Orphan Black na power ya casting na character

marcoveratti

JF-Expert Member
Sep 21, 2017
967
1,692
Kama ni series bora basi naweza kuitaja Game of thrones,Prison break na 24 au Once upon a time ya mheshimwa Rumple stiltr skin na hii ni kutokana na mpangilio wa story matukio ubora wahusika uwekezaji na mambo kadha wa kadha,,
ila kama ni series ambayo imenifanya nione ni namna gani charater na cast in nguvu kwenye Movie ama series basi wala sita waza Orphan Blaack haina mpinzani kwenye hili.

Ni series ya Canada ilikua ina rushwa ABC america kuanzia mwaka 2014 na baadae ikachuliwa na Netflix ilipofika season 4,
aslimia zaidi ya 80 ya watu nilio wa recomend wakaangaliae hii series walikujua na mrejesho kua ni series mbaya haileweki na haina mvuto.

Sijawahi kushangaa sababu naelewa kuna series za kila mtu kama ilivyo squid game,MOney heist pia kuna sries za watu wachache kama LOKI, Person of interest pamoja hii kutoka na interest knowledge na attitude.

Humo ndani kuna mwanadada anaitwa Tatiana Maslany ambae kapiga character 17 tofauti ndani series moja alaf kama hakija tokea kitu yani!

Main character ni moja ya cast ya Tatiana anae tumia jina la Sarah Minning.
wengine ni Kasima, Helena, Beth Childs ,Katja Obinger, Aryanna Giordano, Janika Zingler, Janika Zingler, Alison Hendrix, Rachel Duncan, M.K., Jennifer Fitzsimmons, Krystal Goderitch, Tony Sawicki, Miriam Johnson, Camilla Torres na mmoja hakua na jina alikuja kuonekana season ya 5 hawa wote ni Tatiana ila amecast tofauti tofauti ndani ya Orphan black.

kilicho nivutia ni namna mwanadada Tatiana anavyo vaa uhusika wa character wote17 kwenye series moja kiasi kwamba mtazamaji unaona kabisa wahusika wana tabia, vibe na muonekano tofauti licha ya kua mtu mmoja.

kwa ufupi story ya Orphan black ni Science Fiction ya Human Cloning, inaaminika hii Tecnolojia ipo ila kwa mtu Ordinaly kama mimi bado ni fiction.

Kinachomkuta Saraha minning ni kwamba anakutana na binadamu anayefanan na yeye kwa 100 kabala haja mhoji chochote anaparamia treni anakufa.

Hapo ndio ana naza kukutana clones wake wengine ambao anafanana nao kwa asilimia mia na kuanza kutafuta ukweli nini kulicho nyuma ya pazia mpaka wafanane hivi wakati huo huo clones hao wanawindwa wapotezwe.

Sio sries bora kama ukiitazama kwa ubora tofauti na castng ila ni series bora kwa kile kinacho ifanya kua ya kipekee ORHAN BLACK humo ndani namuelewa zaidi Helena ni clone alie kua akictrainiwa kuua maisha yake yote na kukulia UKRAIN.

1650146799450.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom