Oscar Pistorius ampiga risasi mpenzi wake

Oscar Pistorius ampiga risasi mpenzi wake

rosemarie

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
6,887
Reaction score
3,441
Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, anahojiwa na polisi kufuatia mauaji ya mpenzi wake nyumbani kwake mjini Pretoria.
Kulingana na vyombo vya habari, mkuu wa polisi, Sarah Mcira, aliambia wanahabari kuwa mwanamke aliyefariki nyumbani kwa mwanariadha huyo alipigwa risasi kwenye mkono wake na kichwani.
Hata hivyo hali iliyosababisha mauaji hayo bado haijulikani. Duru zinasema kuwa Pistorius huenda alimuua mwanamke huyo kimakosa kwa kudhania kuwa ni mwizi aliyekuwa amemvamia.
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 26, alikuwa mwanariadha wa kwanza mlemavu kushiriki michezo ya Olimpiki.
Afrika Kusini ni moja ya nchi zenye visa vingi vya uhalifu duniani na watu wengi wanamiliki silaha za kujilinda.View attachment 83155
 
Duh! Valentine zingine ni noma. Sujui kama jamaa alikusudia au ndio bahati mbaya..............kwani yote yanawezekana.😕
 
Huo wote ni uoga utapigaje risasi bila kumjua adui? Ashtakiwe kwa uzembe na kunyimwa kumiliki silaha.
 
Oscar na mpenzi wake
reg_634.Oscarstorius.ReevaSteenkamp.jlc.2012.jpeg
 
Hiyo ndio FALL FROM GRACE. Ingekuwa kule kwetu Somalia, adhabu yake imgekuwa kuenguliwa mikono kwa kosa kama hili
.
 
Back
Top Bottom