Our founding fathers spilled rivers of sweat to build this country but these Politicians …!

Entrepreneur

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
1,087
620
Ndugu zangu,
Wakati wa kampeni za uchaguzi ni wakati muhimu sana katika jamii yoyote. Ni wakati muhimu kwa sababu jamii husika hujiandaa kuchagua viongozi wao wa kuwaweka mstari wa mbele (frontline) katika kukabiliana na changamoto za kimaisha iwe kijamii, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni. Ni wakati muhimu kwa wananchi kusikiliza sera za wagombea na kupembua mchele katikati ya pumba, ni wakati wa kutafuta dhahabu katikati vipande vya chupa. Je haya ndio yanayoendelea huko ARUMERU?

Tunashuhudia tambo za kila aina! matusi ya kila aina! (hata mbele za watoto) badala ya Sera, Sera zitakazomkomboa mwana wa Arumeru Mashariki. Ndugu zangu, Taifa hili limejengwa katika misingi ya kuheshimu UTU WA MWANADAMU, (Dignity of Man). Je ni nani kati ya hawa wanasiasa waliopo huko ARUMERU anaweza akasimama na kusema anafanya siasa zinazoheshimu UTU? Kwa siasa hizi tutafika wapi?

Inasemekana kuwa SIASA ni UCHUMI, na uchumi wetu ndio huo tena unazidi kuporomoka, hivyo basi ni vyema hawa wanasiasa walio mstari wa mbele watupatie HOJA zao na si VIOJA vyao, watupe SERA zao na si SIRI zao, ili wananchi wajue dhahabu ni ipi na chupa ni zipi, wajue Mchele ni Upi na makapi ni yapi. Sasa kama leo wanafanya SIASA za namna hii (visasi,kuchafuana,chuki,udanganyifu,matusi, ..) tena kwenye ngazi ya Jimbo tu, je kesho watafanya siasa za namna gani?

Ewe mwanaJF, mpenda mabadiliko, tena usiyevutiwa na mtindo huu wa siasa za kupakana matope
ungana nami kuwataka wanasiasa wetu wafanye siasa safi.

Ewe mwananchi unajua nguvu ulizonazo? Tusikubali kikundi cha wanasiasa wachache na wafuasi wao watuharibie mfumo wetu wa maisha

nguvu tuliyonayo.jpg
 
Kwa nini kikundi cha watu kama 1% (wanasiasa uchwara serikalini) kinafanya maamuzi ya watu 99% (wananchi) tena bila kuzingatia maslahi mapana ya 99% (wananchi) na bado hao wananchi wanakaa kimyaa!
Hii haikubaliki. Kuchukua hatua sasa ni wajibu wetu sote kwa pamoja na kila mmoja kwa nafasi yake.
 
ni kweli. tusikie hoja na sera si vioja na siri. umenena vyema kabisa.:)

Ndugu
zangu,
Wakati wa kampeni za uchaguzi ni wakati
muhimu sana katika jamii yoyote. Ni wakati muhimu kwa sababu jamii
husika hujiandaa kuchagua viongozi wao wa kuwaweka mstari wa mbele
(frontline) katika kukabiliana na changamoto za kimaisha iwe
kijamii, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.
Ni
wakati muhimu kwa wananchi kusikiliza sera za wagombea na kupembua
mchele katikati ya pumba, ni wakati wa kutafuta dhahabu katikati
vipande vya chupa. Je haya ndio yanayoendelea huko
ARUMERU?
Tunashuhudia tambo za kila aina!
matusi ya kila aina! (hata mbele za watoto) badala ya Sera, Sera
zitakazomkomboa mwana wa Arumeru Mashariki. Ndugu zangu, Taifa
hili limejengwa katika misingi ya kuheshimu UTU WA
MWANADAMU
, (Dignity of Man). Je ni nani kati ya hawa
wanasiasa waliopo huko ARUMERU anaweza akasimama na kusema anafanya
siasa zinazoheshimu UTU? Kwa siasa hizi tutafika wapi?
Inasemekana kuwa SIASA ni UCHUMI, na
uchumi wetu ndio huo tena unazidi kuporomoka, hivyo basi ni vyema hawa
wanasiasa walio mstari wa mbele watupatie HOJA zao na si VIOJA vyao,
watupe SERA zao na si SIRI zao, ili wananchi wajue dhahabu ni ipi na
chupa ni zipi, wajue Mchele ni Upi na makapi ni
yapi
. Sasa kama leo wanafanya SIASA za namna hii
(visasi,kuchafuana,chuki,udanganyifu,matusi, ..) tena kwenye
ngazi ya Jimbo tu, je kesho watafanya siasa za namna
gani?
Ewe mwanaJF, mpenda mabadiliko, tena
usiyevutiwa na mtindo huu wa siasa za kupakana matope
ungana nami kuwataka wanasiasa wetu
wafanye siasa safi.
Ewe mwananchi unajua nguvu ulizonazo? Tusikubali kikundi cha wanasiasa
wachache na wafuasi wao watuharibie mfumo wetu wa maisha
View attachment 49591
 
Kwa nini kikundi cha watu kama 1% (wanasiasa uchwara serikalini) kinafanya maamuzi ya watu 99% (wananchi) tena bila kuzingatia maslahi mapana ya 99% (wananchi) na bado hao wananchi wanakaa kimyaa!
Hii haikubaliki. Kuchukua hatua sasa ni wajibu wetu sote kwa pamoja na kila mmoja kwa nafasi yake.

Waulize viongozi wako walioenda Ikulu.
 
Back
Top Bottom