Otouh aula UN, Hosea aula au inakuwaje?

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,710
2,226
Unajua huwa ninakwazika sana hao watajwa hapo juu wametukwaza big time mmoja kwenye issue ya Jairo mwengine kwenye issue ya Richmond.

Na Leon Bahati:
UMOJA wa Afrika (AU) umemteua Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), Dk Edward Hosea kuongoza Secretarieti ya Bodi ya Kuzuia Rushwa Barani Afrika.AU pia imeteua makao makuu ya Sekreterieti hiyo kuwa mjini Arusha, ambapo shughuli zake zote zitaratibiwa.

Akizungumzia kuhusu uteuzi huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema ulifanywa na AU katika mkutano wake uliomalizika hivi karibuni mjini Addis Abba, Ethiopia.

Alipoulizwa mambo yaliyoifanya Dk Hossea na Tanzania kupata heshima hiyo wakati ambapo Taifa limekuwa likikabiliwa na misuguano ya rushwa, Membe alisema:

"Uhuru huo wa kuruhusu mijadala ya rushwa nchini ndiyo yanayoijengea heshima Tanzania. Hii inaonyesha uwazi wa mapambano dhidi ya rushwa."Alisema kwamba rushwa ipo sehemu nyingi duniani lakini ni nchi chache zinazotoa uhuru wa wa kuzungumza mambo hayo hadharani kama ilivyo Tanzania.

"Vyombo vya habari vimekuwa huru... Kuwepo kwa mijadala, misuguano, kunatoa fursa ya kuweka sera na mipango ya kukabiliana na rushwa," alisema Membe.

Katika hatua nyingine Membe alisema kwamba AU imeshindwa kumchagua Katibu Mkuu wa Umoja huo baada ya aliyekuwa anatetea nafasi hiyo, Jean Ping wa Gabon kukataliwa kwa kura.

Membe alisema uchaguzi huo sasa utafanyika Julai mwaka huu mjini Lilongwe, Malawi na kuna uwezekano mkubwa wa katibu mpya kutoka katika nchi za Kusini mwa Afrika.Wakati huo huo, Membe alisema kwamba AU imekasirishwa na kitendo cha Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kuwaandama viongozi wa Afrika peke yao, huku wakiwaaacha wa mabara mengine.Kutokana na hali hiyo wametaka ICC ifanyiwe marekebisho ili iweze kuendesha shughuli zake kwa haki duniani.

Source: Mwananchi
 
kishika posti muhimu kwa nchii za kiafrika si kwamba una uwezo.
ASHAROSE ametokea bongo mpaka UN tujikumbushe ni upi uliokuwa ufanisi wake kupelekea JK kumpendekeza kwa BAN MOON???

sofia simba ni waziri ila naamin IQ yake ni ndogo kuliko ya kuku wa kienyeji.
 
Sasa mtu kama Hosea anapewa nafasi ya level ya Afrika kwa rekodi gani ya perfomance aliyoionyesha hata hapa Tanzania tu?
Shida kama wanapewa recommendations toka kwa maafisa wa Tanzania au Rais, basi ujue ni kazi bure!
Sasa imagine mbtu mbovu kama Hosea anaenda kuzuia rushwa gani Africa?...my hairs!
 
kishika posti muhimu kwa nchii za kiafrika si kwamba una uwezo.
ASHAROSE ametokea bongo mpaka UN tujikumbushe ni upi uliokuwa ufanisi wake kupelekea JK kumpendekeza kwa BAN MOON???

sofia simba ni waziri ila naamin IQ yake ni ndogo kuliko ya kuku wa kienyeji.
Duuuu Marytina umeua sn bhana!!!, kwa kifupi naungana na ww yaani viongozi sasaivi huteuliwa kutokana na interest ya mkuu, lakini sio IQ wala ufanisi hilo halina ubishi kabisa?
 
Ninaanza kuhisi usikute JK ndo anatoa recommendation ya hao watu.
Sasa hao wanaopitisha majina hawafanyi hata homework!
Usikute wanamwamini JK kama Raisi Tz so hawezi waingiza chaka kumbe ni kinyume chake
 
Kwa kumchagua Hosea, inaonyesha ni jinsi gani Africa hatuko serious na rushwa.

Anyway, jamaa wana akili kweli!! Katika nchi zote wakaona ni Bongo ndiko wanaweza kupata mtu wa kubangaiza na kuigiza kuwa wanapambana na rushwa. Kazi aliyoifanya PCB ya kufunika na kupiga danadana kesi za rushwa inaelekea zimewafurahisha sana AU. Sasa wameona inabidi awasaidie huo utaalamu. Si unajua tena, hakuna kiongozi Africa aliye serious na rushwa!! Kama wangekuwa serious, there is no way Hosea angeteuliwa!!!
 
Duuuu Marytina umeua sn bhana!!!, kwa kifupi naungana na ww yaani viongozi sasaivi huteuliwa kutokana na interest ya mkuu, lakini sio IQ wala ufanisi hilo halina ubishi kabisa?
Hiyo ni kweli kabisa na imefanya Tanzania kuonekana nchi isiyo na watu makini,kwani mara nyingi waliowekwa kwa interest za mkuu,wamevuruga sana mf Mongela,hata Migiro hajafanya la maana ndo maana Ban kampiga BAN ingawa kuna muhula mwingine iliwezekana kupewa.
 
Kwa kumchagua Hosea, inaonyesha ni jinsi gani Africa hatuko serious na rushwa.

Anyway, jamaa wana akili kweli!! Katika nchi zote wakaona ni Bongo ndiko wanaweza kupata mtu wa kubangaiza na kuigiza kuwa wanapambana na rushwa. Kazi aliyoifanya PCB ya kufunika na kupiga danadana kesi za rushwa inaelekea zimewafurahisha sana AU. Sasa wameona inabidi awasaidie huo utaalamu. Si unajua tena, hakuna kiongozi Africa aliye serious na rushwa!! Kama wangekuwa serious, there is no way Hosea angeteuliwa!!!
jamani eh... Hizo position ni za maagano, kama vile kupokezanavijiti. Zamu imefika
 
Ninaanza kuhisi usikute JK ndo anatoa recommendation ya hao watu.
Sasa hao wanaopitisha majina hawafanyi hata homework!
Usikute wanamwamini JK kama Raisi Tz so hawezi waingiza chaka kumbe ni kinyume chake

sijaelewa kwa kiingereza kipi JK aandike reference nzito kama hizi...we umeona barua aliyoandika kwa yule mama wa world bank?? ungezimia ..hata mwanangu gaude yuko shule ya upili hawezi kuandika vile ..yaani yalikuwa ni mautumbo ya bata
 
Ninaanza kuhisi usikute JK ndo anatoa recommendation ya hao watu.
Sasa hao wanaopitisha majina hawafanyi hata homework!
Usikute wanamwamini JK kama Raisi Tz so hawezi waingiza chaka kumbe ni kinyume chake

Mkuu, kama hujui vile!? Hii ni fadhira ya JK kwa hao mabwana na fadhira haijali competence ya mtu
 
Duh! Yaani kwa kuruhusu mijadala ya wazi kuhusu rushwa ndio kigezo cha Hosea kuonekana anafanya kazi nzuri?!

Hakika hiyo post amependekezwa na mabogus wenzake.
 
Tanzania has a reputable and honourable outlook in the outside world than anyone could believe. Our reputation goes back in the pre-independence era when we dedicated a huge amount of efforts to actively help our neighbours free themselves from colonialism. We can keep on playing down the status of our nation but that can't stop others from viewing us as the most democratic and liberal land in Africa. Though its true that to some extent our inept political and government leaders have failed to take advantage on this honour accorded to us by an international community.
 
kishika posti muhimu kwa nchii za kiafrika si kwamba una uwezo.
ASHAROSE ametokea bongo mpaka UN tujikumbushe ni upi uliokuwa ufanisi wake kupelekea JK kumpendekeza kwa BAN MOON???

sofia simba ni waziri ila naamin IQ yake ni ndogo kuliko ya kuku wa kienyeji.

Duh! ama kweli umemchoka huyu mama yaani IQ sawa ya kuku?
 
Yaani nikiangalia RADAR,Richmond etc yaani sioni ata chembe ya useriousness na rushwa apa.
Rushwa in Africa is too serious to be left to Hosea
 
Back
Top Bottom