Orodha ya maamuzi yaliyoliangamiza taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Orodha ya maamuzi yaliyoliangamiza taifa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mbogela, Jul 1, 2009.

 1. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Wana JF nimeona uchambuzi umefanyika huko GP.
  Nilipoangalia orodha ya hayo maamuzi yaliyowekwa sidhani kama yamewekwa kwa usahihi. Naona kama maamuzi muhimu makubwa yanayolitia hasara taifa hili au kulifanya liwe kama lilivyo hayajasemwa au hajapewa umuhimu na kipaumbele. Kwa vile hapa ndipo jamvi la great thinkers of the time wanakutana nikaona niazime hii hoja na kuileta hapa.

  Je unadhani ni nani lini alitoa uamuzi (Utaje) ambao unaweza kusemwa ni uamuzi mbovu (wa hovyo hovyo) ambao uliingiza taifa letu na watu wake matatani wakati huo, au ni uamuzi ambao umetuletea au unatuleta hasara mpaka leo. Je kwenda vita na Idd Amin ulikuwa uamuzi mzuri? Azimio la Arusha? Kuipa TICTs container terminal? Kujenga Uwanja wa Mpira mkubwa wa kisasa? Kutanua njia? Kupiga marufuku mabasi kusafiri usiku? Ebu tufikirie kwa mapana zaidi, ningependa kutoa list ya maamuzi 100 mabaya yaliyowahi kufanywa aidha na kiongozi kama yeye au serikali, Bunge mahakama au chombo chochote cha dola ambayo yameitia nchi hii hasara. Tusaidiane kutengeneza list
   
 2. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kuwapa wabunge ukuu wa mikoa. Siasa na serikali wapi na wapi?
   
 3. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Operation vijiji,huu uamzi ulitolewa miaka ya 1970,ilileta umaskini mkubwa na kusababisha vifo maana watu walibebwa na kutupwa maporini kuanzisha vijiji vya ujamaa.
   
 4. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Nani alifanya uamuzi huu? wengine wanasema alikuwa JKN, wengine wanasema ilikuwa kamati kuu ya TANU, wengine wanasema sera kama sera haikuwa mbaya lakini utekelezaji na usimamizi chini ya PM simba wa Vita Mfaume Rashid Kawawa ndio lilikuwa tatizo. Unasemaje?
   
 5. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  MAAMUZI YALIFANYWA NA UONGOZI ULIOKUWA MADARAKANI CHINI YA NAHODHA MWL JKN NA MSAIDIZI WAKE MKUU BWANA RASHIDI.
  UTEKELEZAJI WAKE ULIKUWA WA KUKURUPUKA PASIPO MAANDALIZI.
  WANANCHI HAWAKUPEWA NAFASI YA KUTOA MAONI WALISOMBWA KWA NGUVU.
  nADHANI HILI NDO LIMETUFIKISHA MAHALA AMBAPO HADI LEO VIONGOZI WETU HAWASHIRIKISHI WANANCHI KATIKA MAAMUZI.
   
 6. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Nasikia kuna watu waliliwa na simba, pia nasikia watu waliacha mazao yao mashambani huko walikohamishwa hasa mazao ya kudumu kama minazi na mogomba na miti ya matunda mbali mbali. Je kuna document yoyote inayoonyesha hasara za hili kama vile watu waliokufa kwa maralia kwa kulala nje na kungátwa na mbu? watoto walioshindwa kwenda shule ili wasaidie mama zao (wajane mfano) kujenga nyumba mpya huko walikohamishiwa?
   
 7. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Mbogela
  kama jina la operation linavyo jieleza waadhilika hasa walikuwa wana vijiji,ni kweli waliacha mazao yao ya kudumu kwani walihamishwa kupelekwa maeneno ya mbali na makazi yao ya awali. Magari yaliwasomba bila kuwasafirishia mazao yao wengi waliadhirika na njaa,wengine waliliwa na simba kwani hawakuwa na nyumba za kuwaweka mtu alitupwa nje kwenye kiwanja alichopewa alitengeneza kibanda cha muda vingine havikuwa imara vikawezesha wengine kuchomolewa na simba.wengine waliachwa nje huku mvua kubwa zikinyesha hapo haijalishi una mtoto mchanga/mdogo sana.Viongozi wa operation kazi yao ilikuwa kuhamisha mengineo hawana habari kwani wao wame accomplish mission yao.
  Kama nilivyotangulia kueleza mambo haya yalifanyika vijijini naunajua uwezo wa kuelewa na kuweka kumbukumbu kwa wanaikijiji.Hivyo waliomboleza kivyao na kubakia kimya.Mfano mzuri na kwa mtu anayetaka kufanya research/utafiti wa madhara haya Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa iliyoadhilika sana na operation hiyo.
   
 8. O

  Ogah JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ELIMU
  1. Matumizi ya lugha kwenye elimu........kiswahili std 1 mpaka std 7...kuanzia hapo form I kwenda juu kiingereza
  2. Waziri Mungai Kupiga marufuku michezo mashuleni
  3. Waziri Mungai kubadilisha mitaala ya elimu ya msingi na kufuta baadhi ya masomo
  4. Crush program za ualimu
  5. Upunguzaji wa Bajeti ya Elimu kwa ujumla.....mwaka hadi mwaka

  NATURAL RESOURCES
  kuruhusu Mikataba mibovu mibovu isiyo na faida/tija kwa wananchi............i.e....sekta ya Madini na Nishati

  SERIKALI KUBWA na matumizi yake
   
 9. D

  Dr.Mbura Senior Member

  #9
  Jul 1, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tumshukuru Mungu kwani wakati wa vijiji vya ujamaa kulikuwa hakuna ukimwi maana watu wengi wangekufa, kuingiliana kulikuwa inje inje.
   
 10. O

  Ogah JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Karibu sana Dr.Mbura
   
 11. D

  Dr.Mbura Senior Member

  #11
  Jul 1, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Asante sana mkuu Ogah
   
 12. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Nani alipitisha uamuzi huu? Lini?
  Lakini wanaoukingia kifua wanasema ili kuwa nataifa moja (kama tulivyosasa) lisilo na ukabila na ilikuwa muhimu kuwa na lugha moja yneye ubantu ndani yake na pia kufuta uchifu/utemi. Leo hiii kila mtanzania anajisifu kwa kuwa matanzania asiye weka mbele ukabila wake. Mkuu huoni kama Faida zinazidi hasara? Kwani kutumia kiswahili kufundishia kumelitia taifa hasara gani?
   
 13. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #13
  Jul 1, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Doc mimi nadhani watu hupenda/hufanya ngono wakiwa kwenye amani na starehe, kulikuwa na amani gani wakati huo? na kwa ujumla wakati huo wakaka walikuwa sio wa kujieleza kama sasa na walikuwa wanasubiri wakimpenda mtu ni wa kuooa, wadada walikuwa sio watoaji wa kufuli (wengi hawakuvaa huko vijijini) kinadharia kirahisi kiasi hicho
   
Loading...