Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,529
- 19,384
..Balozi Elly Mtango alikuwa balozi Geneva, halafu akarudishwa nyumbani na Mzee Mwinyi kuwa PS wizara ya habari. Mzee Mkapa akamteua kuwa PS Mambo ya Nje. Baada ya hapo akateuliwa tena kuwa Balozi Japan.
..Balozi Hassani Kibelloh ndiye aliyempokea Elly Mtango U-PS pale Mambo ya Nje. Wakati Mtango anakwenda Japan, Raisi Mkapa alimteua Dr.Ben Moses na Charles Sanga kuwa Ubalozi.Siyo kweli kwamba Balozi Mtango amekaa Japani miaka 16!
..Mabalozi waliokaa nje muda mrefu ni wa aina ya Gen.Sarakikya, Lt.Gen.Mwakalindile na Lt.Gen.Silas Mayunga "mti mkavu." Hawa ukiwarudisha nyumbani bila kuwastaafisha Jeshi watawasumbua watu kama Waitara,Mwamunyange,na Shimbo.
..Mabalozi wanabadilika siku hizi. Mkapa alipoingia madarakani aliteua Mabalozi kama watano kama wakuu wa idara wizarani. Kituo kama Harare wali-serve Muganda na baadaye Mbita. UN alimbadilisha Mwakawago na Mahiga. India alikwenda Capt.Kiwanuka, halafu baadaye Mama Nzaro. London alipelekwa Prof.Abdul-Kadiri badala ya Col.Mchumo. Hata itifaki alianza na Mwawado, akaja Opanga, akamaliza na Cisco Mtiro.
..Hiyo ni mifano michache tu...Lusekelo amekosea kuzungumzia kiujumla-jumla, bila data, suala kama hili.
Nafikiri swala siyo kwa mabalozi wenyewe ila wale wanaoitwa maofisa wa ubalozi; hawa ndio wanaokaa muda mrefu sana.