja kwa nini umfiche mwenzio salary slip yako? Wanaume wanaoficha salary slip zao kwa wake zao ni wale bahili.
 
Wanaume wanaoficha salary slip zao kwa wake zao ni wale bahili.

Ubahili mhimu kwani lazima ujue? Na ukisha jua itakusaidia nini?
Watu wanafilisika hivi hivi kwa kuweka mambo yao wazi.
 
Back
Top Bottom