Orodha Rasmi ya Watu wanaokaa Mtandaoni Muda mwingi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,884
Wakuu Kwema!

Kuna kasumba moja ambayo watu wasiotumia akili Yao kuchambua mambo wapo nayo, kasumba hiyo ni kudhani watu wanaoshinda Mtandaoni hawana kazi Jambo ambalo sio Kweli.

Lazima watu waelewe kuwa, Mtandaoni huwezi ingia pasipokuwa na Bundle, na wote tunajua Bundle ni pesa, Nani asiyejua kuwa vifurushi vimepanda kiasi kwamba Kwa mtu mwenye matumizi ya kawaida Mtandaoni itampasa atumie elfu 2 Kwa siku ambayo Kwa mwezi ni elfu 60.

Tuachane na hayo, ifuatayo ni orodha Rasmi ya Watu wanaoshinda Mtandaoni mara nyingi zaidi;

1. Wafanyabiashara hasa wa maduka, na supermarket,
Wafanyabiashara hupageuza Mtandaoni Kama sehemu Yao ya ku-refresh, kuondoa upweke, kupiga Stori, kuuza bidhaa zao n.k.
Kwa ambao wanauza maduka ya nguo katika majiji na miji watakubaliana na Mimi kuwa muda mwingi huwa wapweke,

Ninauzoefu na Jambo hili, unakuta unakaa karibu masaa matatu hakuna mteja anayekuja dukani kwako, hivyo Kama huna bando wengi hujikuta wanalala ofisini.

Ukifika Kariakoo, au maduka mengi yaliyopo Sinza, Kinondoni, Tabata nafikiri na miji mikubwa Tanzania Asilimia kubwa ya wauzaji utawakuta aidha walikuwa wanachezea simu Mtandaoni, wachache wamepitiwa na usingizi, baadhi wakicheza gemu.

Vibanda vya M- Pesa, tigo na airtelmoney pia utawakuta Wafanyabiashara wakitumia mitandao ya simu.

Hivyo kusema mtu kusema mtu asiye na kazi ndio anashinda Mtandaoni anapaswa afikiri vizuri.

2. Wanachuo wa elimu ya juu kabisa.
Waliofika elimu za juu watakubaliana na Mimi kuwa, kuna kipindi Chuo kinaboa mno, kusubiri vipindi vilivyoachana Kwa masaa karibu matatu mpaka manne kunachosha, wote tunajua kuwa wengi wetu tunasoma nyakati za mitihani tuu.

Hivyo wanachuo wengi muda mwingi huutumia Mtandaoni kujivinjari, wengine kupost picha, kurekodi video, kuperuzi, wengine kuangalia video za ngono, wengine Jamii forum, basi ilimradi kufukuza Upweke.
Wasio na bando au simu kubwa wengi wao hulala kwenye hostel wakiomba wamalize Chuo tuu waondoke.

Chuo kinachosha Kama hauna simu kubwa au laptop, pia kama hauna Bumu, na kwenu ni apeche Alolo.

3. Wamiliki wa makampuni,
Wakurugenzi Wakuu WA makampuni wasio na majukumu mengi muda mwingi hupitia Mtandaoni kupoteza muda, huku wakisubiri ripoti ya Miradi inavyoendelea.
Mara chache kutokana na umri wao wengi wao kuwa mkubwa hujikuta wakipitiwa na usingizi.

4. Wabunge
Ni kawaida Sana kuwakuta wabunge wawapo bungeni wakiperuzi peruzi Mtandaoni Kama hawana chakuchangia bungeni, au hata wakiwa nje ya Bunge hutumia mitandao ya kijamii kutafuta habari za hapa na pale zitakazowasaidia katika kujenga hoja bungeni, au kujijenga Kisiasa.

5. Madalali na Mawakala
Madalali wa magari na nyumba wengi wao hushinda Mtandaoni kwani huko ndio hutangaza bidhaa na Huduma zao,
Sio ajabu mitandao ya Instagram, Facebook n.k ikiwa na matangazo mengi ya bidhaa na Huduma kutoka Kwa madalali na mawakala wa bidhaa au Huduma Fulani.

6. Wasanii
Wasanii wa Muziki na bongo Flava, ni moja ya watu wanaoongoza kukaa muda mwingi Mtandaoni, Kwanza wao ndio wanahakikisha kila muda wanapost chochote ili wasisahaulike.
Hushinda Mtandaoni kujivinjari, kujidai na kujigamba, kuburudisha na kuwafurahisha wafuasi wao n.k

7. Wachungaji
Hawa ni moja ya makundi ambayo muda mwingi huutumia mtandaoni kwaajili ya kuwahudumia wateja wao.
Wapo wachungaji wa Mtandaoni tuu pasipo Physical Address na wapo walio na Physical address.

8. Malaya
Hawa hushinda Mtandaoni Kwa lengo la kupata wateja, huposti picha za kimitego kunasa mawindo Yao. Wakishapata huwahudumia wateja wao huo ndio muda huwa-, offline.
Lakini wapo ambao hutoa huduma za online sex Kwa kuwaunganisha wateja wao kupitia video call na kupata kipato.
Kama hiyo haitoshi, wapo Malaya ambao huruma picha dm na kuwaomba wateja wao angalau elfu 2 tuu za kujiunga kifurushi, hata hivyo baadhi ya hawa huwa ni wanaume wanaojipa utambulisho wa kike.

10. Wanaharakati waliomaliza Chuo hawana Ajira.
Hili ni kundi ambalo siku Kwa siku linakua, na linapata idadi kubwa Mtandaoni kujifanya wanaharakati wa kuipinga SERIKALI, kupinga Jambo lolote lile ilimradi kupinga.
Kundi hili lipo zaidi Mtandao wa Jamii Forum kutokana na kupewa Utambulisho bandia, lipo pia Twitter, na Facebook.

Hawa hupata pesa kwenye vibarua mshenzi ambavyo huwasaidia kujiunga bando.
Mtandaoni ni sehemu Yao ya kupoteza muda, kuondoa upweke na wakati mwingine kutoa dukuduku na sumu ya maisha magumu wanayopitia.

Sifa Yao Mtandaoni ni kujifanya kila kitu wanajua, hasira zisizo na maana zinazowafanya wanatukana tukana hovyo kila mtu.

11. Wasio na kazi na hawana Elimu.
Hili ni kundi dogo Sana ukilinganisha na makundi mengine hapo juu.
Kundi hili ni wachache wenye smartphone, na hao wachache hawana pesa ya kujiunga bando kutokanà na kutokuwa na kazi yoyote Ile.

Kundi hili Mtandaoni uhusika wake ni kupost picha zao, ku-like na ku-share post za watu mashuhuri wanaowakubali.

Kundi hili ni bendera fuata UPEPO,
Na linapendelea zaidi endapo watu wajuu Yao kiuchumi au kielimu wakihenyeka. Sio ajabu kundi hili kuwa ni Wafuasi waaminifu wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano.

Ndio maana Mtandaoni utakuta Watu wanaiponda Serikali na kumzingua JPM lakini mtaani Hali ni tofauti kabisa Kwa sababu kundi hili wapo wengi zaidi mtaani kuliko Mtandaoni.

Na hiyo ndio orodha ya watu wanaoshinda Mtandaoni Kulingana na kukaa kwao muda mrefu Mtandaoni.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Umemsahau Robert Heriel.
 
Back
Top Bottom