Orodha ya Benki za Kitanzania nchini Kenya

Orodha ya Benki za Kitanzania nchini Kenya

Mkuu UCHUMI walishasanda game mbn [emoji39] [emoji39] [emoji39]
Uchumi wamesanda kwa hapa bongo na uganda baada ya kutofanya vizuri lakini huko Kenya bado wana~operate vizuri sema tu hawana ushindani na Nakumatt kivile washindani wakubwa wa Nakumatt sasa hivi ni Naivas na Tasky's
 
Hakuna,hata benki zetu hapa nyumbani zinaitwa benki za wapiga dili na mkuu amezinyanganya fedha zilizokuwa zimehifadhiwa huko labda ana lengo la kuziua benki hizo

Hongereni kenya nyie hamna roho ya korosho
 
Sisi,watanzania tulikua tunafursa ya kufundisha kiswahili katka vyuo vikuu,Uganda,Kenya,Congo,rwanda,Burundi,lakin tumeshindwa.nilienda kituo kimoja Uganda wanafundisha lugha za kigen,kikiwemo na kiswahili,lakin anayefundisha kiswahili hapo sio mtanzania ni mganda.
 
Walete vyote ila watuletee na kale ka waziri kao ka mambo ya nje.kale ka mama mmewe anafaid sana asee
 
Waganda na Wakenya wamefungua matawi ya vyuo vyao vikuu huku kwetu (KIU, JKUAT) sisi sijui kama tuna chuo kikuu chetu chenye tawi Kenya au Uganda. TZ ni mabingwa wa kuongea, kubishana, kudanganyana, kujidai, bila mkakati kuanzia kwenye siasa, uchumi hadi michezo!!!!!
 
Tunao Wawekezaji (wauza mitumba) pale Nairobi-soko la Gikomba, pia tunao ndugu zetu (Ombaomba) waliotapakaa miji mingi kama Kisumu, Nakuru, Eldoret, Nairobi au Mombasa. Bahati mbaya.....
 
Bado watanzania benki zetu hazijawekeza Kenya ingawa wakenya wame~invest huku kwetu sana. Na sio KCB na Equity tu ndio wako huku akina Nakumatt na Uchumi supermarket ni wakenya pia so nadhani ni wakati mwafaka watanzania kujitanua, kufungua matawi na kuwekeza kwa jirani zetu pia.
NIA TUNAYO..., SABABU TUNAYO....., UWEZO TUNAO

Advantage wanazopata bank za kenya ni kua kampuni nyingi za kenya zimewekeza hapa nchini hivyo ni rahisi sana kwa hizo kampuni kupata huduma za kibank ktk bank za kenya.sasa ss hakuna kampuni tulizowekeza kenya tutawezaje kufungua bank huko!?tutapata wateja ndio lkn si kwa kiwango cha kupata faida.

Angalia kampuni karibia zote za bima,consultancy,marketing,advertising nk ni za wakenya bado wafanya kazi kibao ni wakenya hivyo wakiwa ile kauli penda cha nyumbani lazima bank zao zishamiri.
 
sio kila kampuni iliyowekeza hapa TZ ni ya wakenya kisa tu hiyo kampuni Kenya ipo pia wawekezaji wametoka huko abroad ila wameanzia Kenya na nchi nyingine ndio wamekuja huku kwetu
kukariri si vizuri
Mfano wako ni upi sasa maana zinazoongelewa ni za Kenya
 
Mi nadhani si jambo la kujishusha kwakuwa tu hatujawekeza nchi jirani, kwanza ni sera nzuri kujiimarisha ktk soko la ndani kabla ya kuvuka mipaka. Mfano, hadi sasa kuna wilaya hazina huduma za kibenki kwanini sasa benki zetu zivuke borders?

Nakumbuka hotuba moja ya Hitler, ktk alichokijivunia ni idadi kubwa ya wajerumani hivyo kuwa na uhakika na soko lake la ndani. Soko la ndani ni la uhakika zaidi na kwa East Africa sisi ndo wenye watu wengi.

Ikumbukwe makampuni ya ubia miaka ya EAC yalivyotuharibia kwa mali zilizokuwa ndani ya Kenya, sisemi tusiwekeze huko ila kama la ndani lipo, hakuna haja ya kuvuka borders.
 
Back
Top Bottom