Orijino Komedi ya TBC1

Mjanga

JF-Expert Member
Feb 13, 2011
1,238
324
kundi hili linafanya vizuri sana katika tasnia ya ucheshi hapa Bongo,lakini wadau naomba kuuliza hivi watoto wetu ambao ni mashabiki wakubwa wanajifunza nini? hasa pale wanapoporomosha matusi ""mfano JIBWA, NYOKO na mengine mengi tu! imekua kero badala ya Burudani! wadau mnalongaje!
 
ni ngumu kuzuia watoto, maake muda wenyewe ni mbaya!
 
Ni kosa kubwa sana kuwaruhusu wanao kuanagalia kundi hili ambalo kwalo matusi ndo uchekeshaji, wameishiwa siku hizi na kuendekeza matusi ni sababu nyingine ninayokushauri uangalie Mizengwe kila jpil ITV angalau wanajua kile wanachokifanya na hakihitaji kuwa rated
 
Hivi bado hiyo comedy ipo? House girl wangu basi ndiye huwa anaifaidi!
 
wasipoangalia watafulia vibaya! naona wanaanza kulitia maji tembo!
cjui baraza la sanaa wanafanya kazi gani?
 
Ulilinganisha na wengine wale wako juu! ila matusi kweli siyo mazuri watoto sasa hivi wataanza kutukana jibwa etc.
 
kweli kabisa!

Ni kosa kubwa sana kuwaruhusu wanao kuanagalia kundi hili ambalo kwalo matusi ndo uchekeshaji, wameishiwa siku hizi na kuendekeza matusi ni sababu nyingine ninayokushauri uangalie Mizengwe kila jpil ITV angalau wanajua kile wanachokifanya na hakihitaji kuwa rated
 
wako juu lakini kwa matusi haya wataaanza kuporomoka!
jana tu mtoto baada ya kuangalia akaanza kuyaporomosha... ilikuwa so!

Ulilinganisha na wengine wale wako juu! ila matusi kweli siyo mazuri watoto sasa hivi wataanza kutukana jibwa etc.
 
wako juu lakini kwa matusi haya wataaanza kuporomoka!jana tu mtoto baada ya kuangalia akaanza kuyaporomosha... ilikuwa so!
Baada ya mtoto kuanza kuyaporomosha ulimchukulia hatua gani?? Unajua wazaz wa siku hz mnalealea watoto kizembe sana, kudekeza kwingi utafikiri ye ndo mzaz wako. Kwa mzaz wangu mimi haikuwa rahs kumsikia mtoto akisema tusi hata kma kalicopy sehem. Sasa ww mtoto anaporomosha matus ya Zeko na we upo, hii inaleta picha gani?? Umedekza huyo mtoto, vinginevyo asingethubutu kufanya hivyo. Sisemi kwamba hujui kulea ila usiache comed wakulelee mtoto.
 
we nani mshabiki labda mtoto wako wewe mi nilishapiga marufuiku nyumbani kwangu huwa naangalia ya Channel 10 na EATV. Hawa toka Muhando aondoke sitaki tena

kundi hili linafanya vizuri sana katika tasnia ya ucheshi hapa Bongo,lakini wadau naomba kuuliza hivi watoto wetu ambao ni mashabiki wakubwa wanajifunza nini? hasa pale wanapoporomosha matusi ""mfano JIBWA, NYOKO na mengine mengi tu! imekua kero badala ya Burudani! wadau mnalongaje!
 
Ze Comedy kwisha. Kila jambo na enzi yake. Huwezi kupingana na wakati... Hawana jipya hawakusoma alama za nyakati mapema. Binafsi nilijitahid kupitia barua pepe yao kuwashauri waweke sura mpya tangu wakiwa EATV hawakujali, sasa watu wamewachoka wamebaki kutapatapa. Na bado.
 
Back
Top Bottom